Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afya: Jinsi ya kugundua saratani ya urithi na aina ya matibabu unayohitaji
Hansa Nandini ambaye ameshiriki kwenye filamu kama 'Attarintiki Daredi' na 'Mirchi', amefichua kupitia mitandao yake ya kijamii kuwa amekutwa na saratani ya matiti.
Katika ufichuzi huu anasema jinsi amepambana na ugonjwa huo. Aliandika kuwa saratani yake ilitokana na mabadiliko ya jenetiki na ina uwezekano wa asilimia 70 wa kuibuka tena hata baada ya matibabu.
Iwapo unataka kujua kuhusu saratani ya jenetiki, unahitaji kujua kuhusu Angelina Jolie.
Mcheza filamu huyu nyota wa Hollywood alitolewa matiti yote mawili muda mfupi kabla ya kukutwa kuwa na saratani ya matiti. Alifanya uamuzi huu baada ya mama yake kufariki kutokana na saratani.
Angelina alikutwa kuwa na jeni aina ya BRCA-1 kwenye mwili wake baada ya kifo cha
Alifanyiwa upasuaji wa matiti na kizazi mwaka 2013 baada ya kukutwa kuwa na uwezekano wa asilimia 87 wa kuugua saratani ya matiti na asilimia 50 ya kuugua saratani ya kizazi.
Kulingana na nakala iliyochapishwa mwaka 2016 na chuo cha Harvard, ni kuwa asiliamia ya watu wanaofanyiwa vipimo vya jenetiki imeongezeka tangu Angelina alipofanya uamuzi huo.
Saratani ni nini?
Saratani hutokea wakati seli hugawanyika bila ya udhibiti. Wakati mwili unapoteza udhibiti wa mgawanyiko wa seli, huwa unatokea kama aina ya saratani, anasema Dr Murali Krishna mtaalamu wa magonjwa ya saratani kutoka Visakhapatnam.
Kuna aina nyingi za saratani zikiwemo ya matiti, tumbo, ya matumbo, ya kizazi, na mapafu.
Saratani ya mattiti ndiyo hugunduliwa sana miongoni mwa wanawake nchini India.
Satani ya matiti inapimwa kwa njia gani?
Njia ya kutafuta ugonjwa bila ya kutumia dalili inaitwa 'screening'.
Vipimo kwa njia ya 'screening' kutambua saratani ya matiti inajukana kama mammogram.
Ni vyema kuomba ushauri wa daktari iwapo kuna mabadiliko ya sura au ukubwa wa matiti, ikiwa titi ni ndogo sana, kama kuna damu au maji yenye rangi yanayotoka kwa titi, au kama kuna mabadiliko ya rangi ya ngozi.
Wanawake wote walio na umri wa zaidi ya miaka 40 wanashauriwa kufanyiwa vipimo vya mammogram kila baada ya miaka miwili. Inapendekezwa kuwa mamogram zinastahili kufanywa mara moja kila mwaka au mara moja baada ya kila miaka miwili.
Dkt. Yugandhar Sharma ansema kuwa ni rahisi kutambua uvimbe kwenye mkono.
Dkt. Muralikrishna anasema mtindo wa maisha, tabia ya kula, familia na mabadiliko ya homoni vinweza pia vinaweza kusababisha saratani.
Mabadiliko ya jenetiki ni nini?
Kuna aina nyingi ya jeni kwenye miili yetu. Mabadiliko yanaweza kutokea kwa jeni hizo.
Dr Yugandhar anaeleza kuwa iwapa mabadiliko haya yatatokea kwa jeni za BRCA1,2 mwili wa mgonjwa aliye na saratani ya matiti, inaweza kutajwa kama saratani ya urithi.
Iwapo mabadiliko ya jeni ya BRCA1,2 yanajulikana kuwepo, kuna uwezekano wa alimia 60 hadi 80 ya mtu kuwa na saratani ya matiti na asilimia 30 hadi 40 ya saratani ya kizazi.
Dr Muralikrishna anasema makadirio yanaonyesha kuwa asilimia 5 hadi 10 kwa kila watu 100 walio nchi zilizostawi wana saratani ya urithi
Vipimo hivi vinafanyiwa wagonjwa wote walio na saratani?
Dr Yugandhar anaeleza kuwa vipimo havihitajiki kufanywa kwa wagonjwa wote wa saratani na mara mgonjwa anapokutwa na saratani ya matiti, ni vyema aanze matibabu.
Wakati huu ni muhimu kujua umri wa mgonjwa, aina ya saratani, imefikia kiwango gani na pia historia ya familia.
Jamaa za mgonjwa( mama, dada, baba, binti, shangazi pia wanastahili kuangalia historia ya familia kuamua iwapo watahitaji vipimo vya jenetiki.
Matibabu yanafanywa kwa njia gani?
"Kuna tofauti ya matibabu baina ya watu walio na saratani ya kawaida na wale walio na saratani yenye mabadiliko ya jenetiki," anasema Dr Yugandhar.
BRCA anasema ni bora kuondoa mattiti yote mawili na ovari kwa wale ambao wamekutwa na saratani ya jeni aina ya 1 na 2,
Angelina Jolie ansema iwapo saratani iliyogunduliwa mapema haikkuwa imesambaa kwenda sehemu zingine za mwili, hatari ya saratani inapungua.
Madaktari Yugandhar na Muralikrishna pia wanasema kuwa matibabu ya saratani yenye mabadliko ya jenetiki ni makubwa kuliko ya saratani ya kawaida.
Hansa Nandini aliandika kwenye mitandao kuwa, "ugonjwa huu hautatawala maisha yangu, nitaupiga vita kwa tabasamu na nishinde, nitaibuka tena na nguvu mpya."
"Haijalishi na changamoto ngapi maisha matarusha, sitaki kuwa muathiriwa, Sitaruhusu hofu iathiri maisha yangu, nitapigana, nitasonga mbele kwa mapenzi na ujasiri."