Wafanyakazi wanaoogopa kupoteza kazi zao kwa teknolojia ya akili ya bandia

Chanzo cha picha, Getty Images
Wafanyakazi wengi wana wasiwasi kwamba teknolojia ya akili bandia (AI) inakuja kuchukua kazi zao. Je, tunaweza kuondoa hofu hii na kupata njia bora?
Claire amefanya kazi kama Afisa mauhusiano (PR) katika kampuni kubwa ya ushauri, iliyoko London, kwa miaka sita. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 34 anafurahia kazi yake na anapata mshahara mzuri, lakini katika miezi sita iliyopita, ameanza kuhofia mustakabali wa kazi yake. Sababu: akili bandia.
"Sidhani kwamba ubora wa kazi ninayotayarisha unaweza kulinganishwa na mashine kwa sasa," asema Claire, ambaye jina lake la ukoo linahifadhiwa ili kulinda usalama wake wa kazi.
"Lakini wakati huo huo, ninashangazwa na jinsi ChatGPT imekuwa ya kisasa kwa haraka. Ipe miaka michache zaidi, na ninaweza kufikiria kabisa ulimwengu ambao roboti itafanya kazi yangu vizuri kama mie. Sipendi kufikiria hilo linaweza kumaanisha nini kwa ajira yangu.”
Katika miaka ya hivi majuzi, huku vichwa vya habari kuhusu roboti zinazoiba kazi za binadamu vikiongezeka - na jinsi zana za kuzalisha za AI kama ChatGPT zinavyopatikana kwa haraka zaidi - baadhi ya wafanyakazi wanaripoti kuanza kuhisi wasiwasi kuhusu maisha yao ya baadaye na kama ujuzi walio nao utafaa katika soko la ajira katika miaka ijayo.
Mnamo Machi, Goldman Sachs alichapisha ripoti inayoonyesha kwamba AI inaweza kuchukua nafasi ya kazi sawa na milioni 300 za kudumu. Mwaka jana, uchunguzi wa kila mwaka wa wafanyakazi wa kimataifa wa PwC ulionyesha kuwa karibu theluthi moja ya waliohojiwa walisema walikuwa na wasiwasi kuhusu matarajio ya kazi zao kuchukuliwa na teknolojia katika miaka mitatu.
"Nadhani wabunifu wengi wana wasiwasi," anasema Alys Marshall, mwandishi wa makala mwenye umri wa miaka 29 anayeishi Bristol, Uingereza. "Sote tunatumai kuwa wateja wetu watatambua thamani [yetu], na kuchagua uhalisia wa [mwanadamu] juu ya bei na urahisi wa zana za AI."
Sasa, wakufunzi wa taaluma na wataalam wa rasilimali (HR) wanasema kwamba ingawa wasiwasi fulani unaweza kuhesabiwa haki, wafanyakazi wanahitaji kuzingatia kile wanachoweza kudhibiti. Badala ya kuwa na hofu juu ya uwezekano wa kupoteza kazi zao dhidi ya mashine, wanapaswa kuwekeza katika kujifunza jinsi ya kufanya kazi pamoja na teknolojia.
Iwapo wataichukulia kama rasilimali wala si tishio, ukiongeza na utaalam, watakuwa wa thamani zaidi kwa waajiri watarajiwa - wakiwa na wasiwasi kidogo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuhofia kisichojuliana
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa watu wengine, zana za uzalishaji za teknolojia ya akili bandia (AI) wanahisi kana kwamba zimekuja kwa kasi na hasira. ChatGPT kwa mfano inazidi kukua kila siku, na kusababisha wafanyakazi kutokuwa na uhakika wa kazi zao.
Carolyn Montrose, mkufunzi wa taaluma na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York, anakubali kasi ya uvumbuzi wa kiteknolojia na mabadiliko yanaweza kutishia. "Ni kawaida kuhisi wasiwasi juu ya athari za AI kwa sababu mageuzi yake, na kuna sababu nyingi za matumizi zisizojulikana," anasema.
Lakini kama teknolojia mpya inavyosikitisha, anasema pia wafanyakazi sio lazima wawe waoga. Watu wana uwezo wa kufanya maamuzi yao wenyewe kuhusu wasiwasi: wanaweza "kuchagua kujisikia wasiwasi kuhusu AI, au kuwezeshwa kujifunza kuhusu hilo na kuitumia kwa manufaa yao".
Scott Likens wa PwC, ambaye ni mtaalamu wa teknolojia, anaunga mkono hili. "Maendeleo ya kiteknolojia yametuonyesha kuwa, ndio, teknolojia ina uwezo wa kubinafsisha au kurahisisha michakato ya kazi. Walakini, kwa seti sahihi ya ujuzi, watu binafsi mara nyingi wanaweza kuendelea kufanya pamoja na maendeleo haya, "anasema.
"Ili kupunguza wasiwasi juu ya AI, wafanyakazi lazima waegemee kwenye teknolojia. Elimu na mafunzo [ni] muhimu kwa wafanyakazi kujifunza kuhusu AI na kile inaweza kufanya kwa jukumu lao mahususi na pia kuwasaidia kukuza ujuzi mpya. Badala ya kuikimbia AI, wafanyakazi wanapaswa kuweka mipango ya namna ya kkwenda nayo sambamba na kujielimisha.
Thamani ya kipekee ya wanadamu
Ingawa wataalam wanasema wasiwasi na hofu za wafanyakazi unaweza kukubaliana nao ,lakini si wakati wa kupaniki. Baadhi ya utafiti hivi majuzi umeonyesha hofu ya AI (roboti) kuchukua nafasi za kazi za binadamu huenda unakolezwa.
Utafiti wa Novemba 2022 wa profesa wa sosholojia Eric Dahlin katika Chuo Kikuu cha Brigham Young huko Utah, Marekani, ulionyesha kuwa sio tu kwamba roboti hazichukui nafasi za wafanyakazi binadamu kwa kiwango ambacho watu wengi wanaamini, lakini baadhi ya watu pia hawaelewi kasi ambayo teknolojia hiyo inachukua nafasi.
Wiki chache zilizopita, Claire, afisa uhusiano, aliamua kuwa anataka kuanza kujifunza zaidi kuhusu teknolojia ambayo inabadilisha tasnia yake. Sasa anatafiti kozi za mtandaoni ambazo anatumai kujifunza kujiongezea uwezo.
"Teknolojia nyingi zilinitisha, kwa hivyo nilipuuza, lakini kulingana na kila kitu ninachokiona, huo ni ujinga," anasema. "Kupuuza kitu hakika hakuwezi kukifanya kiondoke, na polepole ninaanza kuelewa kwamba ikiwa nitachukua muda wa kukifanya kuwa kisichojulikana - ambayo huifanya iwe ya kutisha - inaweza kunisaidia sana."















