Akili bandia inaweza kubaini kubaini magojwa kama saratani, waeleza wataalamu

Chanzo cha picha, Getty Images
Harufu tunayotumia kuboresha harufu za sehemu za umma na uwezo wetu wa kubaini harufu vinaweza kuwa maeneo ya mwisho ya mabadiliko makubwa.
Kiasi kikubwa cha data na kompyuta zenye kasi kubwa zinatumiwa kubaini mtindo mpya duniani wa harufu ili kutengeneza bidhaa haraka kuliko awali.
Kwa upande mwingine ulimwengu wa akili bandia unatengeneza teknolojia ambayo inaweza kung'amua magonjwa katika hatua zake za mwanzo kwa njia ya kunusa, ili kusaidia watu kuishi maisha yenye afya namarefu.
Chini tunaonyesha jinsi akili bandia inavyoweza kuathiri kila kitu kuanzia harufu tunayotumia hadi jinsi tunavyotambua magonjwa
Kugundua matatizo ya harufu

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni inayoibukia ya teknolojia Aribal inatathmini harufu mbali mbali kuangalia iwapo zinaweza kutuathiri na ni nini zinaweza kutuambia kuhusu afya yetu.
Lakini harufu huwa ngumu kuzifuatilia, na wakati kuna mawimbi ya urefu fulani yenye tabia ya mwanga na sauti, hakuna njia yoyote rahisi ya kupima kiwango cha harufu.
Badala yake, kampuni ya Ufaransa hutumia harufu za protini zilizowekwa katika kitambaa cha kaki kutambua ni aina gani ya harufu wanayoivuta , ili kuepuka gesi kama vile Oksijeni, nitrojeni na kaboni monoksaidi ambazo hisia zetu haziwezi kuzipata kwa kwa njia ya pua.
Tunahitaji akili bandia AI kwasababu hatuwezi kuelezea harufu, anasema Mkurugenzi mkuu wa Sam Gilume. Aliongeza kuwa , "Kile tunachoweza kufanya ni kufundisha kompyuta kwa njia ambayo ''Jibini ni hii, na hii ni strawberry... na kadhalika ."
Teknolojia inaweza kuwa na mchango mkubwa katika kufuatilia kwa karibu maeneo ambayo tunakaa kwa muda mrefu ili kuhakikisha mazingira ni sahihi, kitu ambacho tumeanza kukifuatilia tangu janga la Covid lilipoanza.
Kitu kimoja zaidi : Tumebaini kwa muda kwamba magonjwa yanaweza kubainika kwa harufu, na mwaka jana uwanja wa ndege wa Helsinki ulifanya majaribio ya kuwatambua wasafiri wenye Covid kwa kutumia mbwa.
Hii inaweza kuwezesha utengenezaji wa bidhaa ambazo zinaweza kufuatilia afya zetu kila siku ili kung'amua dalili za ugonjwa.
"Labda ninapo piga mswaki meno yangu, kutakuwa na king'amuzi katika mswaki wangu ambacho kinaweza kufuatilia afya yangu, na kitaweza kuwa na uwezo wa kukwambia ninaona athari za kisukari, ninaweza kuhisi dalili za saratani ," anasema Guilome.
Kugundua na kutibu maginjwa mapema, kabla hayajasababisha madhara makubwa, itatusaidia pakubwa katika kukabiliana na ugonjwa kwa ufanisi. Guilumi anaamini kwamba vifaa vya kisasa vya smart ambavyo hutumia akili bandia, kama vile mswaki wa meno, ambavyo vinaweza kutambua maradhi viko njiani vinakuja na tutaweza kuvitumia.
Swali ni iwapo tutakuwa na vifaa hivyo, lakini swala ni lini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Akili bandia hutumiwa kutengeneza harufu mpya.
''Nimekuwa mraibu wa manukato tangu nilipokuwa na umri wa miaka minne, jambo ambalo ni la aibu,''anasema Maria Nurislova. ''Nilikuwa ninaiba manukato ya mama yangu alifahamu hilo.
Uraibu huu wa awali wa manukato ulimfanya Norispalmova kuwa muasisi mweza wa Centbird, kampuni ya Marekani ya manukato inayoibukia ambayo hutuma sampuli za harufu mbali mbali za manukato kila mwaka kwa waliojisajiri kuzipata kila mwezi .
Wakati kampuni ilipoamua kuzindua duka lake la manukato, ilitumia akili bandia kutathmini data za makampuni 300,000 yaliyojisajiri kwa ununuzi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni hiyo huchunguza athari za harufu kwa hisia za watu.
Ina mpango wa kisayansi wenye lengo la kutumia akili bandia kutengeneza harufu nzuri na za kuliwaza.
Utafiti wao pia uliangazia kuhusu jinsi ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya mfumo wa neva.
"Katika kuboresha thamani ya maisha, iwapo utafikiria kuhusu maradhi ya Alzheimer's, tunafahamu kuwa hisia kama vile kuona na kunusa vinaweza kuwa na mchango muhimu, sio katika matibabu , bali katika kuchochea ubongo ili kupunguza uwezekano wa hali yake kuwa mbaya ,"












