Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia 2022: Je kuna umasikini katika taifa la Qatar mojawapo ya nchi tajiri zaidi duniani?
Kuuona umasikini na kuuzungumzia sio suala rahisi nchini Qatar.
Baadhi ya wale wanaokubali kuzungumza kuhusu suala hili huchagua maneno yao kwa uangalifu kwasababu ni "suala gumu kiasi kwamba unapaswa kujilinda na maafisa wanaojaribu kulilinda," anasema dereva wa tesksi Mpakistan ambaye aliiambia BBC hakutaka utambulisho wake ujulikane.
Qatar, mojawapo ya nchi tajiri zaidi duniani, haikosi umasikini. Na hauzungumziwi vya kutosha. Na ni kwasababu umasikini huu umefichwa mbali na mahali ambapo unaweza kuonekana.
Baadhi ya raia wa kijgeni wananaishi katika umasikini huu katika maeneo yaliyotengwa na ya watu masikini, mbali na maeneo yanayotembelewa mara kwa mara na watalii na mashabiki.
Qatar ni taifa tajiri kutokana na pesa zitokanazo na mafuta na gesi, na kutokana na hilo pato la ndani yan chi GDP ya nchi hii ni dola bilioni 180 na hilo limewavutia maelfu kwa maelfu ya wahamiaji kuwekeza katika ujenzi katika jangwa.
Qatar ina wakazi karibu milioni tatu. Kati yao ni 350,000 (10% ya watu) tu ambao ni WaQatar asili. Waliobakia ni wageni. Waqatar na wataalamu wa Magharibi hupata mishahara ya juu na maslahi ya kijamii.
Kulinagana na twakwimu rasmi, Qatar imetokomeza kabisa umasikini, ingawa hali halisi ni tofauti kwa wahamiaji wengi kutoka Kusini mashariki mwa Asia.
Ukosefu wa usawa
Katika nchi ambapo Waqatari na wataalamu kutoka nchi za Magharibi wanaweza kupata mshahara wa maelfu ya dola kwa mwaka pamoja na marupurupu, wafanyakazi wengi wasio na ujuzi wana hakikisho la kupata sio zaidi ya kima cha chini cha mshahara wa dola $275 tu.
Qatar Ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kupiga marufuku kikamilifu mfumo tata wa kafala (hisani kwa lugha ya kiarabu) mwaka 2020 na ya pili kuanzisha mshahara wa kimo cha chini kwa wafanyakazi wote bila kujali uraia wao baada ya Kuwait.
Wakati mfmo wa kafala ulipokuwa ukitekelezwa, iwapo mfanyakazi angebadili kazi bila idhini, kwa mfano aangeweza kukabiliana na mashitaka ya uhalifu, kukamatwa na kurejeshwa katika nchi yake ya asili.
Waajiri wakati mwingine walibana paspoti za wafanyakazi, na kuwalazimisha kuendelea kubakia nchini bila ukomo.
Wahamiaji wengi pia walitakiwa kulipa gharama ya kuajiriwa kwa waajiri wao ya kati ya $500 na $3,500 kabla ya kuondoka nchini katika nchi zao.
Lakini licha ya hali hiyo, mashirika kama vile Human Rights Watch (HRW) yanasisitiza kwamba "wafanyakazi wahamiaji bado wanawategemea waajiri wao kuwasaidia kuingia, kupata makazi na ajira nchini humo, hii ikimaanisha kuwa waajiri ndio wanaowajibika kwa ombi, kuongeza muda wa kufanya kazi na kufuta vibali vyao vya makazi na kazi ".
"Wafanyakazi wanaweza kuachwa bila nyaraka japo sio kosa lao wakati waajiri wanaposhindwa kutimiza mchakato huo , na ni wao, na sio waajiri, wanaoumia kwa thari za kutotekeleza hilo ," inasema ripoti ya mwaka 2020 ya HRW.
Msemaji wa serikali ya Qatar aliiambia BBC kwamba mageuzi yaliyofanywa na nchi yanaboresha hali za kazi kwa wafanyakazi wengi wa kigeni.
"Mafanikio makubwa yamefanyika kuhakikisha kwamba mageuzi yametekelezwa kwa ufanisi," alisema msemaji.
"Idadi ya makampuni ambayo yanavunja sheria itaendelea kupungua huku hatua za utekelezwaji wake zikiendelea kutekelezwa," alisema.
Kombe la Dunia
Qatar ilijenga viwanja saba kwa ajili ya Kombe la Dunia, pamoja na kiwanja kipya cha ndege, leri, mitaa na malazi.
Uwanja wa fainali , Uwanja wa Lusail, uko kando ya mji ambao una jina sawa na la uwanja katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Kulingana na serikali ya Qatar, wafanyakazi wageni 30,000 waliajiriwa kujenga vijanja. Wengi wao walitoka Bangladesh, India, Nepal na Ufilipino.
Idadi ywa wahamiaji hawa waliokufa wakati wa maandalizi ya Kombe la Dunia ni suala lenye utata na linaloleta mgawanyiko.
Kulingana na taarifa kutoka katika balozi za Qatar, magazeti ya The Guardian yaliripoti kwamba wafanyakazi 6,500 kutoka India, Pakistan, Nepal, Bangladesh na Sri Lanka walifariki nchini Qatar tangu 2010, wakati walipopewa kazi katika uwanja wa Kombe la Dunia.
Lakini Qatar inalaani idadi hiyo kama ya upotoshaji na yasiyo sahihi, kwasababu sio vifo vyote vilivyorekodiwa vya wafanyakazi vilikuwa na uhusiano na Kombe la Dunia na wengu huenda walikufa kutokana na uzee na sababu nyingine za kawaida.
Lakini shirika la kimataifa la kazi (ILO) linasema kwamba idadi hiyo haionyeshi ukweli halisi, kwasababu Qatar haihesabu vifo vinavyohusiana na na kazi, vifo vitokanavyo na shinikizo la damu au kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa kupumua, ambazo ni dalili za kawaida za kiharusi kinachotokana na joto na kazi kubwa katika maeneo ya hali ya hewa ya viwango vya juu vya joto
Kulingana na ILO, wafanyakazi wa kigeni 50 waliuawa na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa vibaya katika mwaka 2021 pekee, huku wengine 37,600 wakiumia na kupata majeraha madogo.
Idhaa ya BBC ya Kiarabu pia ilikusanya ushahidi kwamba serikali ya Qatari ilipuuza vifo miongoni mwa wafanyakazi wa kigeni.
Lakini eneo, ambalo maelfu ya mamilioni ya dola yamewekezwa, imezuiwa kwa vyombo vya habari nchini Qatar na imekuwa ikikosolewa kwa kulitenga eneo hili lililopo viungani mwa mji mkuu Doha na mbali na raha za kifahari zinazoonekana kwenye televisheni wakati wa Kombe la Dunia.