Ifahamu aina ya ndege iliohusika na ajali Tanzania

Na Abdallah Dzungu

BBC Swahili

Saa 8:53 saa za Afrika mashariki mnamo tarehe 6 Novemba, ndege ya Precision Air PW 494 ilihusika katika ajali ilipokua inataka kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba (BKZ) katika taifa la Afrika mashariki , Tanzania.

Ndege hiyo ilibeba abiria 39 ambapo kati yao kulikuwa na watu wazima 38 na mtoto mmoja mdogo mbali na wafanyakazi wanne wa shirika hilo.

Kwa mujibu wa ch-aviation, shirika la ndege la Precision linaendesha kundi la ndege tisa: ATR 42-500 mbili, ambapo moja imehusika katika ajali ya Jumapili, Ndege zingine mbili aina ya ATR 42-600 ambazo hazifanyi kazi, na ndege tano aina za ATR 72-500 , ambapo mbili kati yazo hazifanyii kazi.

Ndege zote zimekodishwa kutoka kwa kampuni ya Swala Leasing & Finance yenye makao yake huko Ireland.

Shirika la ndege la Precision Air linaendesha huduma za ndani, kikanda, na za kukodi kwa maeneo mengi ya kitalii, ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Visiwa vya Zanzibar.

Lakini ndege aina ya ATR 42 ni ndege ya aina gani?

ATR 42 ni shirika la ndege la kieneo lililoundwa na watengenezaji wa ATR wa Ufaransa-Italia, na vipande vya ndege hiyo hatimaye kuunganishwa huko Toulouse, Ufaransa.

Mnamo tarehe 4 Novemba 1981, ndege hiyo ilizinduliwa na ATR, kwa ushirikiano wa kampuni ya ndege ya Aérospatiale kutoka Ufaransa (sasa Airbus) na ile ya ndege kutoka Itali Aeritalia (sasa Leonardo S.p.A.).

ATR 42 ilifanya safari yake ya kwanza mnamo tarehe 16 Agosti 1984 na kupewa kibali chake cha kwanza kuhudumu Septemba 1985.

Ina na urefu wa mita 22.7m na kimo cha urefu wa 7.6m

Je ATR ina maana gani?

Kiwango cha wastani cha kweli (ATR) ni kiashirio tete cha soko kinachotumika katika uchanganuzi wa kiufundi. Awali ATR ilitengenezwa kwa matumizi katika masoko ya bidhaa lakini sasa inatumika kwa shughuli za aina zote, ikiwemo kubeba abiria.

Ndege hiyo yenye mabawa ya juu inaendeshwa na injini mbili za turboprop, Pratt & Whitney Canada PW120s. Nambari "42" inayotumika katika jina lake inatokana na uwezo wa asili wa ndege ya kubeba abiria 42.

Turboprops ni bora zaidi kuliko ndege nyengine kwenye sekta ya masafa mafupi, kwa sababu zinasafari angani kwa kutumia nguvu kidogo na hivyo basi mafuta machache.

Ndio ndege zinazotumika sana katika safari fupi za saa moja au kilomita (550km), wakati ambapo huna haja ya kuruka juu sana na kuwa na kasi ya juu.

Hatahivyo muundo mpya wa ndege hiyo umeboreshwa kwa kutumia avionics mpya, chumba cha marubani cha glasi, na matoleo mapya ya injini. ATR 42 ni toleo jipya la ATR 72 , iliyoanzishwa mnamo Oktoba 1989.

ATR 42-500 ni toleo lililoboreshwa la -320 kwa kutumia propela zenye ncha sita kwenye injini za PW121 zinazofanana.

Ndege mbili pekee za kiraia za ATR 42-400 zilizoundwa (msn 487 na 491) ziliwasilishwa kwa Mashirika ya Ndege ya CSA Czech mnamo 1995/1996 kama uboreshaji wa muda kabla ya kuwasili kwa ATR 42-500s.

Mnamo 2006, ndege hizi mbili ziliuzwa kwa Conviasa – kampuni kubwa ya ndege nchini Venezuela.

Je ATR 42 ina kasi ya kiwango gani?

Inaweza kufikia kasi ya hadi 556 km/h) ikiwa hewani.

Ndege hiyo ina uwezo wa kuondoka na kutua kwa muda mfupi) mbali na kuruka kutoka kwa njia fupi za kuruka kwa ndege zenye urefu wa mita 800 (futi 2,600) ikiwa na hadi abiria 42.

Mazingira

Ina faida kubwa ya mazingira ikilinganishwa na ndege nyengine za kikanda , ikiwa na chini ya utoaji wa asilimia 40 wa gesi ya kaboni kwa kila safari ya kilomita 550.

ATR 42 haina kelele

Kelele ya nje ya ndege aina ya ATR 42-500 ni 8.9 dB ikiwa ni kiwango cha chini cha Shirika la kimataifa la usafiri wa anga ICAO.