''Rubani alisema anaangalia jinsi ya kutua, iliposhindikana hakuweza kusema lolote''

''Rubani alisema anaangalia jinsi ya kutua, iliposhindikana hakuweza kusema lolote''

Eva Mcharo aliyenusurika katika ajali ya ndege Bukoba amesimulia namna ilivyokuwa mpaka ajali inatokea na namna alivyookoka.

Ndege ilisogezwa hadi karibu kabisa na ukiongo wa Ziwa Victoria. Ndege hiyo ilikua ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kupitia Mwanza. Ilipata ajali wakati inakaribia kutua katika uwanja wa mji wa Bukoba.

Precision Air ndiyo shirika kubwa la ndege la binafsi la Tanzania na kwa sehemu inamilikiwa na Kenya Airways. Ilianzishwa mnamo 1993 na inaendesha safari za ndege za ndani na kikanda.