Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afcon 2023: Je, vigogo wa Afrika wanaweza kunusurika nusu fainali?
- Author, Piers Edwards
- Nafasi, BBC
Baada ya mechi za robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023, ikiwa ni pamoja na ushindi wa dakika ya 122 na kipa kuokoa penalti nne katika mikwaju ya penalti, nusu-fainali ya Jumatano huko Ivory Coast imewadia.
Mabingwa mara tatu Nigeria wanakabiliana na timu ya Afrika Kusini inayotaka kushinda taji lao la pili - lakini ni la kwanza ugenini kwani taji lao la kwanza ni 1996 huko Johannesburg.
Wenyeji Ivory Coast hawajawahi kushinda taji katika ardhi ya nyumbani - waliishinda Senegal mwaka 1992 na Equatorial Guinea 2015 - wana kibarua kipevu mbele ya DR Congo, ikiwa wanataka kucheza fainali Jumapili mjini Abidjan.
Tembo wa Ivory Coast
Ivory Coast bila shaka wamekuwa kwenye panda-shuka tangu kuanza kwa mashindano hayo.
Baada ya kufanya vibaya kwenye hatua ya makundi, Tembo hao walipenya hatua ya 16 bora kama timu bora iliyomaliza nafasi ya tatu kwenye kundi.
Kiungo wa kati Franck Kessie anasema wachezaji wameonyesha ari ya ajabu walipofunga mabao ya dakika za lala salama dhidi ya Senegal na Mali katika hatua ya 16 bora na robo fainali.
Mabao yote matatu ya Ivory Coast kwenye mtoano yametoka kwa wachezaji wa akiba.
"Hatutakuwa na bahati kama hii wakati wote, lakini ni muhimu kujua kwamba wale walio kwenye benchi wanaweza pia kuchangia," anasema kocha Emerse Fae.
Timu hiyo itarejea kwenye Uwanja wa Alassane Ouattara kwa mara ya kwanza tangu ifungwe 4-0 na Equatorial Guinea katika mchezo wao wa mwisho wa kundi.
"Katika michezo iliyopita, motisha kutoka kwa mashabiki imesaidia - tunatumai wataendelea kutushabikia," anasema Emerse Fae.
Fae atawakosa wachezaji wanne waliosimamishwa Odilon Kossounou na Oumar Diakite, walitolewa kwa kadi nyekundu dhidi ya Mali - wa kwanza alicheza rafu, wa mwisho kwa kuvua shati lake baada ya ushindi wa dakika ya 122, na nahodha Serge Aurier na Christian Kouame, kwa kuwa na kadi mbili za njano.
DR Congo itapenya kwenda fainali?
Huku mabingwa mara mbili DR Congo wakitinga nusu fainali ya pili ya Kombe la Mataifa ya Afrika karne hii na ya kwanza tangu kushindwa na Ivory Coast mwaka 2015.
Timu hiyo itavaa vitambaa vyeusi kwa wale wote walioathiriwa na mzozo wa vita katika taifa hilo.
Jambo la kushangaza ni kwamba, DR Congo ilifuzu robo fainali baada ya kutoka sare katika michezo ya kwanza katika michuano hiyo, na kuwashinda Misri kwa mikwaju 8-7 katika hatua ya 16 bora.
"Ushindi wetu wa kwanza ulikuja wakati mwafaka kwa sababu tunazidi kushika kasi," anasema kocha Sebastien Desabre, ambaye amekiunda kizazi cha sasa cha timu ya DR Congo.
"Tunaweza kuwa tumeshinda mara moja tu lakini kumbuka bado hatujapoteza."
Mshambuliaji wa Brentford, Yoane Wissa ndiye anayeongoza kwa mabao akiwa na mabao mawili, huku mlinzi wa zamani wa Newcastle United, Chancel Mbemba na beki wa kushoto wa zamani wa West Ham, Arthur Masuaku, pia wakipachika mabao.
Je, Nigeria itasonga mbele?
Nigeria itamenyana na Afrika Kusini mjini Bouake. Nusu-fainali ya Kombe la Mataifa ya 2000, Super Eagles waliwashinda Bafana Bafana baada ya nchi hizo kukutana kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo.
Wenyeji hao wa Afrika Magharibi wana nafasi kubwa katika michuano ya Afcon, wakishinda mechi zote tatu - na mechi ya hivi karibuni zaidi kati ya hizo ni robo fainali mwaka 2019.
Ikicheza katika nusu fainali ya 15 ya Afcon, Nigeria wamevutia katika safu ya ushambuliaji na ulinzi, ambapo wameshinda michezo yao minne iliyopita bila kuruhusu bao.
Huku Frank Onyeka akiwashinda wakosoaji wake na kutawala katika safu ya kati, wachezaji kama Ademola Lookman na Moses Simon wameonesha mchezo mzuri - wakitengeneza bao pekee la robo fainali dhidi ya Angola .
"Tuna imani kubwa na safu yetu ya ulinzi," mlinzi Semi Ajayi aliambia BBC Sport Africa.
Kocha Jose Peseiro amekuwa akisema mara kwa mara kufunga goli kutahakikisha ushindi kwa timu yake kutokana na umahiri wao mbele, ambapo Mwanasoka Bora wa Afrika wa Mwaka Victor Osimhen ameonekana kucheza bila kuchoka licha ya kufunga bao moja pekee.
Kocha Broos ataivuusha Bafana Bafana?
Wengi walitarajia Nigeria kufika mbali, wachache walifikiria vivyo hivyo kuhusu Afrika Kusini ambao wamefaidika na uongozi wa kocha Hugo Broos, ambaye aliiongoza Cameroon kunyakua ushindi ambao haukutarajiwa 2017.
Kocha huyo mwenye umri mkubwa zaidi katika michuano hiyo, umri wa miaka 71, anaitegemea klabu ya Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns kuipeleka Bafana Bafana katika nusu fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 24.
Wachezaji wanane wa klabu hiyo yenye maskani yake mjini Pretoria iliyoshinda Ligi ya Soka ya Afrika mwaka jana, huku pia ikifika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, walianza robo fainali dhidi ya Cape Verde.
"Amechukua wachezaji wa Sundowns kwa sababu anaelewa wachezaji hao wana uzoefu kutoka barani kote - na aligundua kuwa bidii na kazi ya pamoja ni muhimu," nahodha wa zamani wa Afrika Kusini Aaron Mokoena aliambia BBC.
Broos alisema kiwango chao dhidi ya Cape Verde kilikuwa kibaya , ingawa Bafana Bafana wameshinda mechi nne mfululizo. Nahodha Ronwen Williams amefanya kazi kubwa kwa kuzuia penalti nne kwenye mikwaju ya penalti.
Katika safu ya kiungo Teboho Mokoena, mchezaji mwingine wa Sundowns, ameonesha mabadiliko. Nigeria itahitajika kuwa makini na mshambuliaji mzoefu Themba Zwane aliyefunga mara mbili katika ushindi wa hatua ya makundi dhidi ya Namibia.
Broos amewachezaesha wachezaji wake bila kubadilisha tangu mechi ya pili, wasiwasi mkubwa utakuwa ni uchovu, huku kiungo wa zamani wa Afrika Kusini Dean Furman akionyesha kuchoka katika mechi dhidi ya Cape Verde siku ya Jumamosi.