Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Man Utd kumsajili Semenyo Januari

Semenyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester United itafanya kila iwezalo kumsajili mshambuliaj i wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo mwezi Januari na wanatumai kutokuwa na uhakika juu ya mustakabali wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City kunaweza kuongeza nafasi yao ya kumpata mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Telegraph - usajili unahitajika)

Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Ruben Neves, 28, amesusia kutia saini mkataba mpya na klabu ya Al-Hilal ya Saudi Pro League. Tetesi zinaseama anataka kurejea Ulaya huku Manchester United ikionekana kuwa shabaha ya kiungo huyo wa zamani wa Wolves. (Times - usajili unahitajika)

Manchester United iko tayari kumuuza Kobbie Mainoo, 20, katika dirisha la uhamisho wa Januari ikitapata ofa nzuri. Unite inasita kumruhusu kiungo huyo wa kati wa Uingereza kuondoka kwa mkopo. (Sky Sports)

Kocha mkuu wa Chelsea Enzo Maresca, 45, anaongoza wagombea ambao Manchester City inawafikiria iwapo kocha Pep Guardiola, 54, ataondoka Etihad msimu ujao. (Athletic - michango inahitajika)

Saint-Etienne wamekataa ofa ya awali ya euro milioni nane (£7m) kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya Djylian N'Guessan, 17, lakini klabu hiyo inafikiria kumuuza mshambuliaji huyo wa Ufaransa kwa euro 12.5m (£11m). (L'Equipe - kwa Kifaransa),

Mchezahi mahiri Mholanzi AZ Alkmaar Kees Smit, 19, ni mmoja wa viungo wanne wanaofuatiliwa na Newcastle, huku mlinzi wa Toulouse Mfaransa Dayann Methalie, 19, pia anadhaniwa kuwa kwenye orodha yao. (Mail - usajili unahitajika)

Bruno Fernandes

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, kifungu cha kutolewa kwa Bruno Fernandes chafichuliwa

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ureno Bruno Fernandes, 31, ana kipengele katika mkataba wake ambacho kinamaanisha kuwa klabu zilizo nje ya Ligi ya Premia zinaweza kumsajili kwa paunu milioni £56.6m. (Mail - usajili unahitajika)

Atletico Madrid wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 28, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Barcelona kutoka Manchester United. (Fichajes - kwa Kihispania)

Kuna uwezekano mkubwa Bayern Munich kutumia chaguo la kubadili uhamisho wa mkopo wa Nicolas Jackson kutoka Chelsea kuwa wa kudumu msimu wa joto, huku mshambuliaji huyo wa Senegal, 24, akitumika kama msaidizi wa mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Harry Kane, 32. (Bild - kwa Kijerumani).

Bukayo Saka

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Saka alikuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichoishinda Chelsea na kushinda Kombe la FA mnamo 2020, ingawa hakucheza

Bukayo Saka, 24, atakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Arsenal kulipwa mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki, huku klabu hiyo ikikaribia kutangaza mkataba mpya wa kuvunja rekodi kwa winga huyo wa Uingereza utakaodumu hadi 2031. (Teamtalk)

Winga wa West Ham Luise. Guilherme anataka kusalia na kupigania nafasi yake katika klabu hiyo, licha ya tetesi zinazomhusisha Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 19 na uhamisho wa mwezi Januari. (Sky Sports)

Pia unaweza kusoma:

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi