Mauaji ya watu kulinda Ngombe nchini India yazidi kuzua hofu nchini humo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mapema mwezi January mwaka huu magari yaligogana huko Tauru, mji mdogo katika jimbo la kaskazini mwa India la Haryana.
Ndani ya gari hilo kulikuwa na vijana watatu wa Kiislamu: Waris, Nafiz na Shaukeen. Waris sasa tayari amefariki dunia na Nafiz yupoo jela. Na Shaukeen bado anapambana na hofu kutokana na ndoto anazoziota za kutisha usiku.
Shaukeen anadai kuwa rafiki yake alipigwa hadi kufa na kundi la wanaume wa kihindi baada ya kuona ng'ombe akiwa amejibanza nyuma ya gari lao. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 anadai ng'ombe huyo alikuwa wa Nafiz, ambaye alikuwa akimrudisha nyumbani kwake Haryana kutoka wilaya ya Bhiwadi katika jimbo jirani la Rajasthan.

Chanzo cha picha, Getty Images
Shaukeen na Waris walikuwa wakiongozana naye walipofukuzwa na kundi la watu wanosemakana kuwalinda ng'ombe. Hawa ni wanaume wa kihindi wengi wao wakiwa wamejihami kwa fimbo na silaha nyingine ambao huvizia magari yanayosafirisha ng'ombe ili kuzuia mauaji ya ng'ombe, ambayo ni kinyume cha sheria katika majimbo mengi ya India.
Polisi, hata hivyo, wanasema kwamba hakukua na makovu yanayonesha kuwa waris alijeruhiwa."Tulitaarifiwa kuhusu ajali hiyo ya barabarani na dereva wa lori na baadhi ya ''Gau rakshaks'' kundi lilojitolea kuwalinda Ngo’mbe kama wanavyotambulika nchini humo.Tulipofika katika eneo hilo watu watatu walikuwa ndani ya gari, tukawapeleka hospitali ya jirani, mmoja wao alifariki dunia kwa majeraha baadaye," alisema Varun Singla, msimamizi wa polisi katika wilaya ya Nuh ya Haryana, ambako Tauru ipo. Aliongeza kuwa gari hilo lililokuwa limebeba mboga pia lilikuwa limeharibika.
"Dereva hakuwa amejeruhiwa lakini mtoto wake aliyekuwa kwenye kiti cha abiria alipata majeraha madogo." Polisi waliwakamata Nafiz na Shaukeen kwa mashtaka ya kusafirisha ng'ombe kwa sababu "walimpata ng'ombe ndani ya gari" lao anasema Singla

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini Shaukeen, ambaye kwa sasa yuko nje kwa dhamana, anasema kuwa gari lao liligonga gari hilo kwa sababu tu walikuwa wakifukuzwa na gari ambalo lilikuwa la walinzi wa ng'ombe.
BBC imepata picha za CCTV za ajali hiyo huko Tauru.picha hiyo inaonyesha gari moja likiwa na king'ora likikaribia gari lingine muda mfupi baada ya ajali.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
kulingana na video iliyorekodiwa na shuhuda mmoja katika eneo la tukio , kundi la wanaume waliojitolea kuwalinda ngo’mbe nchini humo walioonekana kuwa na silaha, ikiwa ni pamoja na bunduki, walimtoa ng'ombe kutoka kwenye buti ya gari na kuwaweka wanaume watatu wa Kiislamu ndani ya gari lao.
Shaukeen anadai kuwa yeye na wenzake walipigwa na genge hilo ambalo baadaye waliwapeleka hospitali na kwamba Waris alifariki njiani.
"Waris hakufa katika ajali hiyo. Hakukuwa na jeraha hata moja kutokana na ajali hiyo," anasema, akiongeza kuwa yalikuwa "mauaji yaliyolengwa" dhidi ya Waisilamu
Ng’ombe anachukuliwa kama mnyama mtakatifu na idadi kubwa ya rai nchini India , hivyo kitendo cha kumchinja au kuonekana kumsafirisha kwa baadhi ya watu haikubaliki.
Uchinjaji wa ng'ombe ni mada nyeti nchini india na imepigwa marufuku katika baadhi ya majimbo, jambo ambalo mpaka sasa limekuwa suala linalojadiliwa sana tangu Waziri Mkuu Narendra Modi wa chama cha Bharatiya Janata (BJP) aingie madarakani nchini humo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Makundi ya vijana waliojitolea kuwalinda Ngo’mbe nchini India yameshutumiwa kwa kutekeleza marufuku hii kupitia ghasia,na mara nyingi huwa wanawashambulia wauzaji wengi wa nyama na wafanyabiashara wa ng'ombe ambao asilimia kubwa ni waisilamu.
Narendra Modi amekosoa vikali makundi hayo siku za nyuma lakini mashambulizi kadhaa ya hali ya juu yametokea hata baada ya hapo ,Nyumbani kwa Waris huko Nuh, familia yake bado inapambana na mshtuko wa kifo chake.
"Ikiwa mtu anafanya uhalifu,tena uhalifu wa aina yoyote ile basi polisi wanapaswa kuwaadhibu," anasema Imran, kaka mkubwa wa Waris.
Anahoji ni kwa nini makundi hayo katika jimbo hilo "yamepewa haki ya kujichukulia sheria mkononi".
Lakini Ravi Kiran, inspekta jenerali wa polisi wa Haryana, aliambia BBC kwamba ripoti ya uchunguzi wa maiti ilithibitisha kwamba kifo cha Waris kilisababishwa na ajali hiyo. Aliongeza kuwa polisi wako tayari kuchunguza suala hilo zaidi iwapo watapata taarifa mpya kuhusu kesi hiyo.
Shaukeen anadai kwamba mwanamume kwa jina Monu Manesar anaefahamika saana kwa sera zake tata za kuwalinda Ngo’mbe ambaye sura yake sio ngeni mtandaoni kutokana na kuchapisha video zake akiuliza swali moja tu kwa nini watu nchini humo au kusafirisha Ngo’mbe ndie aliekua akiliongoza kundi lilowavamia na kwashambulia .
Siku ya tukio, Manesar alirusha tukio zima moja kwa moja mtandaoni huku akiwaulizaWaris na wenzie swali lake lile lile lililozoeleka na wengi , la kwa nini wanawasafirisha Ngo’mbe.Katika video hiyo, ambayo sasa imefutwa kwenye mtandao wake wa Facebook Manesar na wanaume hao Waislamu walikuwa na majeraha usoni.
"Monu ilikuwa ikisema 'wapige' na kila mtu alikuwa akitupiga. Yote yalifanyika kwa mwelekeo wa Monu," Shaukeen alidai.
BBC haikuweza kuwasiliana na Manesar, ambaye kwa sasa anasakwa na polisi ili kuhojiwa katika kisa kingine cha madai ya kuwadhuru watu wanaosafirisha Ngo’mbe. Lakini katika mahojiano na BBC mwezi Januari mwaka huu alikana kuhusika kwa vyovyote na kifo cha Waris.
Alidai kuwa kundi lake lilipewa taarifa kwamba ng’ombe alikuwa akipakiwa kwenye gari la kina waris na walipofika kwenye eneo la tukio dereva wa alilokuwa waris alianza kuendesha kwa kasi.
“Nilifika eneo la ajali baada ya takribani dakika 35, nikaona magari mawili ya polisi, watu waliokuwa kwenye gari walikuwa wameumia kidogo hivyo nikawaambia watu wawape maji, baadaye polisi waliwapeleka hospitali,” alisema. akiongeza kuwa alisikia tu kuhusu kifo cha Waris saa chache baada ya ajali hiyo.
Imran anadai kwamba kifo cha kaka yake kilikuwa sehemu ya mtindo mkubwa wa mashambulizi ya kikatili ya makundi ya vijana yaliojitolea kuwalinda Ngo’mbo nchini humo
Alihusisha kifo cha Waris na kesi nyingine maarufu ya mauaji ya wanaume wawili Waislamu, Junaid na Nasir - ambayo iligonga vichwa vya habari nchini India wiki chache baadaye.
Miili iliyoungua ya Junaid na Nasir ilipatikana kwenye gari lililoteketezwa katika wilaya ya Bhiwani ya Haryana mwezi Februari mwaka huu. Jamaa zao wamedai waliuawa na wanachama wa kundi la watu wenye msimamo mkali wa Kihindi ambao, kulingana na ripoti za vyombo vya habari, waliwashutumu kwa kusafirisha ng'ombe. Wanaume watano akiwemo Manesar walitajwa kwenye malalamishi hayo ya polisi lakini polisi wamesema ni washukiwa watatu pekee ambao wamekamatwa kufikia sasa.
BBC ilitembelea familia ya Junaid na Nasir huko Bharatpur huko Rajasthan.

Chanzo cha picha, Getty Images
“Mwili wake uliletwa kwenye begi, ulikuwa ni majivu, hapakuwa na kitu, majivu machache tu na mifupa michache,” alisema mke wa Junaid, Sajida huku akifuta machozi.
Aliogeza kuwa alikuwa na wasiwasi kuhusu jinsi atakavyowatunza watoto wao sita peke yake.
Vifo hivyo vimesababisha maandamano makubwa ya Waislamu mjini Bharatpur, ambao walidai kuwa sheria za ulinzi watu wanaolinda ng'ombe zilikuwa zikitumika kuwalenga.
"Kila mtu anaogopa. Hofu ni kwamba wanaweza kukuchukua. Wanauwezo wa kumchukua mtu yoyote yule kisha wanakuwekea kesi ya kusafirisha Ngo'mbe kwa njia isiokua halali," alidai Mahmur, kaka mkubwa wa Nasir.
Umbali wa maili mia moja, katika mji wa Manesar wa Haryana, kundi la wanaume waliojitambulisha kuwa walinzi wa ng'ombe walikusanyika kwenye makazi mengi ya watu.
BBC ilizungumza na wengi wao, ambao walidai kuwa walifanya kazi na polisi na wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria. Baadhi yao walisema kwamba wao pia wakati mwingine hushambuliwa wanapokua kwenye doria.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kama kuna mwanamke sokoni na tukaona kuwa mtu anafanya mambo ambayo hayafai kiukweli huwa hatuwasubiri polisi, tusubiri polisi ?anauliza Dharminder Yadav, ambaye alikuwa kiongozi wa kikundi cha kulinda ng'ombe kabla ya Manesar kuchukua hatamu.
Yadav alikanusha madai ya Waislamu kulengwa. "Sheria zetu zinasema tunatakiwa kuwalinda ng'ombe. Kila kitu ambacho sheria yetu inasema ni wajibu wetu kufuata. Adui yetu ni mfanyabiashara wa ng'ombe na si Waislamu pekee," alisema.
Shaukeen anadai sasa anaogopa sana kuondoka nyumbani kwake."Waris amekufa na sitaki kuuawa kama yeye."












