Pande mbili za mji mkuu wa Somalia Mogadishu

Chanzo cha picha, SORAYA ALI
Katika mfululizo wa barua zetu kutoka kwa waandishi wa habari wa Kiafrika, Soraya Ali anajaribu kulinganisha kati ya taswira ya Somalia ambayo alikua nayo na sifa yake kama mahali pa uhasama.
Hadi wiki chache zilizopita sikuwa nimewahi kufika nyumbani.
Nchi ambayo ninazungumza lugha hiyo, na kuonekana kama watu wengine lakini sijawahi kuikanyaga.
Mahali hapo ni Somalia.
Lakini mwezi huu, nilifuata nyayo za watoto wengi wanaoishi nje ya nchi na kukata tikiti ya kwenda nchi yangu.
Nilizaliwa na kukulia London, kilomita 9,700 hivi kutoka kwa familia yangu.
Nilipokuwa nikikua, sikuzote nilihisi kuchanganyikiwa na kile kilichosikika kama miji miwili tofauti sana.
Ningesikia kuhusu Mogadishu kwenye habari. Mji mkuu uliojaa vifo na uharibifu, unaotajwa kuwa "mahali hatari zaidi duniani".
Lakini wazazi wangu wangezungumza kwa furaha sana kuhusu "Xamar", kama wenyeji wanavyoiita. Walielezea jiji zuri, lililoko kwenye mwambao mrefu zaidi wa Afrika, unaojulikana kwa wengi kama "lulu ya Bahari ya Hindi".
Nimegundua kuwa pande zote mbili zina ukweli fulani.

Chanzo cha picha, SORAYA ALI
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Waafrika wengi walio ughaibuni, kama mimi, wamerudi katika nchi yao ya asili au ya mababu zao.
Wakati wa kuwasili mara nyingi kuna hisia ya kina ya kuwa mmoja wao, lakini wakati huo huo, huzuni juu ya tofauti ambazo kuwa katika nchi za kigeni zimejenga.
Wazazi wangu walizaliwa Mogadishu mwishoni mwa miaka ya 1950 na, kama Wasomali wengi wenye umri mkubwa, wana kumbukumbu zao nzuri za nchi hiyo.
"Tulikuwa tukivuta kilicho karibu na kuvaa chochote tunachotaka," mama yangu mara nyingi hukumbuka, akikumbuka matukio yake ya ajabu na hata mitindo ya nywele isiyo ya kawaida. Siku hizi wanawake wanatarajiwa kuvaa na kijihifadhi zaidi.
"Mlichokuwa nacho ni mbuzi," ndugu zangu walitania, kwa mshangao wangu.
Somalia tuliyokua tunaiona kwenye skrini zetu ilionyesha waandishi wa habari wa Magharibi katika kambi za watu waliokimbia makazi yao wakizungumza na wale walio karibu kukabiliwa na njaa. Huko nyuma katika miaka ya 1990, ilikuwa ni kwa sababu ya vita.
Lakini taswira ile ile inaonyeshwa, mpaka 2023, kama matokeo ya kukosekana kwa utulivu na mabadiliko ya hali ya hewa.
Bila kutarajia, picha sahihi zaidi ya Somalia niliyopata ilikuwa kupitia TikTok.
#SomaliTikTok ni kubwa na alama imekusanya takriban maoni bilioni 77.
Kupitia mitandao ya kijamii nilipata muono wa maisha ya kila siku huko Mogadishu, kupitia lenzi za wenyeji na watu kama mimi.
Hii ilinisukuma kwenda kuuona kwa macho yangu na hata kufikiria kuhama hapa.

Chanzo cha picha, SORAYA ALI
Bila shaka Mogadishu bado ni sehemu hatari, kundi lenye uhusiano na al-Qaeda al-Shabab bado ni tishio kubwa. Shambulio la mwezi Oktoba liliua zaidi ya watu 100.
Lakini kuna upande mwingine wa jiji ambao hauonyeshwa mara chache - hofu ya kutokuwa na utulivu inamaanisha kuwa watu wengi wa Magharibi hawasafiri kwa uhuru.
Mzungu pekee ambaye nimeuona yupo uwanja wa ndege wenye ulinzi mkali.
Lakini hisia ya kweli ya Mogadishu inaweza tu kupatikana kupitia migahawa yake, masoko, fukwe na watu.
Jiji huwa na shughuli nyingi usiku na huchunguzwa vyema kwenye bajaja - riksho ya Kisomali.
“Bajaj zipo sita kwa kila mtu,” dereva mmoja alitania.
Vyakula na ladha zinazojulikana hunikumbusha upishi wa mama yangu.
Chakula kikuu cha Kiafrika kama vile nyama na wali hutolewa kila mara pamoja na ndizi, kando ya vyakula kama vile tambi, kutoka kwa ukoloni wa zamani wa Italia.
Wavuvi wenyeji hubeba jodari wakubwa adimu kwenye mabega yao, yenye thamani ya makumi ya maelfu ya dola nchini Japani.
Cha kusikitisha ni kwamba, ukosefu wa miundombinu na uwekezaji katika sekta ya uvuvi iliyochipuka mara moja nchini ina maana ni nadra kufaidika kutokana nayo.
Lakini wakati Rais Hassan Sheik Mohamud anapomaliza mwaka mmoja madarakani, kuna hisia zinazoongezeka kuwa nchi iko kwenye njia ya kujengwa upya.

Chanzo cha picha, SORAYA ALI
"Unaona ujenzi kila mahali, tunaboresha polepole, Mungu akipenda," dereva wangu wa bajaja mwenye umri wa miaka 24 anaonyesha.
Kama wengi, bado hajapata uzoefu wa Somalia tulivu. Vita vilizuka mwaka wa 1991 na karibu 75% ya idadi ya watu nchini ni chini ya miaka 30.
Bado ana matumaini lakini mazungumzo yetu yanaangazia ukosefu wa usawa.
Kama watu wengi wanaoishi nje ya nchi, nina fursa ya kuchagua kurudi.
Wakati Wasomali wengine, haswa walio nje ya mji mkuu wanatafuta njia ya kutoka.
Mnamo 2022, Somalia ilishika nafasi ya nane ya wakimbizi duniani, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Somalia ni mojawapo ya nchi zilizoathiriwa zaidi na hali mbaya ya hewa duniani ambayo imewalazimu mamia kwa maelfu kuondoka makwao, huku ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40 sasa ukiingia msimu mwingine wa mafuriko makubwa.
Tunapoendelea kuingia jijini, ninaona majengo, mapya na ya zamani, na kustaajabia usanifu wa Kiislamu wa Afro-Italia.
Zimeimarishwa nyuma ya vizuizi vya zege na mwingi wa mifuko ya mchanga.
Na karibu kila kona ya jiji ni afisa kijana aliye na bunduki aina ya AK-47.
Miito ya maombi huzungumziwa kupitia spika na kuingiliwa na sauti ya milio ya risasi ya mbali.
Licha ya hili, ninahisi hisia ya kina ya matumaini. Na siko peke yangu.
Jiji limejaa watu wengine wanaoishi nje ya nchi, mara nyingi kutoka Minnesota au Toronto, pamoja na Wasomali wenyeji ambao wameazimia kutafuta utulivu.
“Ninaamini katika nchi yangu,” mfanyabiashara mmoja kijana ananiambia.
Anasema hataki kamwe kuondoka.
"Tunaweza kurudisha Somalia ambayo wazazi wetu walituambia," anaongeza.















