Majengo 10 marefu zaidi barani Afrika 2023

Muda wa kusoma: Dakika 5

Historia ya majengo marefu zaidi barani Afrika ilianza mwaka 1973 kufuatia ujenzi wa jumba refu la Carlton Centers mjini Johannesburg , ambalo lilishikilia taji la jumba refu barani Afrika hadi mwezi Aprili 2019 kulingana na mtandao wa wajenzi wa nyumba CK .

Baada ya kupata sifa ya kuwa na jumba refu zaidi barani , haishangazi kuona kwamba Afrika Kusini imejizatiti kumiliki idadi kubwa ya majumba marefu barani Afrika.

Haya hapa majumba marefu zaidi barani Afrika:

1. Leonardo, Afrika Kusini

Jumba la Leonardo lina urefu wa mita 227-pamoja na ghorofa 56. Jumba hilo lipo katika barabara ya 75 ya Maude, takriban mita 100 kutoka katka jumba la soko la hisa la Johannesburg Stock Exchange.

Kulingana na CK , Ujenzi wa Leonardo ulianza tarehe 17 Novemba 2015 , na jumba hilo liliongoza mengine kwa urefu kufikia mwezi Aprili 2019 – likiwa ndilo jumba refu zaidi barani Afrika .

2. Carlton Centre, South Africa

Kituo cha Carlton Centre, jumba refu lenye urefu wa mita 223 na kituo cha ununuzi huko Johannesburg, Afrika Kusini, hapo awali lilikuwa jengo refu zaidi barani Afrika tangu kukamilika kwake mnamo 1973.

Iliyoundwa na kampuni ya usanifu ya Marekani ya Skidmore, Owings and Merrill, Carlton Center inafanana na Mnara maarufu wa One Seneca huko Buffalo, New York, ambao ulikamilika mwaka huo huo.

Ikiwa na jumla ya ghorofa 50 , Jumba la Carlton lilikuwa jengo refu zaidi katika Ulimwengu wa Kusini .

3. Britam Tower, Kenya

Britam Tower, lina urefu wa mita 200 na limejengwa katika eneo la Upper Hill jijini Nairobi . Lilifunguliwa rasmi kwa umma 2018 , na kulipiku jumba la UAP Old Mutual kama jumba refu zaidi nchini Kenya.

Jumba hilo lenye ghorofa 31 ambalo lilianza kujengwa mwaka 2013 lilikamilika mwezi Septemba 2017, na linajivunia muundo wa kipekee.

Mwaka 2018, Britam Tower lilikuwa jumba la kwanza barani Afrika kukabidhiwa taji la tuzo la Emporis Skyscraper lenye historia ya miaka 19 baada ya kutajwa kuwa jumba la kumi bora duniani.

Likiwa katika eneo la Upper hill jijini Nairobi jumba hilo lenye ghorofa 31 linatoa mandhari ya kupendeza ambapo unaweza kuona eneo la kati la mji mkuu wa Nairobi pamoja na maeneo ya viungani mwake ikiwemo mbuga ya wanyama pori ya Nairobi.

Ujenzi wake ulikamilika mnamo mwezi Novemba 2017, na sasa linamilikiwa na kampuni ya bima ya Britam Life Assurance Limited.

Katika siku nzuri isio na mawingu unaweza kuona Mlima Kilimanjaro pamoja na Mlima Kenya juu ya jumba hilo.

Pia ndio jumba refu zaidi Afrika mashariki

4. Makao makuu ya CBE, Ethiopia

Jumba hilo lina urefu wa mita 198 na linamilikiwa na benki ya biashara ya Commercial Bank ya Ethiopia (CBE) katikati ya mji mkuu wa Addis Ababa Ethiopia.

Ujenzi wake umemaliza utawala wa jumba la mikutano la muungano wa Afrika AU mjini humo.

Jumba hilo lenye ghorofa 46 ambalo liko karibu na hoteli ya Ras Desta katika barabara ya Damtew lina mita 150,000 mraba likiwa makao makuu ya benki hiyo inayomilikiwa na serikali.

Ujenzi wa jumba la Nairobi GTC Office Tower, ambalo ndilo refu kati ya majumba sita ya Global Trade Centre, limeleta mgeni mpya katika orodha ya majumba marefu nchini Kenya.

Jumba hilo lenye urefu wa mita 184 na ghorofa 43 ndilo linalotarajiwa kuwa makao makuu ya kampuni ya China Avic ambayo inataka kujikita katika eneo la Westland mjini Nairobi.

Jumba hilo ambalo ujenzi wake ulianza Julai 2015 liLIkamilika mwezi Disemba 2020.

5. Nairobi GTC Office Tower

Ujenzi wa jumba la Nairobi GTC Office Tower, ambalo ndilo refu kati ya majumba sita ya Global Trade Centre, limeleta mgeni mpya katika orodha ya majumba marefu nchini Kenya.

Jumba hilo lenye urefu wa mita 184 na ghorofa 43 ndilo linalotarajiwa kuwa makao makuu ya kampuni ya China Avic ambayo inataka kujikita katika eneo la Westland mjini Nairobi.

Jumba hilo ambalo ujenzi wake ulianza Julai 2015 liLIkamilika mwezi Disemba 2020.

6. Ponte City, Afrika Kusini

Jumba la Ponte City lenye urefu wa mita 172.8 lipo katika makaazi ya mji wa Johannesburg Afrika Kusini. Likiwa limejengwa 1975, jumba hilo lenye ghorofa 54 limetajwa kuwa jumba la kwanza la umbo la mviringo kujengwa Afrika

7. UAP Tower, Kenya

Likiwa katika Upper Hill, Nairobi, UAP Old Mutual Tower yenye urefu wa mita 163 lilikua jengo refu zaidi nchini Kenya lilipofunguliwa Julai 2016 baada ya ujenzi wa zaidi ya miaka mitano.

Jengo hilo la ghorofa 33, ambalo tangu wakati huo limepoteza hatimiliki ya Britam Tower, linatoa takriban futi za mraba 300,000 za nafasi ya ofisi ya Daraja A katika wilaya ya kibiashara inayokua kwa kasi zaidi Nairobi.

Likisimama kwenye mwinuko wa futi 5,700 juu ya usawa wa bahari, UAP Old Mutual Tower lililishinda jumba la Rahimtulla Tower kama sehemu ya juu zaidi jijini Nairobi.

8. NECOM House, Nigeria

Kulingana na mtandao wa CK , Jumba la NECOM lililojulikana kama NITEL Tower na awali The NET Building, lina urefu wa mita 158 katikati ya mji wa Lagos .

Ndilo jumba refu rasmi nchini Nigeria na eneo zima la Afrika magharibi. Jumba hilo lililokamilika 1979 ndio makao makuu ya kampuni ya Telecomunication Ltd iliokuwa ikimilikiwa na serikali.

NECOM House iliundwa na wasanifu majengo wa Ghana Nickson Borys & Partners na ilijengwa na kampuni ya Costain Group yenye makao yake Uingereza. Ilichukua nafasi ya Cocoa House kama jengo refu zaidi nchini Nigeria

9. Tanzania Ports Authority Tower, Tanzania

Jumba la Tanzania Ports Authority Tower, lina urefu wa mita 157 katika mji wa kibiashara wa Dar esa Salaam.

Baada ya ujenzi wake kukamilika 2016, jumba hilo lenye urefu wa mita 40 ndio makao makuu ya halmashauri ya Bandari nchini Tanzania.

PSPF Towers ni jengo majengo mawili kwa moja yenye urefu wa mita 153 huko Dar es Salaam, Tanzania. Jengo hilo la orofa 35 limeundwa na muundo wa kunyumbulika na linaweza ofisi nyingi.

10. PSPF Towers, Tanzania

Jengo la PSPF Towers mjini Dar es Salaam nchini Tanzania lina urefu wa mita 153 na linatumika kama ofisi.

Majumba marefu zaidi duniani 2023

1.Burj Khalifa. Burj Khalifa. ...

2.Merdeka 118

3.Shanghai Tower. ...

4.Abraj Al Bait. ...

5.Ping An International Finance Center. ...

6.Goldin Finance 117. ...

7.Lotte World Tower. ...

8.One World Trade Center.

9.Chow tai Fook Finance Centre

10.Tianjin Chow Tai Fook Binhai Center