Je, ni wakati wa viongozi wakongwe wa Marekani kustaafu?

Nomia Iqbal & Alex Lederman

BBC News, Washington, DC

Ghafla neno lisilojulikana, "gerontocracy," ambalo linamaanisha serikali inayotawaliwa na watu ambao ni wakongwe zaidi ya wengine, sasa linazidi kuwa sehemu ya msamiati wa Wamarekani.

Sio mengi yanayowaunganisha wapiga kura wa Democrat na Republican lakini suala moja linajitokeza: wengi wanafikiri viongozi wa Marekani ni wazee sana.

Mengi yamesemwa kuhusu enzi za Rais Biden na anayeweza kugombea dhidi yake Donald Trump.

Bw Biden anatimiza umri wa miaka 81 Jumatatu, na kumfanya kuwa rais mkongwe zaidi , huku Bw Trump akiwa na umri wa miaka 77.

Lakini hao hata sio wazee zaidi ukiwalinganisha na Mdemokrat Nancy Pelosi mwenye umri wa miaka 83 ambaye anasema atawania kiti cha urais tena mwaka ujao, Naye Chuck Grassley wa Republican ndiye Seneta mkongwe zaidi nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 90.

Likitokana na neno la Kilatini senex, linalomaanisha 'mzee' na 'mwanaume mzee', Seneti daima imekuwa nyumbani kwa baadhi ya wanaume na wanawake wakongwe zaidi nchini.

Hata hivyo, kwa umri wa wastani wa miaka 65, Seneti ya leo ndiyo kongwe zaidi kuwahi kuhudumu , kulingana na Profesa Kevin Munger na mwandishi wa Generation Gap: Why the Baby Boomers Still Dominate American Politics and Culture.

"Tunatarajia watu wawe na umri wa miaka 50 na 60 - ni jambo la busara kabisa kuwa na watu wenye uzoefu huo wa kuendesha nchi," aliiambia BBC. "Lakini tunazungumza juu yake sasa kwa sababu tuna watu ambao wako katika miaka ya 80 na wanaendesha nchi na hilo ni jambo la kipekee."

Bw Munger alisema sababu za uongozi huu wa sasa wa uzeeni zinatofautiana. Wengi hawawezi kuachia mamlaka, jambo ambalo linasababishwa na kutokuwa na ukomo muhula.

Kuongezeka kwa idadi ya watoto (waliozaliwa kutoka 1946 hadi 1964) pia kulimaanisha kuwa kundi kubwa la viongozi waliochaguliwa wamekaribia umri wa kustaafu.

"Tunashuhudia matokeo yake miongo kadhaa baadaye, na hali hii inajitokeza zaidi kutokana na matukio maalum ya kihistoria na taasisi za kisiasa za Marekani," alisema.

Kwa kuwa ni wachache wanaoondoka madarakani, fursa za vijana kujiunga na nyadhifa hizo ni chache. Wale ambao wameweza kuiongia katika nyadhfa hizi wanasema mara nyingi wanaweza kudharauliwa kwa sababu ya umri wao.

Mbunge wa Democrat wa Florida Maxwell Frost, alikua mbunge mdogo zaidi wa Congress – alipokuwa mbunge wa Gen-Z - alipochaguliwa mwaka huu akiwa na umri wa miaka 25.

"Nakumbuka nilipokuja Congress kwa mara ya kwanza na nilipokuwa nikienda kwenye mlango wa wabunge ilinibidi kuonyesha kadi yangu," aliiambia BBC. "Na yule jamaa wa usalama aliwaita baadhi ya marafiki zake na alikuwa akiniuliza umri gani? Na wewe ni mweusi pia?"

"Wako sahihi! Sionekani kama mjumbe wa Congress."

Ingawa kuwa mdogo kunampa mtazamo katika kizazi ambacho wenzake wazee hawawezi kushiriki, anasema kwamba sio Wamarekani wote vijana ni sawa.

"Siamini kuwa mimi ndiye muwakilishi pekee wa Gen Z," alisema. "Kuna vijana wengi ambao wangesema siwakilishi kila kitu wanachoamini. Haitoshi tu kuwa na vijana katika kumbi hizi."

Mfano halisi: Bw Frost alimpongeza Rais Biden kwa kuyapa kipaumbele mauala kama vile mikopo ya wanafunzi, kuwa kipaumbele.

"Sio kila kitu ni kuhusu umri."

Bado, wengi wanatoa wito kwa kizazi cha wazee kujiuzulu ili kutoa nafasi kwa nyuso kama za Bw Frost.

Seneta wa Democrat Dianne Feinstein, aliyefariki mapema mwaka huu aliwa na umri wa miaka 90 alikabiliwa na simu nyingi zilizomtaka kujiuzulu kufuatia wasiwasi wa muda mrefu kuhusu afya yake.

Wasiwasi huo huo sasa unazushwa kuhusu kiongozi wa Wachache katika Seneti ya Republican Mitch McConnell mwenye umri wa miaka 81.

Alionekana kuishiwa nguvu mara mbili kwa muda mrefu wakati wa mikutano miwili ya waandishi wa habari, na kusababisha kuibuka kwa maswali kuhusu afya yake.

Utafiti wa taasisi ya Pew Research uligundua 79% ya Wamarekani wanataka vikomo vya umri kwa maafisa wa shirikisho na mabadiliko ya kizazi.

Baadhi ya vijana wamepata mafanikio katika ngazi ya ndani. New Hampshire ina idadi ndogo ya watu lakini lina bunge kubwa zaidi nchini Marekani na kwa kuchaguliwa kwa Valerie McDonnell, Mrepublican, akiwa na umri wa miaka 18 kama mbunge wa jimbo hilo kumemfanya kuwa mbunge wa jimbo umri mdogo zaidi.

Mwanafunzi huyo wa chuo alisema hataki umri wake uwe kitu cha kuzingatia, lakini anauona kama rasilimali.

"Ikiwa tuna watu wenye umri wa miaka 18 hadi 25 katika nchi hii ambao wana uwezekano mdogo wa kupiga kura, nadhani mengi ya hayo ni kwa sababu hawajioni wakiwakilishwa," aliambia BBC. "Kwa hivyo sasa nimekuwa na baadhi ya wanafunzi wenzangu ambao walijiandikisha kupiga kura, na kwa upole kunipigia kura yao ya kwanza."

Bi McDonnell, ambaye sasa ana umri wa miaka 19, alisema kuwa kijana kunaweza kuleta mabadiliko, kwa mfano wakati wa kujadili muswada kuhusu mitandao ya kijamii hivi majuzi.

"Ninahudumu katika kamati ya elimu ya watu 20. Na kwa kweli ninahisi kwamba kamati yangu ilithamini maoni yangu, kuwa mtu ambaye angeweza kutoa maelezo ya kisasa ya jinsi mambo yalivyo."

Anahudumu pamoja na rafiki yake na mwenzake wa Republican Joe Alexander, 28, ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge la jimbo miaka mitano iliyopita.

"Nadhani nilikuwa na umri wa miaka 10 na mama yangu alinipeleka kwenye kibanda cha kupigia kura. Alisema, hili ni mojawapo ya mambo muhimu unayoweza kufanya: kufanya sauti yako isikike kwa kupiga kura. Hivyo ndivyo nilivyovutiwa na siasa,"

alisema, akionyesha tattoo yake ya We The People kwenye mkono wake wa juu.

Bw Alexander alisema alichochewa kutafuta nafasi ya uongozi kutokana na gharama ya nyumba. Kura za maoni zinaonyesha kuwa ni suala muhimu zaidi katika New Hampshire.

Wote Bw Alexander na Bi McDonnell wameungwa mkono na Run GenZ, shirika linalolenga kusaidia kuunda kizazi kijacho cha viongozi wa kihafidhina. Mkurugenzi wake mtendaji, Mason Morgan mwenye umri wa miaka 28 kutoka Texas, alisema wengine wanadhani kama wewe ni kijana, huna uzoefu unaohitajika kufanya kazi hiyo.

"Kila mara huwa nasisimka zaidi, ninapozungumza na mtu ambaye alianza biashara yake akiwa na umri wa miaka 16, na hajapata elimu ya miaka minne ya chuo," alisema. "Aina hizo za watu huleta mtazamo tofauti."

Kuwa mwakilishi wa jimbo hakuna faida yoyote - mshahara ni $100 kwa mwaka New Hampshire. Wakatihawahudumu katika wilaya yao ya karibu, Bi McConnell anafanya kazi kwenye duka la mboga, na Bw Alexander ni mhudumu wa baa wa muda. Kevin Munger, profesa wa sayansi ya siasa, alisema ukosefu wa fedha unaweza kufanya kuwa vigumu kwa kizazi kipya kuifanya.

"Wazee wana pesa nyingi zaidi, haswa wale walio na miaka ya 70 na 80," alisema.

Lakini Bw Alexander alisema kwamba 'sio tu kuhusu umri, lakini nguvu ya akili ya mtu.' Anadhani kuna nafasi kwa vijana na wakongwe katika siasa.

"Ni muhimu tukithamini kizazi ambacho kimeleta mengi, na kimetuweka hapa tulipo. Lengo langu kama mwakilishi ambaye ni mdogo, ni kushirikiana na kizazi hicho. Ni washirika katika vita."

Kuna ishara kwamba viongozi wakongwe wanaanza kuondoka, na wakongwe tayari wanaweza kuondoka ili kutoa nafasi kwa mpya.

Seneta wa Democrat Joe Manchin na Seneta wa Republican Mitt Romney, wote wenye umri wa miaka 76, walisema hawatawasilisha maombi yao ya kuchaguliwa tena.

Patrick Leahy, aliyekuwa wa tatu katika kinyang’anyiro cha urais, alistaafu kutoka Seneti mapema mwaka huu, kabla ya kutimiza umri wa miaka 83.

Mdemocrat huyo alisema zaidi wanapaswa kufuata nyayo.

"Nimeona wengi ambao walipaswa kuondoka Congress na hawakuondoka. Wengine walikufia ofisini. Sikutaka kuwa katika kundi hilo," alisema kutoka nyumbani kwake huko Vermont, ambako anaishi sasa.

Alipoondoka, alikuwa mwanachama wa muda mrefu zaidi wa Congress.

Seneta (mhafidhina mwenye cheo hicho maishani) Leahy alisema alifanya yote aliyoweza akiwa madarakani, na alishuhudia nyakati za kihistoria ambazo "zilikuwa za kuhuzunisha na za kutia moyo", lakini ulikuwa wakati wa kuondoka, hasa kufuatia upasuaji wake wa nyonga.

"Hawana maisha mengine ya kuwa waaminifu. Kuna wengine wanataka ukuu wake."Je, Seneta Leahy anajaribiwa kurejea ulingoni? Kama rafiki yake Nancy Pelosi?'Hapana!' alipiga kelele, kisha akatabasamu.

Ingawa bado anajihusisha na siasa za ndani, anafurahia kufundisha katika chuo kikuu cha eneo lake na kutumia wakati na mke wake, watoto na wajukuu.

"Nina umri wa miaka 80. Ni wakati wa mtu mwingine." alisema.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi