Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchunguzi wa machapisho ya uwongo kuhusu tetemeko la ardhi la Uturuki
Saa chache baada ya tetemeko la ardhi lililokumba Uturuki na Syria, maudhui ya uongo na ya kupotosha yalianza kusambazwa mtandaoni.
Picha na video kutoka kwa majanga yaliyofanyika kitambo katika nchi zingine zilishirikishwa mitandaoni na watu waliodai kwamba walionyesha uharibifu uliosababishwa na mitetemeko ya Jumatatu.
Tumeangazia baadhi ya mifano ya picha na video zilizovuma sana mitandaoni.
Kiwanda cha nyuklia
Ujumbe mmoja wa Twitter - kutoka kwa mtumiaji aliyetjibitishwa - ulidai kuonyesha mtambo wa nyuklia ukilipuka, kutokana na tetemeko la ardhi nchini Uturuki.
Video hiyo ilipata maoni zaidi ya milioni 1.2
Chapisho hilo pia lilikuwa limeandikwa maneno "Haijathibitishwa, je hii ni kweli?".
La haikuwa.
Upekuzi wa picha hizo kupitia mtambo wa kutafuta matukio ili kubaini kama ziliwahi kuchapishwa mtandaoni, ulifichua kwamba ni kweli zilitokana na mlipuko wa Beirut mnamo Agosti 2020, ambao ulisababisha vifo vya takriban watu 200.
Twitter baadaye iliweka lebo kwenye ujumbe huo, ikifafanua chanzo halisi.
Kuporomoka kwa jengo la Florida
Mapema Jumatatu, video inayodai kuonyesha kuporomoka kwa jengo nchini Uturuki ilisambazwa mtandaoni, na ilitazamwa na zaidi ya watu milioni moja kwenye Twitter.
Lakini, utafutaji wa fremu muhimu kutoka kwa video hii kwenye Google ulibaini klipu hiyo kweli inaonyesha kuanguka kwa jengo huko Florida mnamo Juni 2021, picha ambazo zilishirikishwa sana mitandaoni wakati huo.
Tsunami Indonesia
Mcheshi wa Uingereza mwenye asili ya Iran Omid Djalili aliweka video ya kile alichodai kuwa "tsunami baada ya tetemeko la ardhi kupiga pwani ya Uturuki" kwenye akaunti yake ya Twitter. Imetazamwa karibu mara 300,000.
Video hiyo inaonyesha wimbi kubwa likisomba majengo karibu na ufuo, huku watu wakikimbia kuokoa maisha yao.
Lakini baada ya kupiga picha na kuzitafuta kwenye mtandao tulibaini kuwa klipu hiyo ni ya Septemba 2018 na ilikuwa ya kutoka Indonesia.
Ilionyesha matokeo ya tetemeko la ardhi la kiwango cha 7.5 ambalo lilikumba kisiwa cha Sulawesi, na kusababisha tsunami iliyoharibu mji wa pwani wa Palu.
Baada ya watu kumweleza hilo, Bw Djalili alitweet tena na kusema, "Nafahamishwa kuwa hii HAIKUWA Uturuki jana ... alitweet kwa hisia usiku wa manane kutoka kwa vyanzo vya kuaminika."
Kuanguka kwa kiunzi cha Japan
Chapisho lingine kwenye Twitter lilionyesha video ikiwa na likianguka chini kutoka juu ya jengo.
Tweet hiyo ya uwongo ilidai kwamba hali hiyo ilisababishwa na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na ilishirikishwa katika majukwaa mengi na kupata maelfu ya maoni.
Video hii kwa kweli ilitokana na tukio huko Japan mwaka wa 2016.
Iliwekwa na mtumiaji huyo ambaye alichapisha picha za mlipuko wa Beirut.
Picha ya mbwa ilyejawa na hisia
Picha ya mbwa akiwa amelala juu ya vifusi, huku mkono wa mtu aliyekwama ukionekana nje ya vifusi, ilisambazwa sana mtabaoni baada ya tetemeko hilo, ikiambatana na nukuu "picha ya siku ya kuhuzunisha" na hastag ya Uturuki.
Picha hiyo imetazamwa zaidi ya mara milioni 1.4 kufikia sasa.
Lakini utafutaji wa picha kwa kutumia teknolojia ya Lenzi ya Google inayopatikana kwa urahisi ulionyesha picha sawa na hiyo iliyoandikwa "Mbwa anatafuta watu waliojeruhiwa katika magofu baada ya tetemeko la ardhi".
Picha hiyo ni ya Oktoba 2018, ikithibitisha kuwa haina uhusiano na tetemeko la ardhi ya wiki hii.
Ripoti ya Shayan Sardarizadeh, Merlyn Thomas na Adam Robinson.