Fursa ya mwisho ya kombe la Dunia kwa Messi na Modric

Washindi wawili wa tuzo ya Ballon d'Or- wanaovalia jezi nambari 10. Wachezaji walioshindwa katika fainali ya kombe la Dunia, Ni manohodha wawili wanaoongoza timu zao , waliosalia na nafasi moja kila mmoja wao kabla ya kustaafu katika soka.
Ni vigumu kuwapuuza Lionel Messi wa Argentina na Luka Modric wa Croatia kama wachezaji tofauti katika nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia Jumanne.
Huku Messi wa Paris St-Germain akiwa na umri wa miaka 35 sasa na Modric 37 wa Real Madrid, inaonekana kuna uwezekano mkubwa mchezo wa fainali au wa kutafuta mshindi wa tatu wikendi hii ndio ambapo maisha yao ya Kombe la Dunia yataisha.
Kwa hivyo wawili hao wanalinganishwa vipi na ni yupi ataongoza nchi yake kwenye fainali dhidi ya Ufaransa au Morocco siku ya Jumapili?
Je wanalinganishwaje katika kombe hili la Dunia?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wachezaji wote wawili wamekuwa muhimu katika harakati za nchi zao kwenye Kombe hili la Dunia, na wote walifunga katika mechi za ushindi wao kupitia mikwaju ya penalti ya mechi za robo fainali.
Messi alipiga mkwaju wa kwanza wakati Argentina ilipoilaza Uholanzi, huku Modric akifunga bao la tatu la Croatia katika ushindi wao dhidi ya vinara Brazil.
Modric ndiye mchezaji wa kwanza kufunga penalti tatu katika mikwaju ya penalti kwenye Kombe la Dunia (pia alifunga dhidi ya Denmark na Urusi mnamo 2018).
Katika dakika 90 au 120, Messi ni moto wa kuotea mbali. Amefunga mabao manne na kusaidia mawili, wakati ambapo Modric bado hajaandikisha bao au asisti yoyote - hata hivyo Messi anacheza mbele, huku Modric akiwa kiungo mchezeshaji.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Nyota wa PSG Messi alifunga penalti dhidi ya Saudi Arabia, akafunga na kusaidia bao dhidi ya Mexico na akapoteza penalti yake dhidi ya Poland katika hatua ya makundi.
Alifunga bao la kwanza dhidi ya Australia katika hatua ya 16 bora na kusaidia bao la kwanza dhidi ya Uholanzi katika robo fainali, kabla ya kufunga bao la kwanza dakika ya 73 - kupitia mikwaju ya penalti.
Akizungumza kwenye BBC One, Martin Keown alisema: "Lionel Messi anaendelea kutengeneza. Ilikuwa penalti ya ubora. Yuko katika hali bora. Kujiamini kwake kunawapatia motisha wachezaji wenzake .
Kufuatia ushindi wa Argentina dhidi ya Australia, mlinzi mwenzake wa zamani wa Uingereza Rio Ferdinand alisema: "Mchezo bora wa kibinafsi kutoka kwa mchezaji kwenye Kombe hili la Dunia. Alikaribia kuwa kama mungu. Sijaona kitu kama hiki."
Naye mchezaji mwenzake wa zamani wa Argentina, Pablo Zabaleta alisema: "Nadhani Messi anajua kwamba hili ni Kombe lake la mwisho la Dunia na unaona kabisa kwamba anafurahia."
Kiungo wa zamani wa Tottenham Hotspur Modric alivutia jicho la Micah Richards katika robo fainali ya Croatia dhidi ya Brazil.
"Tulifikiri lingekuwa Kombe lake la mwisho la Dunia," beki huyo wa zamani wa Uingereza alisema kwenye BBC One. "Baadhi ya pasi alizopiga, kudhibiti kasi - aliamuru kwa kasi yake na Brazil haikujua la kufanya."
Modric alibadilishwa kabla ya mikwaju ya penalti katika ushindi wa 16-bora wa Croatia dhidi ya Japan - lakini alibakia dhidi ya Brazil.
"Tena, Luka aliongoza kwa dakika 120 na alikuwa kichwa cha timu," Kocha wa Croatia Zlatko Dalic alisema. "Haiaminiki jinsi anavyocheza kwa umri wake, na hakuchoka.
"Tulipojipata nyuma kwa magoli, tulikuwa tunafikiria kuchukua nafasi ya kiungo wa kati na kumuuliza hali yake ikoje. Alisema bado yuko tayari kabisa. Alionyesha tena kuwa ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani."
Messi amefanya mashambulizi mengi (25) na mashuti 12 yaliomlenga kipa kuliko mtu mwingine yeyote katika Kombe la Dunia - huku Mfaransa Kylian Mbappe, mchezaji mwenzake wa Paris St-Germain, akishika nafasi ya pili kwa viwango vyote viwili. Hatahivyo Mbappe anamuongoza kwa 5-4 katika mbio za kuwania taji la mchezaji mwenye magoli mengi.
Wachezaji wanne pekee wamepiga pasi zenye mafanikio zaidi katika safu ya mashambulizi kuliko 201 za Modric; Messi ni wa nane kwenye orodha hiyo akiwa na 171. Modric amepiga krosi tano kwa wingi, 28, kwenye michuano hiyo.
Modric pia amevutia zaidi safu ya nyuma uwanjani, huku wachezaji wawili pekee wakiwa wameshinda mpira mara nyingi (39) au kupenya zaidi (nane) kuliko raia huyo wa Croatia.
Katika ukadiriaji mdogo wa kisayansi wa wachezaji wa BBC Sport, kama ilivyochaguliwa na wasomaji wetu, wastani wa Messi zaidi ya michezo mitano ni 7.01, huku Modric akiwa 7.46.
Je, sifa zao za kimataifa zinalinganishwaje?
Fainali mbili zilizopita za Kombe la Dunia zimeshuhudia mmoja kati ya wawili hawa akishindwa .
Mnamo 2014, Argentina ya Messi ilipoteza 1-0 kwa Ujerumani kupitia bao la Mario Gotze la muda wa ziada. Miaka minne iliyopita, Croatia ya Modric ilichapwa 4-2 na Ufaransa.
Wote wawili walishinda taji la mfungaji bora, tuzo ya mchezaji bora wa mashindano, katika mchakato huo. Na wote wawili wana uwezo wa kufikia viwango vya juu katika mchezo wa Jumanne.
Messi atafikia rekodi ya Lothar Matthaus ya mechi nyingi zaidi za Kombe la Dunia (25). Kisha angevunja rekodi ya Mjerumani huyo mwishoni mwa juma katika mechi ya fainali au ya kutafuta mshindi wa tatu.
Messi amefunga mabao 10 kwenye Kombe la Dunia. Ni wachezaji saba pekee ambao wameweza kufanikiwa zaidi - huku Mjerumani Miroslav Klose akiongoza kwa 16. Yuko goli moja tu nyuma ya Sandor Kocsis wa Hungaria na Mjerumani Jurgen Klinsmann, na mawili nyuma ya Pele.
Tayari anashikilia rekodi ya kutoa pasi nyingi zaidi za mabao katika michezo ya mtoano ya Kombe la Dunia, akiipita rekodi ya zamani ya Pele ya mabao manne katika mechi yao ya mwisho.
Messi amefunga na kusaidia bao katika mechi tatu tofauti za Kombe la Dunia, zikiwemo mbili za mwaka huu. Tangu data hiyo iliporekodiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1966, hakuna mchezaji aliyefanya hivyo katika michezo minne.
Amefunga mabao 95 katika mechi 170 - rekodi zote za kitaifa.
Modric ameshinda rekodi ya Croatia mara 160 na kufunga mabao 23 ya kimataifa.
Modric atakuwa mchezaji wa nje mwenye umri mkubwa zaidi kuanza michezo sita kwenye Kombe moja la Dunia - akimshinda beki wa pembeni wa Brazil Nilton Santos, ambaye alikuwa ametimiza umri wa miaka 37 mwaka 1962.
Amecheza mechi nyingi zaidi za Kombe la Dunia (17) na mechi nyingi zaidi kwenye mashindano makubwa (30) akiwa na Croatia - kabla ya nusu fainali hii.
Messi anajivunia taji moja la Copa America analoonyesha katika maisha yake ya kimataifa, wakati Modric bado hajashinda kombe.
Pia kuna ulinganifu mzuri kati ya taaluma ya wachezaji. Messi alifunga bao lake la kwanza la Argentina na Modric akaichezea Croatia kwa mara ya kwanza katika mchezo huo huo - mechi ya kirafiki kati ya timu hizo mnamo Machi 2006, ambayo Croatia ilishinda 3-2.
Vipi kuhusu taaluma zao kwa ujumla?
Nusu fainali hii itakuwa mchezo wa 1,002 wa maisha ya Messi kwa klabu na nchi. Amefunga mabao 790 na kutoa asisti 339.
Takwimu za kazi za Modric ni ngumu zaidi kuwa na uhakika nazo kutokana na vipindi vyake huko Croatia na Bosnia-Herzegovina kwa Dinamo Zagreb, Zrinjski Mostar na Inter Zapresic ambavyo havijarekodiwa vizuri.
Wote wameshinda Ballon d'Or, Messi mara saba na Modric mwaka 2018. Gwiji wa Ureno Cristiano Ronaldo na mshambuliaji wa Ufaransa Karim Benzema ndio wachezaji wengine pekee walioshinda tangu 2007.
Modric ameshinda Ligi ya Mabingwa mara tano dhidi ya nne za Messi - wakati wote wameshinda mataji ya ligi katika nchi mbili.
Rekodi za wachezaji katika ligi tano bora za Ulaya na Ligi ya Mabingwa.












