Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trigger mechanism ni nini na ipi hatari zake kwa Iran?
- Author, Reza Sepehri
- Nafasi, Mwandishi
- Muda wa kusoma: Dakika 9
Alhamisi, tarehe 28 Agosti 2025, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zilianza rasmi mchakato wa kuanzisha mfumo unaoitwa Trigger Mechanism, ambao unalenga kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran kwa njia ya kufanywa bila kufikiri.
Hatua hii inafuatia vitisho vya awali kutoka kwa nchi hizo tatu, ambazo zilikuwa zimeonya serikali ya Tehran kuhusu uwezekano wa kurejeshwa kwa vikwazo vya kimataifa kupitia mfumo huo, baada ya Iran kutangaza kusitisha kwa hiari ushirikiano wake na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA).
Uamuzi huo wa Iran ulitolewa kama majibu kwa mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Israel na Marekani dhidi ya miundombinu ya nyuklia ya Iran.
Mfumo huu wa kuchokoza ulitambuliwa rasmi ndani ya Makubaliano ya Nyuklia ya Iran (JCPOA) yaliyoafikiwa tarehe 14 Julai 2015.
Sasa, takriban muongo mmoja baada ya makubaliano hayo kushindwa kufanikishwa kwa ukamilifu, mchakato wa kuutekeleza umeanzishwa na mataifa ya Ulaya yaliyotia saini makubaliano hayo.
Kwa mujibu wa Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nambari 2231, lililopitishwa mwaka 2015 ili kuidhinisha utekelezaji wa JCPOA, baadhi ya masharti muhimu ya makubaliano hayo yakiwemo yale yanayohusu uwezo wa kuanzisha mfumo wa kurejesha vikwazo yanatarajiwa kufikia kikomo mnamo Oktoba 2025 (Mehr 1404 kwa kalenda ya Iran).
Hivi sasa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, ambazo ni watia saini wa "Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji" unaojulikana kama JCPOA, zimeanza mchakato wa kuamsha utaratibu wa kuwekea vikwazo Iran kwa kutuma barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Marekani ilitoka rasmi kwenye makubaliano ya JCPOA mwaka 2018 chini ya utawala wa Rais Trump, ikarejesha vikwazo kwa Iran.
Hata hivyo, Marekani sasa inajumuika tena kwenye mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Iran wakati Israel ilishambulia Iran kwa kushtukizia lakini kwa sasa mashambulizi yameshitishwa.
Marekani haikuweza kuanzisha "trigger mechanism" kwa kuwa haikuwa tena mshiriki rasmi wa makubaliano hayo, hivyo ilibidi nchi za Ulaya zilizo ndani ya JCPOA zipate jukumu hilo.
Iran ipo katika hali ngumu kisiasa na kiuchumi kutokana na mashambulizi na vikwazo vikali.
Kabla ya mwezi Khordad 1404 (sawa na Mei/Juni 2025), chaguo la kijeshi lilikuwa likichukuliwa na mataifa ya Magharibi kama "fimbo" ya kuishinikiza Iran kutoa ustahimilivu au kukubali masharti fulani katika meza ya mazungumzo.
Lakini sasa kwa kuwa chaguo hilo la kijeshi limewekwa katika vitendo, na madhara makubwa yamesababishwa kwenye miundombinu ya nyuklia ambayo ilikuwa sehemu ya majadiliano, mizani ya nguvu na maamuzi imebadilika kwa kiasi kikubwa.
Viongozi kadhaa wa serikali ya Iran wamesema kuwa, kwa kuzingatia kwamba chaguo la mashambulizi ya kijeshi limetekelezwa huku mazungumzo yakiendelea, hakuna tena kilichosalia cha kupoteza.
Hivyo, Iran inapaswa kukomesha kabisa ushirikiano wake wa nyuklia na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) na kusitisha mazungumzo yote, kisha ijikite tu katika kutekeleza mikakati yake ya kimkakati bila vizuizi vyovyote.
Hata hivyo, mashambulizi ya Israel yameonesha kuwa, si tu anga la Iran halina ulinzi wa kutosha, bali pia Iran imo katika hali ya upweke wa kimataifa isiyokuwa ya kawaida.
Katika mazingira kama haya, kupuuza kwa Iran matakwa ya Magharibi na Israel ambayo Iran imeyaona kuwa ya dhulma na yasiyo ya haki kunaweza kuhatarisha pakubwa usitishaji wa mapigano ulio dhaifu.
Hayo yatachochea kufanikisha kuanzishwa rasmi kwa mfumo wa kurejesha vikwazo, hali ambayo itaiweka Iran katika shinikizo kubwa la vikwazo vya kimataifa hasa wakati huu ambapo uchumi wake uko kwenye hali tete.
Hapa tunajibu maswali ya nini hasa mbinu ya kuchokonoa, jinsi inavyofanya kazi, na ni hatima gani inayoingoja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwa utaratibu huu utatekelezwa rasmi.
Mfumo wa "Trigger Mechanism" ni nini?
Mfumo huu ni njia rasmi ya kusuluhisha mizozo katika JCPOA ambapo pande zinazohusika zinaweza kuanzisha mchakato wa kisheria kusababisha kurejeshwa kwa vikwazo.
Mchakato huu umeelezwa katika aya ya 36 na 37 ya JCPOA, na hufanyika kwa hatua zifuatazo:
- Iwapo nchi mojawapo kati ya zile zilizotia saini JCPOA itahisi kuwa Iran haitekelezi wajibu wake, inaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Kamisheni ya Pamoja (chombo kinachosimamia utekelezaji wa JCPOA).
- Kamisheni hiyo inakuwa na siku 15 za kujaribu kusuluhisha mgogoro huo.
- Endapo hakutakuwa na mwafaka, jambo hilo linawasilishwa kwa mawaziri wa mambo ya nje wa pande husika, ambao pia hupewa siku 15 zaidi kujadili suala hilo.
- Ikiwa mgogoro bado haujatatuliwa, Kamisheni hupewa siku 5 za mwisho kufanya jitihada za mwisho za upatanisho.
- Ikiwa mgogoro haujatatuliwa ndani ya siku 35 kati ya pande husika, basi suala linafikishwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN.
- Ikiwa mwanachama mmoja wa kudumu wa Baraza la Usalama(Marekani, Urusi, China, France ama Uingereza) atapiga kura ya turufu, vikwazo vinaanzishwa moja kwa moja bila kura mpya.
- IAEA ina haki ya kuingia kwenye maeneo yanayoshukiwa ndani ya siku 24, na ukikataa ushirikiano, basi "mbinu za uchokozi " zinaweza kuanzishwa.
Mwaka 2020, Marekani ilijaribu kuanzisha mfumo wa kuchokonoa kwa lengo la kurejesha vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran.
Hata hivyo, idadi kubwa ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama, zikiwemo washirika wa karibu wa Marekani kama Ufaransa na Uingereza, walipinga vikali hatua hiyo.
Nchi hizi zilieleza kuwa kwa kuwa Marekani ilijiondoa rasmi kwenye JCPOA mwaka 2018, haikuwa tena "mwanachama anayeendelea kushiriki" kwenye makubaliano hayo, na hivyo haikuwa na haki ya kisheria ya kutumia mfumo wa mbinu ya kuchokonoa.
Azimio la Baraza la Usalama nambari 2231
Azimio 2231, lililopitishwa tarehe 20 Julai 2015, ni nyaraka muhimu inayosaidia utekelezaji wa JCPOA kwa kiwango cha kimataifa.
Lilitolewa siku sita baada ya kutiwa saini kwa JCPOA kati ya Iran na kundi la mataifa sita (P5+1: Marekani, Uchina, Urusi, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani).
Azimio hilo lilianzisha mfumo wa kisheria wa kuhalalisha utekelezaji wa JCPOA ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa, na kulipa makubaliano hayo hadhi ya kisheria duniani.
Miongoni mwa mambo muhimu yaliyofanywa na azimio hilo ni:
Kufuta maazimio sita ya awali ya Baraza la Usalama yaliyopitishwa kati ya mnamo mwaka 2006 na 2010, ambayo yaliweka vikwazo vya kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia dhidi ya Iran.
Maazimio hayo yalikuwa chini ya Sura ya Saba ya Katiba ya Umoja wa Mataifa, inayoruhusu hatua kali kama vikwazo au hata mashambulizi ya kijeshi iwapo kuna tishio kwa amani ya kimataifa.
Kwa kufutwa kwa maazimio hayo, Iran iliwekwa nje ya Sura ya Saba kwa masharti yaani, ilimradi tu itazingatia wajibu wake chini ya JCPOA, haitakabiliwa tena na vikwazo vya kimataifa.
Mbali na kuondoa vikwazo, Azimio hili liliweka utaratibu wa wazi wa kuyarejesha vikwazo endapo Iran itakiuka ahadi zake, kulingana na masharti ya JCPOA.
Mbinu ya kuchokonoa, uliotajwa katika aya mbili za JCPOA, umepewa uzito wa utekelezaji kupitia aya ya 11 na 12 za Azimio 2231.
Kama ilivyoelezwa awali, kama nchi yoyote ndani ya JCPOA itadai kuwa Iran imekiuka ahadi zake, inaweza kuanzisha mchakato unaoweza kupelekea kurejeshwa kwa vikwazo vyote vya zamani bila hata kupigiwa kura mpya.
Azimio hili pia lina masharti yanayolenga mpango wa makombora wa Iran.
Katika aya ya 3 ya Kiambatisho B, Iran "inahimizwa" kuepuka shughuli zinazoweza kusababisha kutengenezwa kwa makombora yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia.
Hata hivyo, Iran mara kwa mara imesisitiza kwamba mpango wake wa makombora ni wa kiulinzi pekee, na kwa kuwa kifungu hicho kinaanza kwa maneno 'Iran inahimizwa', hakihesabiki kama cha lazima kisheria.
Kuporomoka kwa JCPOA, kujiondoa kwa Marekani na kupungua kwa ahadi za Iran
Makubaliano ya JCPOA yalisainiwa mwezi Julai 2015, yakiwa na lengo la kupunguza mpango wa nyuklia wa Iran kwa masharti ya kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa.
Iran ilikubali:
- Kupunguza kiwango cha urani inayorutubishwa (enriched uranium),
- Kudhibiti kiasi cha nyenzo za nyuklia ilizonazo,
- Kuruhusu ukaguzi mpana zaidi kutoka kwa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomu (IAEA).
Katika miezi ya mwanzo baada ya utekelezaji wa JCPOA mnamo Januari 2016, hali ya kidiplomasia ilikuwa nzuri, na makubaliano yalionekana kufanikiwa.
Lakini Iran haikufaidika vya kutosha kiuchumi, hasa kutokana na hofu ya makampuni makubwa ya kimataifa kushirikiana na Iran, hali ya kutoaminiana na ukosefu wa mifumo madhubuti ya fedha na biashara ya kimataifa.
Miezi michache baada ya utekelezaji wa JCPOA, kampeni ya uchaguzi ya Donald Trump ilianza Marekani.
Trump alikosoa vikali JCPOA na kuitaja kama "mkataba mbaya zaidi kuwahi kufanywa," akiapa kwamba angeufuta.
Alipochaguliwa kuwa Rais, mnamo Mei 2018, serikali yake ilitangaza kujiondoa rasmi kutoka JCPOA, na kuanza kuweka vikwazo vipya na vikali zaidi dhidi ya Iran, licha ya pingamizi kutoka Umoja wa Ulaya, China na Urusi, na ripoti kutoka IAEA kwamba Iran ilikuwa inazingatia mkataba.
Lengo la Trump lilikuwa makubaliano mapana na magumu zaidi, ambayo yangeshughulikia pia:
- Mpango wa makombora wa Iran,
- Uswahiba wake na makundi ya wanamgambo katika Mashariki ya Kati.
Marekani ilianzisha sera ya "maximum pressure" (shinikizo la juu), ambayo:
- Iliathiri vibaya uchumi wa Iran, hasa mauzo ya mafuta,
- Ilishusha kwa kasi thamani ya sarafu ya kitaifa,
- Ilizua hofu miongoni mwa wawekezaji wa kigeni kufanya biashara na Iran kwa kuogopa kuwekewa vikwazo na Marekani.
Juhudi za Umoja wa Ulaya kuokoa JCPOA zilijumuisha kuanzishwa kwa mfumo wa INSTEX (unaolenga kuwezesha biashara ya kibinadamu na matibabu), lakini haukuwahi kufanya kazi kikamilifu.
Kutokana na Marekani kujitoa katika mapatano ya JCPOA, mchakato wa kudorora kwa mapatano hayo ulianza ikiwa ni miezi 16 tu baada ya kutekelezwa kwake rasmi, na Iran nayo ilianza kupunguza hatua kwa hatua ahadi zake kuhusu utumizi wa nyuklia.
Asilimia 60% ya urutubishaji na shambulizi la Israel
Baada ya Marekani kujiondoa, Iran iliendelea kuheshimu masharti ya JCPOA kwa takriban mwaka mmoja, ikitarajia nchi zilizosalia hasa Ulaya zingefidia kwa namna fulani.
Lakini baada ya kushindwa kwa jitihada hizo, Iran ilianza hatua tano za kurudi nyuma, kama ilivyoelezwa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran mnamo Mei 2019, chini ya vifungu vya 26 na 36 vya JCPOA:
- Kuongeza kiwango cha urani na maji mazito kupita kiwango cha JCPOA.
- Kuongeza kiwango cha urutubishaji wa urani kutoka asilimia 3.67% hadi asilimia 4.5%.
- Kufuta vizuizi vya utafiti na uundaji wa mitambo ya kurutubisha (centrifuges) ya kisasa.
- Kufufua shughuli za nyuklia katika kituo cha Fordow na kuingiza gesi katika mitambo.
- Kuacha masharti yote ya kiutendaji kuhusu uwezo, kiwango cha urutubishaji, kiasi cha nyenzo na R&D.
Iran imesisitiza kila mara kuwa hatua hizi zinaweza kurejeshwa kama ilivyokuwa awali iwapo pande nyingine zitatekeleza wajibu wao.
Wakati huo huo, IAEA imeendelea kuripoti kuwa Iran:
- Imepitiliza viwango vya urutubishaji vilivyowekwa,
- Imesakinisha mamia ya mitambo ya kisasa, na
- Imefikia kiwango cha urutubishaji cha asilimia 60% kiwango karibu na cha matumizi ya kijeshi.
Onyo la Ulaya
Ufaransa, Ujerumani na Uingereza walitoa onyo mara kadhaa kuwa mwendelezo wa mwenendo huu unaweza kusababisha:
Kuanzishwa kwa mfumo wa utatuzi wa migogoro, na hatimaye mbinu ya kuchokonoa.
Lakini kwa kipindi hicho, hatua hizo hazikuchukuliwa.
Katika miaka ya baadaye, chini ya utawala wa Ebrahim Raisi nchini Iran na Joe Biden nchini Marekani, majadiliano mapya kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yaliendelea kufanyika lakini hayakufanikisha makubaliano mapya.
Wakati huo huo, hali ya kutoaminiana ilizidi kuongezeka, huku Iran ikiendelea na mpango wake wa urutubishaji wa urani na nchi za Magharibi zikitilia shaka nia yake ya kweli.
Donald Trump, alirejea tena madarakani, na mara moja alirejea kwenye msimamo wake mkali wa awali dhidi ya Iran.
Katika matamshi ya vitisho, aliwataka viongozi wa Iran warejee kwenye meza ya mazungumzo, akiwatuhumu kwa kuchelewesha kwa makusudi na kudai kuwa Iran ilikuwa karibu sana kutengeneza silaha za nyuklia kutokana na kiwango kikubwa cha urutubishaji.
Hatimaye, mnamo tarehe 13 Khordad 1404 (sawa na Juni 2025), Israel ilizindua shambulizi kubwa la kijeshi dhidi ya Iran, ikidai kuwa:
Iran ilikuwa inachelewesha mazungumzo kwa makusudi,
Akiba ya Iran ya urani iliyourutubishwa hadi asilimia 60% ilikuwa tishio la moja kwa moja kwa usalama wa Israel, kwa kuwa iko karibu na kiwango cha silaha za nyuklia (90%).
Licha ya madai ya Tehran kuwa mpango wake wa nyuklia ni wa amani, shambulizi hilo lilisababisha uharibifu mkubwa kwenye miundombinu ya nyuklia ya Iran.
Na kulingana na taarifa za Israel na Marekani, lilichelewesha sana maendeleo ya mpango wa nyuklia wa Iran, huku likizua hali mpya ya kijeshi na kisiasa.