Hezbollah imebadilika vipi tangu vita na Israel mwaka 2006?

Chanzo cha picha, Getty Images
Na Caryn Trobey
BBC News Arabic
Baada ya mfululizo wa mauaji na mashambulizi ya hali ya juu, mvutano kati ya Israel, Hezbollah na Iran inayoungwa mkono na Iran sasa umefikia kiwango cha juu.
Katika kuelewa uwezo wa kijeshi wa kundi hili la wanamgambo wa Lebanon na mgogoro wake wa kihistoria na Israeli ni muhimu kutabiri kile kinachoweza kutokea.
Hezbollah na Israel zimekosolewa kwa vitendo vyao wakati wa maadhimisho ya miaka 18 ya vita vya Julai 2006.
Ukosoaji huo unakuja wakati kukiwa na uwezekano wa vita vipya vya kiwango cha juu kati y apande hizi mbili baada ya miezi 10 ya mapigano makali.
Kwa upande mmoja, Israel ina uwezo wa mashambulio ya angani na wa hali ya juu wa kijasusi, wakati kwa upande mwingine, Hezbollah ina hifadhi kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani za kijeshi.
Ili kuelewa vita kamili kati ya pande hizo mbili, mambo mawili muhimu lazima yazingatiwe: masomo yaliyopatikana kutoka kwa vita vya Julai 2006 na miezi 10 ya mapigano ya kila siku kati ya pande hizo mbili.
Licha ya Israel kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi ya anga nchini Lebanon, jeshi la Israel linahisi kuchoshwa na vita vya muda mrefu zaidi ambavyo Israel imepigana kwa miongo kadhaa katika Ukanda wa Gaza.
Kwa upande wa Hezbollah, wanasema hadi sasa wamepoteza zaidi ya wapiganaji 350 kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel, akiwemo kamanda wao wa ngazi ya juu, Fouad Shukar, na viongozi watatu wa ngazi ya juu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hata hivyo, kundi hilo, ambalo ni kundi la Waislamu wa madhehebu ya Kishia, litapigana katika vita vyovyote vinavyowezekana, vikisaidiwa na miaka kadhaa ya mapigano katika vita vya Syria ambavyo vimesaidia kuzalisha makamanda wapya na wenye uzoefu.
Hezbollah inaungwa mkono na Iran na inapata msaada wa kifedha na kijeshi kutoka kwao.
Kundi hilo limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na nchi nyingi za Magharibi, ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, pamoja na baadhi ya mataifa ya Kiarabu.
Serikali ya Lebanon inalichukulia kundi hilo kuwa ni kundi la upinzani dhidi ya Israel. Katika nchi hiyo, kinatambuliwa kama chama cha kisiasa chenye uwakilishi mkubwa katika Bunge.

Mwaka 2006, vita kamili vilizuka kati ya pande hizo mbili wakati Hezbollah ilipovuka mpaka, na kuwaua wanajeshi wanane wa Israel na kuwateka nyara wawili. Kisha wakataka kubadilishana wafungwa na Israeli.
Waangalizi wanaamini kwamba ikiwa vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hezbollah vitakusanya vikosi vyote vinavyowezekana kujiimarisha kwa ajili ya vita kamili, Israeli inaweza kukabiliana na hali kama iliyokabiliana nayo mwaka 2006: Walianzisha mfululizo wa mashambulizi makali ya anga, yakifuatwa na mashambulizi ya ardhini.
Licha ya kupeleka silaha pamoja na vikosi vyao, hawakuweza kufikia malengo yao ya kuwaokoa wanajeshi wawili waliotekwa nyara wala kuwashinda kijeshi Hezbollah.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vita hivyo vilisitishwa mwaka 2006 kufuatia azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la mwaka 1701. Ilipitishwa kwa kauli moja mnamo Agosti 11, 2006, baada ya siku 34 za mapigano, ambayo ilikuwa maandishi yaliyoidhinishwa kumaliza vita.
Mara tu Israel ilipositisha operesheni zake za mashambulizi, Hezbollah ilisitisha mashambulizi yake ya makombora dhidi ya Israel asubuhi ya tarehe 14 Agosti.
End of Unaweza pia kusoma:

Chanzo cha picha, Getty Images
Mashambulizi ya Hezbollah dhidi ya Israel
Hezbollah ilianza kuyashambulia maeneo ya Israel mnamo Oktoba 8 mwaka jana.
Walisema kuwa wanafanya hivyo "kwa kuunga mkono Gaza". Hii ni baada ya Hamas kushambulia Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023, kujibu mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya raia na wanajeshi kusini mwa Israel. Hamas imeliita shambulio hilo kuwa ni "Mafuriko ya Al-Aqsa".
Hezbollah imetangaza kuwa operesheni hizo zitaendelea hadi pale makubaliano ya kusitisha mapigano yatakapofikiwa katika Ukanda wa Gaza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Israel imeonya kuwa vita na Hezbollah vitairejesha Lebanon katika "Enzi ya Kihistoria", lakini Hezbollah na maafisa wa Israel wamesema wako tayari kwa vita lakini wanapendelea kuepuka mzozo kamili.
Mashambulizi ya mpakani yamewalazimisha zaidi ya watu 90,000 wengi wao wakiwa raia kuyakimbia makazi yao nchini Lebanon, Umoja wa Mataifa umesema.
Shirika hilo limesema raia 100 na wapiganaji 366 wa Hezbollah waliuawa katika mashambulizi ya Israel.
Maafisa wa Israel wanasema mashambulizi ya Hezbollah yamewakosesha makazi raia 60,000 na kusababisha vifo vya watu 33, wakiwemo raia 10.
BBC imechapisha uchambuzi wa picha za satelaiti zinazoonyesha zaidi ya majengo 3,200 kusini mwa Lebanon yaliyoharibiwa kwa sehemu au kikamilifu, huku vyombo vya habari vya Israel vikisema zaidi ya majengo 1,000 yameharibiwa kaskazini mwa Israel.
"Mpinzani mkali zaidi"

Chanzo cha picha, Getty Images
Mtaalamu wa masuala ya kijeshi wa Uingereza Justin Crump anasema Hezbollah inaweza kuwa "adui mkubwa wa Israel kwa sasa" na kwamba iwapo mzozo huo utaongezeka, matukio ya kushtukiza yanaweza kutokea.
"Hezbollah ina kila kitu ilichokuwa nacho mwaka 2006, lakini kwa kiwango kikubwa zaidi," anasema Crump, ambaye alikuwa mshauri wa kijeshi wa London.
Kwa mujibu wa Shirika la Ujasusi la Marekani, Hezbollah ina makombora 150,000 na makombora mengine ya aina mbalimbali pamoja na wapiganaji 45,000. Kiongozi wa kundi hilo, Hassan Nasrallah, awali alidai kuwa lilikuwa na wapiganaji zaidi ya 100,000.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika vita vya Israel vya Julai 2006, walitumia sana makombora ya Katyusha na Grad na makombora ya kupambana na vifaru, pamoja na makombora ya Kornet yaliyotengenezwa na Urusi.
Wakati Israel ina uwezo wa hali ya juu wa mashambulizi ya anga, "Hezbollah ina faida ya ardhi, ambayo inamaanisha kuwa ni vigumu kwa wapinzani kusonga mbele upande wao," Crump anasema.
Hifadhi ya makombora
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hezbollah haifichui ukubwa wa silaha zake au aina ya makombora ambayo iliyo nayo hadi yatakapotumiwa.
Kwa mujibu wa ripoti kadhaa za kijasusi zilizochapishwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, chanzo kikuu cha silaha za Hezbollah ni Iran, huku silaha zikipita katika maeneo ya Iraq na Syria.
Miongoni mwa silaha hizo ni kombora la Almas-3 ya kupambana na vifaru, kizazi kipya cha makombora ya Iran yenye uwezo wa kulenga shabaha kwa usahihi.
Hezbollah pia ilitumia kombora la Burkan dhidi ya Israel kwa mara ya kwanza na kombora la Jihad Mughniyeh, lililopewa jina la kiongozi wa Hezbollah aliyeuawa nchini Syria mwaka 2015.
Amal Saad, profesa katika Chuo Kikuu cha Cardiff na mwandishi wa "Hezbullah: Siasa na Dini", anasema: "Leo tunaona aina ya Hezbollah iliyoendelea zaidi na iliyoendelea kuliko tulivyoona mwaka 2006."
"Hezbollah imekuwa zaidi ya kuwa jeshi mseto ambalo linachanganya sifa za jeshi la kawaida na sifa za vikundi vya kijeshi visivyo vya kawaida," anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Anasema uainishaji huo unatokana na shirika la kijeshi, ukubwa, maendeleo ya mbinu, kiwango cha mafunzo na vikosi maalum vya kitaaluma ambavyo Hezbollah inavyo. Pia inategemea silaha walizonazo, hasa makombora.
Kiongozi wa muda mrefu wa Hezbollah Hassan Nasrallah awali alizungumzia kuhusu makombora ya juu ya kundi hilo yenye uwezo wa kufika ndani ya Israel.
Ali Jasini, mwandishi wa habari wa kijeshi na mchambuzi wa Mayadeen, kituo cha televisheni cha Lebanon kilicho karibu na Hezbollah, alisema taarifa hiyo inaweza kuwa ishara kwamba wana makombora ya masafa mafupi, yanayolengwa kwa usahihi ambayo yanaweza kufikia umbali wa kilomita 300 (maili 190). .

Chanzo cha picha, Getty Images
Vita vya Droni
Mbali na makombora, sehemu kubwa ya vita vya sasa inaweza kutegemea sana ndege zisizo na rubani. Hezbollah inaweza kutumia ndege zisizo na rubani zilizobeba makombora kwa mara ya kwanza.
Mtaalamu wa kijeshi wa Uingereza Justin Crump anasema, Hezbollah inatumia ndege zisizo na rubani kwa njia bora na za ubunifu zaidi.
Mtaalamu huyu wa kijeshi wa Uingereza anaeleza kuwa Hezbollah ilikuwa na kitengo cha ndege zisizokuwa na rubani kabla ya mwaka 2006, lakini zilikua za kijeshi.
"Leo wanategemea zaidi na zaidi ndege zisizo na rubani za kibiashara, kama ilivyo kwa makundi yote yenye silaha na majeshi, kwani jukumu la ndege zisizo na rubani katika vita kwa ujumla linakuwa muhimu zaidi na zaidi."
Vyombo vya habari vya Israel hivi karibuni vilizungumzia juu ya matumizi ya Hezbollah ya ndege isiyo na rubani. Ni ndege isiyo na rubani ya Iran ya aina ya Shahed 101, ambayo haipigi kelele yoyote wakati wa kuruka. Kwa hivyo ni vigumu kuikatiza. Ina uwezo wa kuruka kwa kwa urefu wa chini na haigunduliwi kwa urahisi na rada. Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na Hezbollah, ndege hiyo isiyo na rubani hapo awali ilitumiwa na makundi ya Yemen na Iraq.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jasini anataja kile anachosema ni tofauti kubwa kati ya Hezbollah ya Oktoba 2023 na Hezbollah ya leo: "Jeshi la Israeli lina ubora zaidi ulimwenguni katika ishara za ujasusi, na kuvuruga mawasiliano. Teknolojia za hali ya juu zinapatikana, kwa hivyo uwezo wa Hezbollah kutuma ndege zisizo na rubani nchini Israel kilomita 20 kutoka mpakani, au kutuma ndege isiyo na rubani ili kupiga picha za maeneo nyeti nchini Israel, inaonyesha kuwa kwa maendeleo ya kiteknolojia ya Israeli kwamba wamejifunza masomo na kuonyesha kubadilika kukabiliana nayo."
Hata hivyo, waangalizi wanaona kuwa hii ni kutia chumvi.
Jasini anaeleza, "Suala la mashambulizi ya anga ni gumu kwa sababu sio tu kuhusu kulenga ndege, ni kuhusu hatua zinazoendelea. Je, inawezekana kuangusha ndege kwa siku 10? Huwezi kufanya hivyo tena?" Pia inategemea na lengo. Lengo ni kupunguza idadi ya ujumbe wa anga wa Israeli na ikiwa hilo litatokea, lengo maalum litafikiwa."

Chanzo cha picha, Getty Images
Trump anaamini kuwa Hezbollah inaweza kuwa na silaha zinazotumiwa na waasi wa Houthi nchini Yemen, na kwamba silaha zozote ambazo Hamas au Wahouthi wanazo, pamoja na silaha nyingine, pia zinamilikiwa na Hezbollah.
Anasema: "Makundi haya yote yanashiriki 'habari, teknolojia na silaha'. Miongoni mwake ni Hezbollah."
Kwa mujibu wa Amal Saad, utabiri wowote kwamba vita vitapanuka lazima uzingatiwe katika muktadha wa sasa. Yaani, "umoja wa uwanja" unaojulikana kama
Mbali na Hezbollah ya Lebanon, mhimili huu unajumuisha Hamas ya Palestina na Islamic Jihad, Ansar Allah wa Yemen na vikundi vya Iraq.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran inasema "matokeo yasiyotarajiwa kwa hatua yoyote mpya nchini Lebanon"
Haijulikani ni jukumu gani makundi haya yatahusika nalo katika vita vyovyote vikubwa dhidi ya Hezbollah, ingawa Israel imeonywa.
Kati ya vita vya mwaka 2006 na shambulio la Oktoba 7, 2023 la Hamas kusini mwa Israel, kilikuwa ndio kipindi kirefu zaidi cha amani kilichoonekana katika mpaka wa Lebanon na Israel, licha ya mvutano na ukiukaji wa sheria ya mipaka ya nchi hizo.
Lakini hiyo haimaanishi kuwa maandalizi hayajafanywa kwa kile kinachokuja, ambacho kinaweza kutokea hivi karibuni.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












