Fahamu aina za saratani rahisi kutibu, na zilizo hatari zaidi

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 6

Saratani ni ugonjwa mbaya unaoleta changamoto kwa wahudumu wa afya duniani kote. Ukuaji usio wa kawaida wa seli katika sehemu yoyote ya mwili isiyodhibitiwa huitwa saratani.

Kwa ujumla, ikiwa saratani itagunduliwa katika hatua ya mapema na matibabu sahihi yakatolewa, mgonjwa ana nafasi nzuri ya kupona.

Ni vigumu kueleza hasa namna saratani husambaa kwa haraka. Namna inavyoweza kuwa hatari hutegemea ni hatua gani iliyofikia, na dalili zake zimegunduliwa kiasi gani, alisema Profesa Msaidizi wa Idara ya Upasuaji Oncology ya Hospitali ya Utafiti wa Saratani nchini Marekani Hasan Shahriar Kallol.

Matibabu ya saratani ambayo yameboreshwa ulimwenguni kote pia yana viwango vya juu vya kutibu.

Kulingana NHS, Taasisi ya Kitaifa ya Saratani nchini Marekani na madaktari, hebu tufahamu kuhusu baadhi ya aina za saratani ;

Saratani ambazo ni rahisi kupona

Kwa mujibu wa Kallol, saratani yoyote inaweza kusababisha kifo ikiwa itachelewa kugunduliwa.

Baadhi ya saratani husambaa kwa haraka sana lakini ni rahisi kutibika zikigunduliwa mapema, huku baadhi ya saratani zikiwa husambaa polepole lakini ni vigumu kutibu iwapo zitagunduliwa kwa kuchelewa.

Kuna zaidi ya aina 200 za saratani ulimwenguni na njia tofauti za matibabu. Kwa mfano, kuna aina kadhaa za saratani ya ubongo au damu ambayo inaweza kutibika kwa matibabu.

Saratani ya matiti

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Saratani ya matiti ndio saratani inayojulikana zaidi ulimwenguni. Maendeleo makubwa pia yamepatikana katika matibabu yake.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Saratani ya Marekani, saratani ya matiti ina hatua aina tatu, ambazo hatua ya kwanza au ya chini hukua polepole. Alama hizi hutegemea jinsi seli za saratani zinakua haraka na kwa kasi gani. Sio sehemu ya hatua nne za saratani.

Dalili ni pamoja na kuhisi uvimbe katika titi, chuchu kutokwa majimaji, na mabadiliko katika titi. Saratani ya matiti ni ya kawaida zaidi kwa wanawake zaidi ya umri wa miaka 50.

Unapaswa kuona daktari ikiwa unahisi mabadiliko katika ngozi, mabadiliko katika umbile au ndani ya titi. Ingawa aina hii ya saratani ni ya kawaida zaidi kuliko aina zingine, kiwango cha vifo vya saratani ya matiti ni kidogo sana.

Hata hivyo, ikiwa hatua ya nne imechelewa, matibabu huwa vigumu zaidi, alisema Dk Call

Saratani ya tezi dume

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Saratani ya tezi dume hukua polepole, haswa kwa wanaume wenye umri mkubwa.

Kulingana na tafiti za NHS, wagonjwa wanaweza kuishi muda mrefu bila kuhisi dalili au kutibiwa. Wakati mwingine hata hauhitaji matibabu. Inawezekana kutibiwa na kupona kabisa ikiwa matibabu yataanza mapema.

Hata hivyo, wakati mwingine madaktari huamua kufanya matibabu kwa utaratibu wa kutibu tatizo moja baada ya jingine kwa sababu matibabu yanaweza kusababisha tatizo la nguvu za kiume, au kuathiri uwezo wa kujamiiana na matatizo ya mkojo.

Hivyo matibabu hufanyika baada ya kubaini ugonjwa unahatarisha maisha kiasi gani.

Ugonjwa huu haujatibiwa sana nchini Bangladesh kwa sababu wagonjwa kwa kawaida huenda kwa daktari wakiwa wamechelewa wakati hakuna matibabu mengi yanayopatikana.

Hata hivyo, kwa kuwa ukuaji wake ni wa polepole, hausababishi madhara kwa haraka, alisema Dk Call.

Matatizo ya mkojo huonekana kama dalili kuu, ingawa dalili huwa hafifu katika hatua za mwanzo.

Kama vile kwenda chooni mara kwa mara, kukaza mwendo ili kukojoa na kuhisi kama mkojo hautoki kabisa.

Uwezekano wa kutibu ni mkubwa ikiwa matibabu yataanza mapema kuanzia hatua ya mapema ya ugonjwa.

Saratani ya utumbo

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Saratani ya koloni pia hufahamika kama saratani ya utumbo. Ambapo hudhuru njia ya haja kubwa. Ingawa hizi ni aina mbili za saratani ambazo matibabu yake ni ya kawaida,alieleza Dr Call

"Saratani ya utumbo mara nyingi hutokea kwenye uvimbe ambao, ukiondolewa, huondoa changamoto nyingi. Kwa sababu hukua polepole baada ya miaka mitano mpaka saba, baada ya miaka kumi inageuka kuwa saratani,” alisema.

Mbali na hilo, saratani hii inapotokea, kuna dalili kadhaa. Kuna mambo mengi kama vile mabadiliko kwenye kinyesi, damu kwenye kinyesi au hata damu, usumbufu baada ya kupata kinyesi, maumivu ya tumbo, kupungua uzito, udhaifu.

NHS inashauri kumuona daktari iwapo umeshuhudia dalili moja kati ya hizi katika kipindi cha wiki tatu au zaidi.

Saratani ambazo ni hatari zaidi

Baadhi ya saratani ni hatari zaidi kwa sababu dalili zake hazionekani wazi, na hutokea kwa kuchelewa sana.

Madaktari wanasema kwamba wagonjwa walio na saratani ya ovari, saratani ya mapafu au kongosho kwa kawaida huwajia wakiwa wamechelewa kwa sababu dalili mara nyingi huchelewa kudhihirika.

Saratani ya kongosho

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kongosho iko chini ya tumbo. Husaidia katika usagaji chakula au uzalishaji wa homoni kama insulini.

Dalili zinazoelezwa na NHS ni pamoja na kuwa na rangi ya njano ya macho au ngozi, muwasho kwenye ngozi, kinyesi kubadilika rangi, kukosa hamu ya kula, kuhisi udhaifu mwilini, kupungua uzito bila sababu, homa, kuhara au kuvimbiwa, kushindwa kumeng’enya chakula, maumivu sehemu ya juu ya tumbo wakati wa kula.

Saratani ya mapafu

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Saratani ya mapafu ni aina hatari zaidi ya saratani ambayo hujadiliwa sana.

Kulingana na Kituo cha utafiti wa Saratani, saratani ya mapafu ni saratani ya pili kwa kawaida baada ya saratani ya matiti na kibofu.

Husambaa kwa haraka na hakuna dalili au kiashiria katika hatua za mwanzo.

NHS inataja kuwa zipo dalili kadhaa.

Kama vile kikohozi cha kudumu, kukohoa damu, upungufu wa pumzi endelevu, uchovu na kupungua uzito, maumivu wakati wa kupumua au kukohoa.

Saratani ya umio(oesophagus)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chakula kawaida hufika kwenye tumbo kupitia umio.

“Saratani ya umio haina dalili nyingi, mfano dalili ya kwanza ambayo mgonjwa anapata ni maumivu wakati wa kumeza chakula, inaweza kueleweka kuwa imefikia hatua ya juu sana,” alisema Dk Call.

Kutojisikia vizuri hapo awali, au kuhisi kama gesi au asidi baada ya kula chakula.

Alisema kuwa aina hii ya saratani ni mbaya zaidi.

NHS inasema kwamba dalili kama vile ugumu wa kumeza chakula, kupungua uzito, kiungulia kwa zaidi ya wiki tatu, na kupungua kwa uzito bila sababu hazipaswi kupuuzwa.

Saratani ya ovari

Kiungo muhimu kinachohusishwa na uzazi wa upande wa wanawake ni ovari.

Inachukuliwa kuwa ugonjwa unaoua taratibu kutokana na kile madaktari wanachoeleza kuwa, dalili za awali za saratani hii huwa hazionekani.

Mara nyingi hakuna maumivu katika hatua za mwanzo.

Hata hivyo, ikiwa kuna historia ya aina hii ya saratani katika familia, ni muhimu kuwa makini kuhusu hilo.

Aidha, moja ya dalili zinazotajwa na madaktari ni kupoteza hamu ya kula.

Kando na hayo, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani au CDC kinashauri kuonana na daktari mara moja ikiwa dalili zozote kama vile maumivu ya tumbo, kutokwa na damu ukeni, mabadiliko katika tumbo hudumu kwa wiki mbili au zaidi.

Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Seif Abdalla