Mafanikio manne katika matibabu ya saratani yanayowaongezea wagonjwa maisha

Chanzo cha picha, Getty Images
Na André Biernath
BBC News Brazil
Katikati ya uvumbuzi mwingi wa kiteknolojia na uzinduzi wa dawa, inashangaza kwamba mkutano wa kisayansi unaoongoza ulimwenguni kuhusu saratani umeonyesha dawa zinazojulikana ambazo zimeuzwa katika miaka ya hivi karibuni.
Habari kuu ya tukio hilo inasisitiza ukweli kwamba moja ya changamoto kubwa kwa wataalamu iko katika jinsi ya kuandaa "njia ya matibabu" yenye ufanisi zaidi kwa mgonjwa, au ni wakati gani sahihi wa kutumia kila rasilimali zilizopo, kuanzia upasuaji hadi utoaji wa dawa.
Katika mkutano wa kila mwaka wa 2024 wa Jumuiya ya Marekani ya kliniki za tiba za saratani (ASCO), maelfu ya madaktari walikusanyika katika jiji la Chicago, USA, kujifunza kuhusu mapendekezo mapya ya matibabu ya ugonjwa huo.
Utafiti uliowasilishwa katika tukio hilo unapendekeza njia tofauti za kupambana na saratani ya umio na ya meloma (aina ya saratani inayosambaa kwa kupitia uvimbo unaoota kwenye ngozi) na utafiti huo pia unaelezea kuhusu suluhisho la mambo yasiyotimizwa kwa watu walio na saratani ya mapafu.
Kulingana na madaktari waliohojiwa na BBC News Brazil, habari hii sasa inabadilisha jinsi magonjwa haya yanavyotibiwa katika kliniki na hospitali.
Wataalamu pia wamezingatia matunzo ya mgonjwa na kupekeza hata tiba ya saratani ya uume:
jaribio lililofanywa nchini Brazil linaonyesha aina mpya wa matibabu ya uvimbe huu unaomfanya mgonjwa kukumbwa na aibu na kutengwa na jamii.
BBC News Brazil ilizungumza na madaktari wanaohudhuria ASCO 2024 na huu ni muhtasari wa habari nne kuu za saratani zilizojadiliwa kwenye mkutano huo.
Saratani ya mapafu: namna maisha yanavyoweza kurefushwa
Watu waliogunduliwa kuwa na aina ya kawaida ya saratani ya mapafu, ambayo tayari iko katika hatua ya 3, ambayo ugonjwa huo umeendelea lakini bado haujaenea kwa sehemu zingine za mwili, hawapaswi tena kufanyiwa upasuaji wa matibabu.
Katika visa hivi , wagonjwa wanatakiwa kupata matibabu ya chemotherapy na radiotherapy.
Katikati ya 2017, utafiti uliofanywa na taasisi kadhaa ulimwenguni kote ulifunua kuwa kuongeza kwa immunotherapy (au kuongezewa kinga ya mwili) huongeza sana muda wa kuishi wa watu hawa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Immunotherapy ni aina mpya ya matibabu ambayo hayashambulii moja kwa moja uvimbe wa saratani, lakini badala yake huchochea mfumo wa kinga ya mgonjwa kutambua na kuharibu seli zilizo na ugonjwa.
Kutokana na kazi hii mchanganyiko wa chemotherapy, radiotherapy na immunotherapy vimekuwa mchanganyiko wa kawaida ywa matibabu, angalau kwa visa ambapo kuna upatikanaji wa dawa za kisasa, ghali zaidi.
"Hata hivyo, kuna kundi maalum la wagonjwa katika ulimwengu huu ambao hawafaidiki na immunotherapy, kwasababu huonyesha matokeo sawa na wale ambao walitumia dawa gushi ," anasisitiza mtaalamu wa marathi ya saratani Mariana Laloni, mkurugenzi wa matibabu ya kiufundi wa taasisi ya Oncoclínicas&Co.
Daktari huyo anataja wale ambao wana mabadiliko katika jeni ya EGFR, ambayo hupatikana katika DNA ya asilimia 15 hadi 25 ya watu walioathirika na aina ya kawaida ya saratani ya mapafu. Utafiti uliowasilishwa katika ASCO 2024 ulitafuta suluhisho hususan kwa kundi hili.
Watafiti walitathmini pia iwapo dawa ya osimertinib, kutoka kampuni ya dawa ya AstraZeneca, inaweza kuongeza muda wa maisha ya wagonjwa waliogunduliwa na saratani ya mapafu iliyofikia kiwango cha 3 ambayo inaweza mabadiliko ya jeni ya EGFR.

Chanzo cha picha, Getty Images
Matokeo yalionekana kuwa chanya: katika kikundi kilichopokea dawa hiyo, wakati wa kuishi bila tiba hiyo ulikuwa ni miezi 39.1 (zaidi ya miaka mitatu). Kwa wale wanaotumia placebo, kiwango hiki kilikuwa miezi 5.6.
Laloni anaamini matokeo hayo yanatia moyo na kutoa matarajio mazuri. Hata hivyo, anaamini kuwa bado kuna maswali ambayo hayajajibiwa.
"Bado ni muhimu kujua kama ni vyema kutumia dawa hii mara tu baada ya matibabu ya awali [ ya chemotherapy na radiotherapy] au wakati ugonjwa unaendelea," anasema mtaalamu.
Daktari wa saratani pia anazungumzia kuhusu utafiti mwingine wa saratani ya mapafu iliotajwa katika ASCO 2024.
Kundi la wataalam wa Marekani waliamua kujifunza ikiwa teleconsultations (nushauri wa daktari simu) katika huduma ya wagonjwa walio na tuvimbe huu katika hatua ya juu inaweza kuwa ya ufanisi pamoja na mikutano ya ana kwa ana na wataalamu wa afya.
"Utafiti huu ulilinganisha kikundi ambacho kilikuwa na ufikiwaji wa mpango wa umatunzo ya kibinafsi na kikundi kingine ambacho kilipata huduma sawa kupitia zana za huduma za simu ," anaelezea.Lengo la wanasayansi lilikuwa kupima ikiwa athari za mashauriano ya mbali zitakuwa mbaya zaidi, sawa au bora.
"Matokeo yanaonyesha kuwa ushauri wa kimatibabu wa njia ya simu sio mbaya zaidi kuliko matibabu ya kibinafsi na, kwa hali fulani, hata ni bora zaidi," daktari anaelezea.
Kulingana na Laloni, mpango huu wa matibabu na ushauri wa tiba wa mbali unaweza kukubalika hasa kwa wale ambao wana shida kupata kliniki au hospitali.
Saratani ya Umio: Utaratibu wa matibabu huleta tofauti
Matibabu ya tiba ya saratani ya umio, moja ya aina ya kawaida ya saratani ya mfumo unaounganisha mdomo na tumbo, ni mada iliyoleta mgawanyiko sana.
Kwa upande mmoja, kikundi cha madaktari kilitetea kinachojulikana kama neoadjuvant treatment regimen. Kwa kifupi, pendekezo linashauri kufanyika kwa tiba ya mionzi- chemotherapy na radiotherapy kabla ya kumfanyia mgonjwa upasuaji ili kuondoa uvimbe wa saratani.
Kwa upande mwingine, wataalam wengine wamependelea matibabu ya perioperative, yaani, mgonjwa afanyiwe chemotherapy kabla na baada ya operesheni.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Takwimu tulizokuwa nazo hadi wakati huo hazikuturuhusu kufafanua ni ipi kati ya mikakati hiyo miwili ulikuwa bora, kwa hivyo uchaguzi wa mmoja au mwingine ulitegemea uamuzi wa kila taasisi," anaeleza Dk Paulo Hoff, rais wa kituo cha Oncologia D'Or.
Ili kumaliza shaka hii, watafiti kutoka vituo kadhaa vya Ujerumani waliamua kulinganisha njia hizo. Matokeo yaliyopatikana yalionyesha faida kubwa kwa matibabu ya perioperative.
Wagonjwa waliofuata regimen hii walikuwa na maisha ya wastani ya miezi 66. Kikundi kilichopokea tiba ya neoadjuvant kilikuwa na maisha ya miezi 37, tofauti ya karibu miaka 2.5 kati ya vikundi.
Matokeo yake, njia ya perioperative inakuwa chaguo kuu kwa madaktari katika visa vya uvimbe wa adenocarcinoma ya juu ya esophageal (wakati ugonjwa tayari umeendelea, lakini bado haujaenea kwa sehemu zingine za mwili).
3. Saratani ya Melanoma (saratani ya ngozi): Dawa kabla ya upasuaji zina faida
Mjadala kuhusu mlolongo wa matibabu pia umekuwa mada ya majadiliano juu ya saratani ya melanoma, aina ya kawaida ya saratani ya ngozi yenye kiwango cha juu cha vifo.
Watafiti kutoka taasisi kadhaa za Uholanzi walijaribu aina tofauti za matibabu kwa kiwango cha 3 melanoma, wakati ugonjwa huo umeendelea lakini haujaenea kwa sehemu zingine za mwili na upasuaji unawezekana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika matukio haya, utaratibu unajumuisha kuondoa uvimbe, katika mfumo wa ulio katika eneo la mkono, shingo ambao unaweza kuwa na seli za saratani ambazo "zimetoroka" kutoka kwa uvimbe wa awali.
Swali kubwa la utafiti lilikuwa: Je, ni bora kuanza matibabu ya dawa kabla au baada ya upasuaji? Ili kujibu swali hili, wanasayansi waligawanya watu 423 na ugonjwa huo katika makundi mawili.
Kundi la kwanza lilipata mizunguko miwili ya ipilimumab na nivolumab (magonjwa mawili ya kinga) na kisha wagonjwa walifanyiwa upasuaji.
Wale ambao walikuwa na majibu mazuri baada ya mchakato huu (yaani, walikuwa na chini ya 10% ya seli za uvimbe zinazofaa) hawakuhitaji kupitia hatua zaidi.
Wale walio na zaidi ya 10% walipewa mizunguko mipya ya dawa: kulingana na wasifu wa maumbile ya wagonjwa, walipokea mizunguko 11 ya kila mwezi ya nivolumab (immunotherapy) au dozi 46 za kila wiki za dabrafenib /trametinib (dawa ya tiba inayolenga seli).
Kundi la pili lilipokea matibabu ya kiwango kilichozingatiwa ambapo washiriki walifanyiwa mizunguko 12 ya kila mwezi ya tiba ya nivolumab.
Baada ya miezi 12 ya ufuatiliwaji, wataalam walihesabu kuwa kiwango cha kuishi bila tukio kilikuwa 83.7% katika kundi la 1 na 57.2% katika kundi la 2.

Chanzo cha picha, Getty Images
Matokeo yanadhihirisha ukweli kwamba kupitia tiba ya kuongeza kinga ya mwili (immunotherapy) kabla ya kufanyiwa upasuaji ni wazo nzuri.
"Jumla ya masomo mengine yaliyochapishwa hapo awali na data iliyotolewa hutoa msingi thabiti sana wa kutumia tiba hii mpya kama njia kuu ya matibabu kwa wagonjwa hawa na hatua ya 3 melanoma," anatathmini mtaalamu wa tiba ya saratani Matheus Lobo, kutoka Kituo cha Saratani cha AC Camargo, huko Sao Paulo.
Ukweli mwingine ambao tuliutambua ni kwamba karibu 60% ya washiriki katika kikundi cha kwanza walikuwa na majibu mazuri na walikuwa na chini ya 10% ya uvimbe zinazofaa baada ya mizunguko miwili ya immunotherapy na upasuaji.
Saratani ya Umme: majaribio ya matibabu mapya
Kila mwaka, zaidi ya wanaume 35,000 duniani kote hugunduliwa kuwa na saratani ya uume.
"Ni ugonjwa ambao kwa kawaida hugunduliwa katika hatua ya kuchelewa sana, kwa sababu ya habari potofu na unyanyapaa," anasema mtaalamu wa tiba ya saratani Fernando Maluf, mwanzilishi wa Taasisi ya Beating Cancer Institute.
Ukosefu wa usafi ni moja ya sababu kuu za maendeleo ya uvimbe huu. Kutopokea chanjo dhidi ya virusi vya Human Papillomavirus (HPV) ni sababu nyingine, kwani kundi hili la virusi husababisha aina hii na nyingine za saratani.
Daktari anasema kuwa katika hali nyingi, matibabu ni pamoja na kunyamazisha hatua za upasuaji na chemotherapy, aambayo haiongezei maisha ya mtu binafsi. Ugonjwa huu kwa kawaida hujitokeza tena baada ya muda.
"Matibabu yanayopatikana ya saratani ya uume yametumika kwa muda mrefu na hatujapata mafanikio hivi karibuni ambayo yamebadilisha itifaki hizi," anaongeza Maluf, ambaye pia anafanya kazi katika Hospitali ya Beneficência Portuguesa na Hospitali ya Albert Einstein ya Israeli, huko São Paulo.
Ili kubadilisha hali hii, daktari wa tiba ya saratani wa Brazil aliongoza kuwa utafiti na Kikundi cha matabibu wa saratani wa Amerika ya Kusini (Lacog).
Lengo lilikuwa kujaribu mchanganyiko mpya wa matibabu unaojumuisha matumizi ya chemotherapy na immunotherapy.
Watafiti waliwashirikisha wanaume 33 wenye uvimbe wa saratani hiyo, ambao walifuatiliwa kwa vipimo vya picha kila mwezi na nusu.
"Kiwango cha majibu tuliyopata na uundaji mpya kilikuwa mara mbili ya yaliyopatikana katika mfumo uliopita," Maluf anahitimisha
Takwimu zilizowasilishwa katika ASCO 2024 zilifichua kuwa 75% ya wagonjwa walikuwa na kiwango fulani cha kupungua kwa uvimbe wa saratani , na 39.4% ya wagonjwa uvimbe wao ulipungua jambo ambalo lilikuwa ni mafanikio.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












