Je, unaweza kubadilisha jinsi ubongo wako unavyozeeka?

dxc

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, Lara Lewington
    • Nafasi, BBC

Inajulikana kwa muda mrefu kuwa mitindo yetu ya maisha, yanaweza kutusaidia kuwa na afya bora kwa muda mrefu. Lakini sasa wanasayansi wanauliza ikiwa teknolojia mpya inaweza pia kusaidia kupunguza kasi ya kuzeeka kwa ubongo wetu.

Asubuhi moja yenye jua kali, Marijke mzaliwa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 76 na mumewe Tom walinikaribisha kwa kifungua kinywa nyumbani kwao Loma Linda.

Uji wa shayiri, mbegu za chia, matunda, lakini hakukuwa na chakula cha sukari kilichochakatwa kutoka kiwandani au kahawa. Kilikuwa ni kifungua kinywa safi kabisa.

Mji wa Loma Linda unatambuliwa kama Blue Zones, mahali ambapo watu wana maisha marefu kuliko wastani. Ni mji wa jumuiya ya Kanisa la Waadventista Wasabato.

Kwa ujumla hawanywi vileo au kafeini, hula lishe ya mboga mboga au vyakula visivyo na nyama. Wanaamini kutunza afya ya miili yao ni sehemu ya dini yao.

Dk Gary Fraser kutoka Chuo Kikuu cha Loma Linda aliniambia watu wa jumuiya ya Waadventista Wasabato, sio tu wanaweza kuishi maisha marefu zaidi, pia maisha yenye afya.

Hakuna siri katika mji wa Loma Linda. Wakazi wake wanaishi maisha ya afya. Kuna mihadhara ya mara kwa mara juu ya kuishi maisha yenye afya, mikusanyiko ya muziki na madarasa ya mazoezi.

Sayansi inasemaje?

sdx
Maelezo ya picha, Marijke na Tom wanaishi Loma Linda - wako kwenye picha pamoja na Lara Lewington

Lara Lewington amesafiri kwenda California, Marekani kukutana na wanasayansi na wataalamu wanaotafiti ubongo na kuchunguza ikiwa tunaweza kubadilisha namna ubongo wetu unavyozeeka.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Nilionyeshwa mifumo ya kompyuta ya kutathmini jinsi bongo zetu zinavyozeeka na kutabiri namna ubongo unavyozeeka, na Andrei Irimia, profesa wa sayansi ya uzeekaji wa binadamu na uchambuzi wa biolojia kupitia komputa katika Chuo Kikuu cha Southern California.

Aliunda mifumo hiyo kwa kutumia vipimo vya MRI, data kutoka katika bongo 15,000 na kwa kutumia akili mnemba, ili kuelewa ubongo, zeekaji wenye afya na ubongo wenye magonjwa, kama vile afya ya akili.

"Ni njia ya kisasa ya kuangalia mifumo ambayo hatuijui kama wanadamu, lakini kompyuta ya akili mnemba inaweza kuchunguza," anasema.

Prof Irimia, alichunguza ubongo wangu, baada ya kuchanganua matokeo, aliniambia nina ubongo wenye umri wa miezi minane zaidi kuliko umri wangu wa kawaida.

Ingawa alinambia kwamba sehemu inayodhibiti uzungumzaji haikuwa imezeeka sana. Na alisema matokeo hayo ni ya ndani ya miaka miwili iliyopita.

Makampuni ya binafsi yanaanza kufanya biashara ya teknolojia hii pia. Kampuni moja huko Brainkey, inatoa huduma hiyo katika kliniki mbalimbali duniani kote. Mwanzilishi wake Owen Philips aliniambia, katika siku zijazo, kupata huduma hiyo itakuwa rahisi.

"Teknolojia itatufikisha mahali ambapo tutaweza kuona mambo mapema zaidi kuliko tulivyoweza hapo awali. Na hiyo ina maana tunaweza kuelewa hasa kile kinachotokea katika ubongo."

Kinyume na kile ambacho Prof Irimia aliniambia kuhusu ubongo wangu, uchunguzi wa kampuni hiyo ulionyesha ubongo wangu umezeeka kwa mwaka mmoja zaidi kuliko umri wangu. Na kuambiwa uzeekaji wake unaendana na umri wangu.

Kutunza afya ya ubongo

X
Maelezo ya picha, Lara Lewington

Ongezeko kubwa la umri wa kuishi katika kipindi cha miaka 200 iliyopita kumesababisha magonjwa mengi yanayohusiana na umri.

Na yote haya yanaturudisha kwenye hatua ile ile. Kila mwanasayansi na daktari, pamoja na wale Blue Zoners, wanasema mtindo wa maisha ni muhimu katika kupambana na magonjwa ya uzee.

Lishe bora, mazoezi, na furaha ni mambo muhimu katika kupambana na kuzeeka kwa ubongo.

Kuna jambo lingine muhimu pia, kulingana na Matthew Walker, profesa wa sayansi ya neva na saikolojia katika Chuo Kikuu cha California, na mwandishi wa kitabu cha Why We Sleep, anasema:

"Kulala ndicho kitu pekee chenye ufanisi zaidi unachoweza kukifanya kila siku ili kurejesha afya ya ubongo na mwili wako.”

Alizungumzia juu ya mfumo wa kusafisha ubongo wetu, ambao hufanya kazi wakati tunapolala kwa kusafisha protini ya beta-amyloid na protini ya tau - hizi ni protini mbaya kwa afya ya ubongo.

"Mabadiliko katika mifumo ya usingizi pia huhusishwa na shida ya kupoteza kumbukumbu," anaeleza Prof Walker.

Msongo wa mawazo usiotibiwa pia huongeza hatari ya matatizo ya akili. Profesa Leanne Williams wa Chuo Kikuu cha Stanford amevumbua mbinu ya kutambua aina fulani za msongo wa mawazo kwenye ubongo kwa kutumia skana ya MRI.

Hilo linaweza kusaidia wanasayansi kuelewa zaidi sababu za matatizo ya afya ya akili kama vile msongo wa mawazo, na pia kutathmini jinsi ya kuyaendea matibabu kwa mgonjwa.

Mildred mwenye umri wa miaka 103, niliyemtembelea huko Loma Linda anasema, “unapaswa kuwa mwangalifu sana na lishe yako."

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah