Sidiria inayogundua saratani ya matiti mapema
Na Aylin Yazan
BBC Turkey

Chanzo cha picha, MIT
Hebu fikiria kuweka kifaa cha ultrasound kinachoweza kuvaliwa juu ya sidiria ambacho kinaweza kinaweza kung’amua (kuskani) uvimbe ndani ya matiti yako huku ukiendelea kunywa kikombe chako cha kahawa au chai.
Wakati ukitafakari hayo mwanasayansi wa Kituruki Dr Canan Dagdeviren, na timu yake katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT) Media Lab, wametengeneza teknolojia hiyo, kwa heshima ya shangazi yake ambaye alifariki kutokana na marathi ya saratani ya matiti.
Kifaa hicho kitarwezesha ufuatiliaji wa mara kwa mara wa wagonjwa walioko katika hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti kabla ya kufanyiwa vipimo vya uchunguzi wa saratani hiyo vya mara kwa mara vya mammogram.
Saratani ya matiti ni aina ya saratani ya kawaida ambapo wanawake milioni 2.3 waligunduliwa na wanawake 685,000 walipoteza maisha yao katika mwaka 2020, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Saratani hii ni sababu ya pili ya vifo vya wanawake duniani.

Chanzo cha picha, MIT
Dr Dagdeviren ni profesa mshiriki katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT)
Wakati saratani ya matiti inapogunduliwa mapema, na ikiwa bado ndani ya eneo moja, inaongeza uwezekano wa kuishi . Iligundulika kuwa katika miaka mitano kiwango cha kupona kilikuwa ni 99%, inasema taasisi ya American Cancer Society.
Dkt Dagdeviren anasema kifaa hicho kinaweza kusaidia kuongeza viwango vya kuishi kwani kiwango cha kuishi ni asilimia 22 tu kwa wanawake ambao wanagunduliwa katika hatua za baadaye.
Jinsi kinavyofanya kazi?
Mwanasayansi wa vifaa vya MIT na mhandisi Canan Dagdeviren alikuja na wazo hilo wakati amekaa kando ya kitanda cha shangazi yake hospitalini.
Shangazi yake aligunduliwa kuwa na aina ya saratani ya matiti, licha ya kufanyiwa vipimo vya matiti mara kwa mara, na alifariki miezi sita baadaye.
Ni kifaa rahisi na ambacho kinachoweza kutumika tena ana kinaweza kushikamana na sidiria, bila hitaji la mwendeshaji.

Chanzo cha picha, MIT
Kuna nafasi sita kwenye kifaa cha umbo la asali na kamera ndogo ya ultrasound inaweza kuhamishwa kati matiti ili uone ndani ya matiti yako kutoka pande zote kinafanya kazi bila kuhitaji geli ya ultrasound.
Dr Dagdeviren anasema inaweza kugundua uvimbe mdogo wa kama ndogo kama sentimita 0.3 , ukubwa wa uvimbe mapema.
Hii "Ina maana kuwa ni kifaa hiki ni sahihi sana katika kubaini hitilafu yoyote ," anasema.
Mammogram ni nini?
Njia ya kawaida ya utambuzi wa saratani ya matiti ni ya kutumia kifaa cha mammogram ambapo matiti yako huchunguzwa kwa kipimo cha mionzi -ni X-ray, ambapo mionzi hupitishwa kupitia mwili ili kupata picha ya matiti.

Kwa nini baadhi ya wanawake huhisi maumivu?
"Matiti ya kila mtu ni ya kipekee kwa kila mwanamke, na tofauti ya kiasi cha tishu za tezi na tishu za mafuta pia ni za kipekee," anasema Helen Yule, mshauri wa tiba ya mionzi ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la ushauri wa wenye taaluma hiyo nchini Uingereza.
Wanawake ambao wana tishu zaidi za tezi wanaweza kupata wasiwasi zaidi wakati wa mammogram kuliko wale ambao wana matiti ya mafuta kabisa. Pia kutumia tiba ya uingizwaji wa homoni (HRT) kunaweza kusababisha maumivu ya matiti kwa muda.
Mshauri wa uchunguzi kimatibabu wa mionzi anasema matarajio ya mwanamke ya jinsi mammogram itakavyokuwa pia huchangia.
Kuna njia rahisi za kuzuia maumivu wakati wa mammogram kama vile kujaribu kuepuka kuwa na mammogram wiki kabla au wakati wa kipindi chako cha hedhi au kumeza tembe ya paracetamol kabla kufanyiwa uchunguzi huo.
Ni nani anayeweza kuvaa kifaa hiki juu ya sindiria ni cha nani?
Uchunguzi unaonyesha kuwa uvimbe wa matiti wa saratani ambao hukua katikati ya kipindi ambacho mwanamke anasubiri kufanyiwa vipimo vya mammogram, huchangia 20-30% ya visa vyote vya saratani ya matiti na saratani hii kusambaa kwa kasi.
Timu ya MIT inasema uvimbe huu – hukua kwa haraka zaidi kuliko ule wa saratani zinazopatikana wakati wa uchunguzi wa kawaida.
Kifaa hiki kinaweza kutolewa kwa wanawake ambao wako katika hatari kubwa ya saratani ya matiti na kuwasaidia kugundua uvimbe kabla ya kufanyiwa vipimo vya mammogram au kufanyiwa uchunguzi wa kibinafsi.
Lakini watafiti wanaonya kuwa "ikiwa hali yoyote isiyo ya kawaida itagunduliwa, mammogram bado itakuwa muhimu".

Kifaa hiki kinachovaliwa juu ya sidiria kilitengenezwa wapi?
Iliichukua timu ya MIT inayofanya kazi ya kutengeneza vifaa vya afya vinavyoweza kuvaliwa miaka sita na nusu kutengeneza kifaa hicho. Ilipata hati miliki ya Marekani mwezi Agosti na majaribio zaidi ya binadamu yanaendelea.
Kifaa kimoja kinagharimu takriban dola 1,000 lakini wavumbuzi wanasema garama hii itashuka kwani wanatengeneza kwa kiasi kikubwa kifaa hicho. Muda wa kufanya hivyo ni kati ya miaka minne hadi mitano.
Skana moja itakuwa na gharama ya "chini ya kikombe cha kahawa ikiwa utachanganua tishu zako kila siku", inakadiria timu ya utafiti.

Chanzo cha picha, Dkt Dağdeviren
Matumaini kwa wanawake
Uchunguzi unaonyesha kuwa ugunduzi , na huduma duni za afya, ndio sababu kuu za viwango vya juu vya vifo vya saratani ya matiti katika nchi zinazoendelea.
Kwa mujibu wa takwimu za WHO, viwango vya kuishi kwa miaka mitano katika nchi zenye kipato cha juu vinazidi asilimia 90, ikilinganishwa na asilimia 66 nchini India na asilimia 40 Kusini mwa Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, Dr Canan Dagdeviren
Kifaa hicho kina uwezo wa kutumika kwa ajili ya kuchanganua sehemu nyingine za mwili, kwani Dkt Dagdeviren alikitumia kumchunguza mtoto wake alipokuwa mjamzito mwaka jana.
"Shangazi yangu alikuwa mdogo sana, alikuwa na umri wa miaka 49 tu. Kufa kwake lilikuwa jambo la ajabu zaidi akilini mwake. Vipi kama shangazi yangu angevaa bra kama hiyo?" anauliza.
Taarifa ya ziada ya Issari ya Praithongyaem













