Mambo 6 ambayo huongeza hatari ya kupata saratani ya matiti

Chanzo cha picha, Getty Images
Saratani ya matiti ndiyo aina inayojulikana zaidi ya saratani, ikiwa na visa zaidi ya milioni 2.2 duniani, kulingana na data ya 2020 kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).
Inakadiriwa kuwa mwanamke mmoja kati ya 12 atapatwa na saratani ya matiti katika maisha yake na ndiyo chanzo kikuu cha vifo miongoni mwao. Mnamo 2020, karibu wanawake 685,000 walikufa kutokana na ugonjwa huu duniani huku karibu robo ya visa vipya vya saratani ya matiti mnamo 2020 vikitokea Marekani.
Katika eneo la Amerika Kusini na Caribbean, idadi ya wanawake walioathiriwa na ugonjwa huo kabla ya kutimizi umri wa miaka 50 (32%) ni kubwa zaidi kuliko Amerika Kaskazini (19%), linasema Shirika la Afya la Pan American.
Kuna sababu kadhaa zinazosababisha saratani ya matiti ambazo haziwezi kurekebishwa, kama vile kuzeeka, mabadiliko ya kimaumbile, na historia ya familia ya saratani ya matiti miongoni mwa masuala mengine.
Lakini kuna mambo mengine ambayo huongeza hatari ya kupata ugonjwa huo na ambayo inaweza kuzuiwa au kupunguzwa kwa kufanya mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kila siku.
Katika siku hii ya Septemba 19, iliyotengwa Kupambana na Saratani ya Matiti Duniani, tunaangazia ni mambo gani yanayoongeza hatari ya saratani ya matiti? Na nini kifanyike ili kuzipunguza hatari ya kupata maradhi hayo.

Chanzo cha picha, Getty Images
1. Kutojishughulisha na mazoezi
Wanawake amabao hajishughulishi na mazoezi ya viungo wako katika hatari ya ya upata saratani ya matiti, kinasema kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa(CDC). Kwa hivyo ni muhimu kufanya mazoezi mara kwa mara ya kunyoosha viungo.

Chanzo cha picha, Getty Images
2. Uzito kupita kiasi
Wanawake wazee walio na uzani mkubwa au wanene wapo katia hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti kuliko wale walio na uzani mzuri kiafya. Jumuiya ya Saratani ya Marekani inapendekeza kudumisha uzani wenye afya maishani mwako na kuepuka kupata uzito kupita kiasi kwa kusawazisha ulaji wa chakula na kujihughulisha na na mambo yatakayosaidia kunyoosha viungo.

Chanzo cha picha, Getty Images
3. Homoni
Baadhi ya aina za tiba ya uingizwaji wa homoni (zile zinazojumuisha estrojeni na progesterone) zinazochukuliwa wakati wa ukoma hedhi zinaweza kuongeza hatari ya saratani ya matiti ikiwa zitachukuliwa kwa zaidi ya miaka 5, CDC inabainisha.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ili kuepuka hili, ni wazo zuri kuzungumza na daktari wako kuhusu chaguzi zisizo za homoni za kutibu dalili za kukoma hedhi, lasema Shirika la Saratani la Marekani.
4. Historia ya uzazi
Kuwa mjamzito kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30, kutonyonyesha, na kutobeba ujauzito hadi mwisho kunaweza kuongeza hatari ya saratani ya matiti.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanawake wanaoamua kunyonyesha watoto wao kwa angalau miezi kadhaa wanaweza kupata manufaa zaidi kwa kupunguza hatari yao ya kupata saratani ya matiti, lasema Shirika la Saratani la Marekani.
5. Pombe
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa hatari ya mwanamke kupata saratani ya matiti huongezeka kadiri anavyokunywa pombe zaidi, inasema CDC.
Hata matumizi katika viwango vya chini yamehusishwa na kuongeza hatari.
Ni vyema kujiepusha na unywaji pombe.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini wale wanaoamua kunywa pombe wanashauriwa kutokunywa zaidi ya chupa moja kwa siku.
Kwa hivyo unafaa kunywa kiasi gani cha pombe kwa siku?
Mili lita 355ya bia, Mili lita 150 ya divai, au Mili Lita 50 ya pombe kali au "vinywaji vikali" vyenye uthibitisho wa 80.
6. Kuvuta sigara

Chanzo cha picha, Getty Images
Ukweli ni kwamba matumizi ya tumbaku yanaweza kusababisha saratani ya sehemu yoyote ya mwili.
Kuepuka kuvuta sigara kunasaidia kupunguza hatari ya kupata saratani.















