Ukraine na Magharibi zina mawazo tofauti kuhusu kuishinda Urusi - Zelenskyi

Rais wa Ukraine amezungumzia kuhusu muundo wa mazungumzo ya Ukraine na Rais wa Urusi Putin, alitabiri wakati vita vitakapoisha, na kuelezea tofauti kati ya maono ya ushindi wa Ukraine katika Magharibi na Ukraine miongoni mwa mambo mengine.

Bwana Zelenskyi, alikuwa akizungumza na Trudy Rubin, mwandishi wa makala kwa toleo la Marekani la Philadelphia Inquire.

kuhusu mashambulizi dhidi ya Urusi na silaha za Magharibi.

Unaweza pia kusoma:

Zelenskyi amesema kuwa uamuzi wa Rais wa Marekani Joe Biden kuipa Ukraine fursa ya kushambulia mkusanyiko wa vifaa vya Urusi katika mpaka wa Urusi na Ukraine ni mzuri, lakini "hautatui tatizo la uharibifu wa miji na vijiji vyetu unaofanywa na mabomu ya angani yanayofahamika kama Corrective Aerial Bombs (CABs)."

Hii "Inatatua masuala ya kimkakati, sio silaha ya kimkakati. Hatuwezi kutumia silaha za mbinu kupambana na matatizo ya kimkakati, kama vile makombora ya kukabiliana na ndege na anga zao," Zelenskyi alisema.

Ili kukabiliana na makombora ya Urusi ya kupambana na ndege za kivita, Jeshi la Ukraine halihitaji mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot kama makombora ya masafa marefu ya ATACMS, rais alisema.

"Patriot haiwezi kupigana dhidi ya KABs," Zelenskyy alielezea, akisisitiza kuwa Ukraine haina makombora ya kutosha ya kukabiliana na Patriot. "Utashinda katika katika masafa mafupi lakini baada ya muda mrefu, Warusi watakupiga. Utatoa makombora yako yote, na kisha watapiga miji, nishati - na utapoteza[maeneo]."

Zelensky amesema Urusi ilitumia zaidi ya mabomu 800 ya angani dhidi ya Ukraine wiki iliyopita.

makombora ya masafa marefu ya Marekani kushambulia viwanja vya ndege ndani ya nyuma ya Urusi.

"Tunahitaji kutafuta suluhisho la masafa marefu dhidi ya viwanja vya ndege ambapo ndege za kijeshi zimewekwa, ambazo Urusi hutumia kutumia makombora ya kupambana na ndege ya ATACMS, ambayo inaweza kushambulia kwa umbali wa kilomita 300, labda itatusaidia kwa sasa. Nataka kusisitiza - leo... Lakini tayari kuna viwanja vya ndege, ambavyo viko umbali mkubwa, ambavyo hutumia makombora makubwa.

Hiyo ni, leo tunahitaji kupewa fursa ya kutumia ATACMS ndani ya Shirikisho la Urusi," Zelenskyi alisema.

Kulingana naye, mikoa ya Donetsk na Kharkiv inateseka zaidi kwa mashambulio yanatoka kwa mashirika ya usalama ya Urusi. Wanaweza kupigana na ulinzi wa anga. Lakini gharama ya makombora kwa mifumo ya Patriot ni ya juu sana, na haizalishwi kwa kiasi kikubwa.

Je, mazungumzo na Shirikisho la Urusi yanawezekana?

Volodymyr Zelensky alipendekeza uwezekano wa mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Urusi Putin.

Hapo awali, alizungumzia mara kwa mara juu ya kutowezekana kwa mazungumzo kama hayo, ambayo hata yamewekwa katika sheria nchini Ukraine.

Kulingana na Zelensky, chaguo pekee la mazungumzo na kiongozi wa Urusi ni kwa njia ya wapatanishi, kama ilivyokuwa wakati wa majadiliano na uundaji wa ukanda wa nafaka wa Bahari Nyeusi.

"Mfano kama huo ulitumika kwa mara ya kwanza kwa mfano wa ukanda wa nafaka, wakati Ukraine ilizungumza sio na Urusi, lakini na Umoja wa Mataifa na Uturuki.

Wao, walichukua jukumu la kufanya mazungumzo na sisi, na kisha kusaini makubaliano kulingana na shirikisho la Urusi. Hivi ndivyo ilivyofanyika: makubaliano mawili kati ya Umoja wa Mataifa na Uturuki," Zelenskyy alielezea.

Kulingana na Zelenskyi, mpango kama huo unaweza kutumika wakati wa mazungumzo juu ya masuala ya "uaminifu wa kimataifa, na nishati". Nchi kutoka mabara tofauti zinaweza kuwa kama wapatanishi, rais anaamini.

"Washirika wetu sio tu Ulaya na Marekani, lakini pia kutoka mabara mengi, ikiwa ni pamoja na Asia, Pasifiki, pamoja na Waafrika, Amerika ya Kusini. Wakati kuna wawakilishi ambao wanaandaa suluhisho la mgogoro huu na ule, na kisha hati hii, ikiwa inairidhisha Ukraine, inapaswa kushughulikia wawakilishi wa Shirikisho la Urusi. Kwa sasa, tuna mfano wa aina hiyo," Zelensky alisema.

Kuna tofauti gani kati ya mawazo ya ushindi wa Ukraine kati ya Magharibi na Ukraine?

Mwandishi wa habari wa Philadelphia Inquirer Trudy Rubin alimuuliza Zelensky ikiwa, kwa maoni yake, Rais wa Marekani Joe Biden anaamini kweli katika ushindi wa Ukraine.

Kiongozi huyo wa Ukraine alijibu kuwa ana uhakika na hilo, lakini akaongeza kuwa ushindi unaeleweka tofauti nchini Ukraine na Magharibi.

"Kwa nchi za Magharibi, ushindi mkubwa ni kuizuia Ukraine kukaliwa, kumweka Putin katika nafasi yake," Zelensky alieleza.

Aliongeza kuwa anasikia ujumbe kwamba kila mtu anaohofia kwamba Urusi itaanguka. "Kila mtu ana hofu ya kile kitakachotokea kwa Urusi bila Putin. Kila mtu anaogopa kama inaweza kubaki kama ilivyo, na sio mbaya zaidi," rais alielezea na kusisitiza kwamba haungi mkono hofu kama hiyo ya Magharibi.

"Tunashukuru kwamba hawakuturuhusu kukaliwa, lakini kuridhika kunahitajika, haki inahitajika na hakika ni moja ya sehemu muhimu. Tutawaangaliaje watu hawa wote ... (Kwa macho ) ni ambao waliwapoteza wapendwa wao, ikiwa hatutajiridhisha na haki?" Zelenskyi alisema.

Pia alielezea jinsi anavyoelewa ushindi wa kweli wa Ukraine.

"Sehemu ya kwanza ni kuzuia uharibifu kamili wa Ukraine na kila kitu katika Ukraine ... Hadi vita vitakapomalizika, hatuwezi kusema kwamba tumetetea uhuru wetu. Ni muhimu kufikia usalama kwa vizazi vijavyo,ikimaanisha kuwa kuna uwezekano wa kurudiwa kwa uchokozi."

Zelensky alisisitiza kuwa itakuwa "hatari kubwa" kwamba Urusi itarudia uchokozi kama Ukraine haitakuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya na NATO.

"Tunapaswa kuwa katika Umoja wa Ulaya - hii ni usalama wa kiuchumi. Tunapaswa kuwa katika NATO. Na ikiwa hatuna hilo, nadhani hizi ni hatari kubwa kwetu... Adui huyu atarudi. Jinsi ya kurudi? Katika uso wa Putin – kama sio Putin, atakuwa mwingine kutoka Kremlin, katika miaka ishirini, miaka arobaini, hamsini - sijui. Tunahitaji ulinzi wa pamoja wa Ukraine," Zelenskyi alisema.

Je Vita hivyo vitadumu kwa muda gani?

Alipoulizwa na Trudy Rubin vita vitadumu kwa muda gani, Zelensky alisema kuwa vita vitaisha hata hivyo. Ukraine tayari imechukua hatua ya kwanza na mkutano wa amani.

Aliahidi kuwa Kyiv itaandaa waraka juu ya mpango wa amani.

"Tutajaribu kufanya kila kitu ili waraka huu ufike kwenye meza ya wawakilishi wa Urusi na kwamba nchi mbalimbali zenye nguvu zinajaribu kumaliza vita hivi kwa haki, hakika katika muundo na mazungumzo mbalimbali," Zelenskyy alisema.

Aliongeza kuwa vita hivyo havitaisha kabisa kwa kila mtu - havitatokea haraka sana.

"Lakini waraka unaweza kutayarishwa ambapo baadhi ya masuala yanatatuliwa si kwa risasi, lakini katika muundo mmoja au mwingine wa mazungumzo," Zelenskyy aliongeza.

Pia kwa maoni yake hakusema ni kwa muda gani vita hivi vitadumu. Lakini alinihakikishia kwamba anajua nini cha kufanya mwaka huu.

"Lazima tutengeneze hati, lazima tufanye kila kitu ili kuandaa mkutano wa pili mwaka huu. Tunapaswa kuvumilia. Na lazima tumdhoofishe adui kadiri inavyowezekana," alisema kiongozi huyo wa Ukraine.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi