Je ngono ya kupanga inaweza kuwa bora zaidi kuliko isiyo ya kupangwa?

Planned Sex

Chanzo cha picha, Getty Images

Vipindi vya ngono kwenye TV na filamu za ngono mara nyingi huwa na matukio ya kusisimua na yasiyotarajiwa ambayo yanaonekana kutojali jambo au kutopangwaa.

Picha hizi kwenye vyombo vya habari hutuma ujumbe kwamba sifa moja ya ngono yenye shauku, yakusisimua na ya kuridhisha ni ile yenye uhiari.

Tulipowauliza wanandoa nchini Marekani na Canada kuhusu wanachopendekeza kwenye tendo la ndoa ama ngono, wengi waliamini kwamba ngono inakuwa ni ya kuridhisha zaidi inapotokea yenyewe tu kuliko ile inayopangwa mapema.

Lakini je, ngono isiyo ya kawaida inaridhisha zaidi?

Ingawa hamu ya kushiriki tendo la ndoa ama ngono inaweza kuwa ya kiwango cha juu unapokuwa katika uhusiano mpya, na kujamiiana kunaweza kuonekana kutokea mara kwa mara bila kupanga, na hamu ya ngono (na kufanya mara kwa mara ya ngono) mara nyingi hupungua kwa kadri muda unavyozidi kusongwa katika uhusiano.

Wanandoa wa muda mrefu ambao husubiri mpaka wote wawili wapate hamu ya kushiriki tendo hilo, mara nyingi huishia kufanya tendo hilo mara chache chache sana.

Planned Sex

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kama hakuna kupanga, mara nyingi ngono haifanyiki

Kupanga kushiriki ngono kunaweza kuwa jambo muhimu ili ngono ifanyike ili mahitaji mengine ya wakati yatimizwe, hata kama kupanga ratiba ya ngono kunachukuliwa kuwa sio kitu kinachovutia na kuhamasisha kwenye tendo.

Kujua wakati wa kufanya ngono kunaweza pia kusaidia watu kujiandaa kwa mavazi, mafuta, manukano na kwa faragha, na hiyo inaweza kufanya ngono kuwa bora zaidi.

Uchunguzi

Planned Sex

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hata wakati wa malezi na ratiba nyingine za kazi, wenza wanapaswa kutenga wakati wa faragha

Licha ya ukweli kwamba ubora wa ngono isiyopangwa unagusa utamaduni wa Marekani na vyombo vya habari, lakini utafiti mdogo umechunguza jinsi ngono ya kupangwa inavyoweza kulinganishwa kwa ubora na ile isiyopangwa.

Timu yetu ya utafiti katika Maabara ya Afya ya Ngono na Mahusiano ya Chuo Kikuu cha York nchini Canada ilihoji watu 303 na wanandoa 102 kutoka Marekani na Canada.

Tuliwauliza washiriki wetu ni kwa kiasi gani walikubaliana na kauli kama vile: "Ngono na mpenzi wangu inaridhisha zaidi inapotokea tu bila kuipanga" na "Napendelea kujua mapema wakati gani nitafanya ngono (ngono ya kupanga)."

Kisha tuliwauliza ikiwa uzoefu wao wa hivi karibuni zaidi wa ngono ulikuwa umepangwa au la. Pia tuliwauliza kama walikuwa wameridhika kingono katika uhusiano wao kwa ujumla na kama walikuwa wameridhika ngono waliyofanya hivi majuzi.

Pia tunarekodi maisha yao ya kingono ya kila siku katika kipindi cha wiki tatu.

Ngono ya isiyopangwa na kuridhika

Katika tafiti zote mbili, watu walionyesha kuwa waliiamini kuwa ngono isiyo pangwa ni bora. Lakini tofauti na imani hizi, ngono isiyopangwa haikuwa yenye kuridhisha hasa kama ile ya kupanga.

Planned Sex

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muhimu kufahamu wakati wa mwanzo wa mahusiano kuna kujiandaa na kujipanga zaidi
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Katika utafiti wa kwanza, ingawa watu ambao walikuwa wakiamini ripoti kwamba ngono isiyopangwa ni ya kuridhisha zaidi, uzoefu wao wa hivi karibuni zaidi wa kingono unaonyesha kuwa ngono isiyopangwa, haikuwaridhisha zaidi kuliko ile iliyopangwa.

Wakati mwingine ngono iliyopangwa inaweza kuonekani siyoridhisha, lakini hii ilikuwa tu kwa wale ambao waliamini kupanga ngono sio kitu sawa na bora.

Katika utafiti wa pili, ambapo tulifuatilia uzoefu wa ngono wa wanandoa kwa siku 21, walionyesha kuwa hakuna tofauti ya kuridhika kingono kati ya ngono ya kupanga na isiyo ya kupanga, hata kwa wale ambao waliamini kwamba ngono isiyopangwa ilikuwa bora.

Pia tulitaka kujua jinsi watu walivyohisi kuwa kujituma na kupanga kulichangia kufurahia kwao kwenye tendo hilo. Jambo la kufurahisha ni kwamba watu walisema kwamba hali hiyo iliwaongezea msisimko wa kingono, shauku na tamaa.

Lakini watu wengi pia walitaja kuwa kupanga ngono kunaweza kusaidia kujenga matarajio na hamu ya ngono.

Na ingawa baadhi ya watu walitaja kwamba kujamiiana kwa kupanga kunaweza kuongeza hamasa, ngono isiyopangwa haikuwa mara zote kichocheo cha tendo: Wengine walibainisha kuwa wakati wa ngono isiyopangwa, hawakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa kwa tendo achilia mbali utulivu wa kiakili au uhakika wa faragha yako.

Planned Sex

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hata kama uko na ratiba ngumu, tafuta muda wa kuwa na faragha