Kombe la Dunia 2022: Mabao matatu halafu kuvunjika moyo - Kylian Mbappe alivyokosa zawadi kubwa zaidi

Chanzo cha picha, Getty Images
Magoli matatu, halafu akavunjika moyo – Ulikuwa usiku wa matumaini makubwa kwa Kylian Mbappe lakini huenda uliishia kuwa njia mbaya zaidi ya kushinda Kiatu cha dahabu cha Kombe la Dunia.
Mshambuliaji wa Ufranasa ataondoka Qatar kama mfungaji bora zaidi wa shindano baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika fainali ya Kombe la dunia tangu alipofunga mabao hayo Geoff Hurst mwaka 1966 -lakini kumbukumbu yake kuu itakuwa ni machungu ya kushindwa.
Baada ya mwisho wa mechi ya kusisimua kusema kweli , Mbappe mwenye umri wa miaka 23 bado aliweza kupanda kwenye jukwaa la ushindi kuchukua tuzo lake binafsi baada ya kuionyesha dunia kipaji chake kikubwa katika soka – lakini kulikuwa na kipindi ambapo ilionekana kuwa alikaribia kupata zawadi kubwa zaidi.
Hii ingekuwa fainali yake, na kufahamika kama shindano lake pia, lakini kwa yoyte haya yote atakumbukwa mchezaji mwingine nambari 10, ambaye pia alinyenyua Kombe la Dunia, ambalo Mbappe alilipeleka nyumbani miaka minne iliyopita.
Alikuwa ni Muargentina na Lionel Messi ambaye alinyakua utukufu huo, lakini Mbappe aliusisimua uwanja wa Lusail na kwa muda wengi walihisi kuwa huu ulikuwa ni muda wake tena.
Azama ya Mbape ya kuwa kijana mdogo zaidi kushinda Kombe la pili la Dunia tangu baada ya Pele, ambaye alikuwa na umri wa miaka 21 wakati alipofanya hivyo mwaka 1962, ilikumbwa na amsukosuko mwanzoni mwa mechi.
Mwanzoni mwa mchezo alionekana kama mtazamaji huku Argentina wakitawala nusu ya kwanza ya kipindi cha mchezo, akifanikiwa kuugusa mpira mara 11 pekee huku timu yake ikihangaika baada ya kufungwa mabao mawili, na mambo hayakuwa maziuri sana waliporejea uwanjani baada ya mapumziko.
Ilichukua hadi dakika ya 71 kwa Mbappe kuweza kupiga mkwaju wake wa kwanza golini, lakini mpira ukapaa juu ya goli, wakati ule ilionekana hakuna njia tena ya Ufaransa kurejea tena.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Yote hayo yalibadilika wakatika Nicolas Otamendi falipomfanyia faulo Randal Kolo Muani alipokua amengia kwenye eneo la hatari, na Mbappe hakufanya kosa akautingisha wavu.
Sekunde 97 tu baadaye, alifunga bao la pili akasawazisha 2-2, na mara hii kwa bao liliingia kwa mtindo uliivutia- mpira uliodondoka katika eneo hatari na bao lake liliiondoa timu yake katika hatari ya kukaribia kushindwa.
"Huwezi kuhoji ubora kwa mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi wa kuirejesha timu yake katika mechi," Alisema mtangazaji mwenza wa BBC Jermaine Jenas wakati mechi ilipoingia kipindi cha ziada.
"Kusema kweli ni nyota mkubwa. Alikua tu anasubiri tu. Timu yake ilikua pale pamoja naye lakini mabadiliko yaliongeza kiasi fulani cha nguvu, baadhi waliiamini ushindi ni wao."
Maajabu zaidi yalifuatia, bao la tatu la usiku – lake la nane katika shindano- lilipatikana wakati alipofunga goli lake la penati katika kipindi kingine cha ziada, kwa mara nyingine tena alionekana kuinusuru timu yake, lakini baadaye mikwaju ilipigwa nje na wachezaji wenzake mbele ya umati wa mashabiki wao ambao hawakuamini kile walichokuwa wakikitazama.
"Tumemuona Rais wa Ufaransa," Jenas aliongeza baada ya Kamera ya matangazo ya mpira kumuonyesha Emmanuel Macron. "Huyo kijana ni mfalme. Mabao matatu katika fainali ya Kombe la Dunia na goli la penati amefanya vyema kwa kiwango ambacho ungependa . Amelifunga eneo sawasawa na alipofunga mara ya mwisho."
Mbappe hakukosa mkwaju wa penati, aliweza kumfunga Emiliano Martinez kutoka kwenye eneo la penati kwa mara ya tatu, lakini sawa na Messi alikuwa ni mlindalango wa Argentina ambaye alipongezwa mwishowe baada ya kuizuia mikwaju ya penati ya Kingsley Coman na Aurelien Tchouameni kuingia wavuni.
Mbappe bado alikuwa shujaa wa Ufaransa pamoja na kushindwa, na alipongezwa na wachezaji wenzake katika kikosi cha Ufransa na pia Rais Macron mwishoni, lakini huu haukuwa mwisho wa ndoto yake, licha ya kwamba hii itakuwa fainali ambayo ni wachache wataisahau.
"Ilikuwa ni furaha kuwa hapa kujionea," Mtanagazaji wa soka BBC Alan Shearealisema. "Asante Mesii na Mbappe. Jinsi Argentina ilivyoendelea kuongeza bidi, walifanya hivyo kiakili. Hongera sana na asante kwa kutuburudisha. Mchezo ulikua mzuri ajabu."
Azma ya Ufaransa ya kutetea Kombe la Dunia iliishia kwa kushindwa kwa mikwaju ya penati, lakini kwa kipindi kikubwa cha mechi, ilionekana ni kana kwamba walikuwa wameamua kuachilia kombe hilo kirahisi.
Meneja wa Les Bleus Didier Deschamps alikuwa amejaribu kubadilisha wachezaji kabla ya kipindi cha kwanza cha mchezo, alipowaondoa Olivier Giroud na Ousmane Dembele na kuwaingiza Kolo Muani na Marcus Thuram, na kumhamishia Mbappe katika nafasi ya mashambulizi zaidi.
"Ulikuw ani mkakati kwasababu niliona walikuwa wanakosa nguvu ," Deschamps alielezea "Siwalaumu Giroud au Dembele,Niliona tu kuwa hawakuwepo 100%.Nilimleta Kylian in kutoka kwenye eneo la wimga – kwasababu tulikuwa katika matatizo makubwa.
"Kimsingi hatukua katika hali bora. Kimwili tulikosa kitu cha ziada, lakini tulihitaji kujipanga upya na kujaribu kubadili kitu fulani.
"Kila mara huwa ninasema, kila kitu kinawezekana, unaweza kubadilisha katika kipindi cha kufumba na kufumbua na tulifanya hilo. Tulirejea kutoka kwa wafu na tukafanya vyema – kwa bahati mbaya haikutosha.
"Lilikuwa ni Kombe la Dunia la rekodi na Kylian ameacha alama yake katika fainali lakini bahati mbaya sio kwa namna ambayo yeye ameipenda."















