Kwa nini wanawake hawa wa India wanalazimishwa kukaa bila kuolewa?

Chanzo cha picha, SEETU TEWARI/BBC
Shama wa Supaul huko Bihar hufadhaika kila anaposikiliza nyimbo za harusi.
Kinachomfanya Shama mwenye umri wa miaka 27 kukata tamaa ni kwamba hajaolewa, lakini uamuzi huu si wake mwenyewe bali ni kulazimishwa kukaa bila kuolewa.
Dadake Shama Sakina Khatoon pia hajaolewa. Umri wake ni miaka 26.
Lakini hadithi hii sio tu ya Shama na Sakina, kwani kuna wasichana kama 15 katika Kata ya 10 ya Kochgama Panchayat ya Supaul block ambao wanalazimika kuishi bila kuolewa.
Wasichana hawa ni wa jamii ya Shershahbadi, ambayo wasichana wanasubiri uwamuzi wa Paigam au kiongozi kabla waolewe.
Hakuna kiongozi aliyekuja kuwaulizia wasichana hawa. Viongozi ni watu wanaopatanisha familia mbili kwa ajili ya ndoa.
Wanawake hawa wanaosumbuliwa na uchungu wa kutoolewa, ni kati ya Shama mwenye umri wa miaka 27 hadi Jameela Khatoon mwenye umri wa miaka 76.
Jamila Khatoon ambaye ni mzaliwa wa Supaul pia alikuwa ameota kwamba msafara wa harusi yake ungekuja na angeolewa, lakini ndoto hiyo haijatimia hadi wa leo. Jamila anaishi na dadake Shamsun mwenye umri wa miaka 57.
Dada wote wawili hawajaolewa na wanajikimu kimaisha na mbuzi wao watano.
Lakini walipoulizwa sababu ya kutofunga ndoa kwa muda mrefu, wote wawili walijibu, "Tufanye nini, na hakuna ujumbe wa ndoa ulioletwa kwa familia) ."
Shamsun anaiambia BBC, "Uchungu unaumiza moyo wangu, nimwambie nani, niseme nini."
Lakini kwa nini wewe na dada yako hamjaolewa? Kujibu swali hili alisema ni kwa sababu yeye ni Muislamu wa jamii ya Shershahbadi.

Chanzo cha picha, SEETU TEWARI/BBC
Waislamu wa Shershahbadi ni nani?
Idadi ya Waislamu wa jamii ya Shershahbadi wa Bihar wanaishi vijijini. Wengi wao wanapatikana wiliya za Supaul, Purnia, Katihar, Kishanganj, Araria eneo la Bihar.
Kulingana na mila yao ili msichana apate kuolewa lazima mpatanishi wa ndoa awasilishe ujumbe na sana sana kutoka upande wa wavulana tu.
Mila hii inazingatiwa sana kwamba ikiwa ujumbe wa ndoa haukuja kwa msichana, yeye hubaki bila kuolewa.
Hii ndiyo sababu popote pale palipo na Shershahbadi huko Bihar, utapata wanawake au wasichana ambao hawajaolewa .
Mume Nurul Hoda, mkuu wa Kochgama Panchayat yenye Waislamu wengi wa Shershahbadi, anasema, "Tulikuwa tumetengeneza orodha ya wanawake hao ambao hawajaolewa miaka michache iliyopita. Wakati huo idadi yao ilikuwa 250, sasa lazima iwe imeongezeka."

Chanzo cha picha, SEETU TEWARI/BBC
Shershahbadis, wanaozungumza Kibengali cha kawaida (mchanganyiko wa Kiurdu na Kibengali), wanajihusisha na Maliki Shershah Suri.
Watu hawa wanadai kwamba wenzao walijiunga na jeshi la Sher Shah kama askari. Sher Shah alikuwa mwanzilishi wa nasaba ya Suri na alianzisha usultani wake kwa kumshinda mfalme Mughal Humayun.
Syedur Rahman Rehman, Rais wa All Bihar Shershahbadi Association, anaiambia BBC, "Watu hawa walikaliwa na Sher Shah. Watu hawa wa nguvu, wachapakazi na wanaishi kando ya mto, nje kidogo ya Bihar, wanaishi kwenye mpaka wa Bengal, Jharkhand na Nepal.
Idadi ya watu huko Bihar ni karibu 400,000 na wana ushawishi mkubwa katika maeneo bunge wa 20 ya Seemanchal. Watu hawa wa Bihar hata hivyo wako nyuma sana kielimu na kiuchumi."

Chanzo cha picha, SEETU TEWARI/BBC
Hofu ya wasichana kutoolewa
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Takriban kilomita 200 kutoka kijiji cha Supaul huko Kochgama panchayat, kuna wakazi wa Shershahbadis pia katika Khairia panchayat ya mtaa wa Kodha wa Katihar.
"Mimi ni mwanamke wa Shershahbadi na baba yangu alitoa rupia elfu kumi kwa kiongozi kwa ajili ya ndoa yangu," anasema Reful Khatoon kutoka kijiji cha Dhimnagar. Mume wa Reful anafanya kazi ya kibarua huko Bengal.
Anasema, "Hii ndiyo kanuni hapa. Kiongozi atatoka kwa mvulana tu. Bila yeye ndoa haitafanyika. Msichana atasalia nyumbani. Kuna wasichana wengi ambao hawajaolewa kijijini kwetu."
"Hofu ya kuolewa au kutoolewa ni kubwa kiasi kwamba hata wasichana wenye umri wa miaka 14 wameingiwa na hofu ya kutoolewa."
Kando na pesa na elimu, rangi ya msichana ni muhimu
Wanawake wa jamii hii wako nyuma kiuchumi na kielimu. Msichana aliyesoma sana amefika darasa la tano.
Wanawake hawana uhuru wa kutoka nje ya nyumba na wanaume pia huenda katika miji mikubwa kama Surat, Jaipur, Kolkata kufanya kazi ya vibarua au kushona nguo.
Mbali na ujumbe wa ndoa, jambo ambalo ni muhimu zaidi katika jamii hii ni rangi ya mwili wa msichana.
Shahnaz Begum ndiye mkubwa kati ya ndugu zake 12. Dada zake wawili wadogo wameolewa lakini yeye hajaolewa.
Shahnaz anasema, "Dada zangu walikuwa waadilifu kwa hiyo waliolewa. Mimi ni mweusi kwa hiyo nani atanioa?
Marjana Khatoon, mwanafunzi wa wa chuo aliyekuwa ameketi karibu na Shahnaz, anasema kwa hasira, "Tunakabiliwa na ulimwengu ambao hauthamini watu weusi. Watu weusi hawaolewi hapa. Pia tulijua tangu utoto mwetu kwamba sisi sote ni maskini na rangi ya ngozi yetu ndio inatumaliza kabisa. Hali ni ngumu."
Abu Hilal, ni mwalimu lakini anafanya kazi ya kutetea haki za jamii ya Shershahbadi.
Anasema, "Katika miaka ya 1980, kulikuwa na mkutano wa Shershahbadi kutoka kote Bihar huko Kochgama. Katika mkutano huo Iliamuliwa kwamba wasichana pia wangechukua nafasi ya mvulana katika uhusiano, lakini hakuna kilichobadilika."












