Ifahamu ngome ya kijeshi iliyokua alama ya upinzani kwa Waukraine na kushindwa kwa Urusi

G

Chanzo cha picha, EPA

Tangu vilipoanza vita nchini Ukraine, kiwanja cha ndege cha kijeshi, na mji vilivyopo viungani mwa jijii la Kherson, vimepata hadhi ya umaarufu.

Mj wa Chornobaivka ulikamatwa na vikosi vya Urusi katika siku chache za mwanzo wa uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine mwezi wa Februari . Wakati huo, vikosi vya Ukraine vililazimika mara mbili kuushambulia.

 Uligeuka kuwa uwanja muhimu zaidi ya vya mapambano.

 Azma ya vikosi Urusi ilikuwa ni kuimarisha vikosi vyake katika eneo hilo la kusini na ilipeleka huko vifaa vyake kwa ndege.

Lengo la awali lilikuwa ni kusonga mbele upande wa mwambao wa kusini mwa Ukraine, na kufika kwanza katika Mykolaiv na Odessa.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ukraine wakitazama vifusi vya uwanja wa ndege , baada ya kuiteka tena

La muhimu zaidi, ngome ya anga ya Chornobaivka iliviruhusu vikosi vya Urusi kuepuka hatari ya kuvuka mto wakati walipokuwa wakisonga mbele kuelekea magharibi.

 Lakini kuendeleza uvamizi wa ngome kulionekana kuwa jambo gumu kwao.

Helikopta za Urusi na magari viliangamizwa na majenerali wawili wa Urusi waliuawa wakati vikosi vya Ukraine vilipozishambulia na kuziangusha chini- Kitu ambacho wakati mwingine kilikuwa kikitokea kila siku.

G

Chanzo cha picha, PLANET LABS

Alama ya upinzani

Ngome hiyo ilisifiwa kwa nyimbo na michoro na Waukraine wakaanza kutoa kejeli za ucheshi huku wakitazama vikosi vya Urusi vikipaa kuelekea kwenye ngome tena na tena, vikikabiliwa na kushindwa katika kila jaribio walilojaribu.

 Jina Chornobaivka liligeuka kuwa mzaha wa vita kwa Waukraine wanapozungumzia majeruhi wengi wa Urusi.

G

Chanzo cha picha, OLEKSANDR GREKHOV

Maelezo ya picha, Vibonzo vilionyesha hilo, kwa Bwana huyu wa Urusi , njia zote zinaelekea Chornobaivka: na kwenye kifo

Mapema mwezi huu, vikosi vya Ukraine viliuteka mji wa Kherson na ngome ya Chornobaivka karibu wakati mmoja. 

Wakati walipokuwa wakiondoka, wanajeshi wa Urusi waliacha eneo kubwa lenye mabomu ya kugekwa ardhini na kaburi la silaha za Urusi, magari na baadhi ya wafanyakazi wao.

Vikosi vya Urusi havijawahi kamwe kuthibitisha maelezo juu ya namna vilivyoshindwa na kupoteza maeneo ya kusini mwa Ukraine.

Katika kipindi cha siku tatu kuelekea kujiondoa kwa Urusi katika maeneo iliyokuwa imeyateka, vikosi vya Ukraine vilishambulia madaraja , vituo vya uongozaji wa vita na magala ya silaha ya Urusi.

Jamii iliyojitenga

Mbali na vifusi vilivyoachwa kutokana na uvamizi wa jeshi, historia ya jamii ndogo ya Chornobaivka inayoishi karibu na ngome ya kikosi cha anga, inaonyesha kuwa ilitengwa na dunia kwa miezi kadhaa, bila kujua kuwa ilikuwa ni alama ya upinzani wa taifa.

 "Tulitoka nje mara chake kwa mwezi kununua chakula. Hatukwenda popote," anasema Victoria, aliyefanya kazi kama mhudumu kwenye ngome hadi mwanzo wa vita, "tulipanda karoti, na viazi karibu na nyumba zetu."

g
Maelezo ya picha, Eneo linalozingira ngome ya vikosi vya anga sasa imezingirwa na mabomu ya kutegwa ardhini

Anakumbuka alivyokwenda kwa rafiki yake kununua mkate siku chache baada ya Urusi kuanza uvamizi , tarehe 8 Machi : "Warusi walikuja dukani wakiwa ndani ya kifaru na kufyatua makombora angani. Nilikuwa sijawahi kuona kifaru halisi cha kijeshi maishani mwangu".

 Mwezi mmoja baadaye, eneo lake la kazi liligeuka kuwa vifusi vya majengo.

 Vikosi vya Urusi biliharibu mawasiliano yote vilipoondoa kutoka Kherson tarehe 11 Novemba. Wakazi wa Chornobaivka hawakuweza kuwapigia sim ujamaa zao.