Noordin Haji: Mfahamu Mkuu mpya wa Shirika la Ujasusi la Kenya

Chanzo cha picha, ODPP
Rais wa Kenya William alimteua Noordin Haji kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Kenya, ambaye alikuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa zamani wa Kenya.
Hatua hii inajiri baada ya kustaafu kwa Jenerali Philip Kameru, ambaye alishikilia wadhifa huu tangu 2014.
Kisha Rais wa Kenya aliwasilisha uteuzi huo kwa Bunge ili kuidhinishwa, baada ya kikao chake kufunguliwa tena mwezi ujao.
Ikiwa wabunge wa Kenya wataidhinisha uteuzi huo, Noordin atarejea katika idara ya NIS baada ya miaka mitano katika idara ya mashtaka.
Noordin Haji ni nani?

Chanzo cha picha, Nurdine Hajji
Noordin alizaliwa tarehe 3 Julai 1973 huko Malindi, mkoa wa Pwani, Kenya.
Alipelekwa shule ya msingi katika maeneo tofauti kwani babake alikuwa mfanyakazi wa serikali ambaye alihamishwa mara kwa mara, kama vile Garissa, Nakuru, Nyahururu, Nyeri, Eldoret na Mombasa nchini Kenya.
Noordin ana shahada ya uzamili katika sera ya usalama wa taifa kutoka chuo kikuu nchini Australia.
Mama yake alikuwa mwalimu. Aliwasifu wazazi wake na kusema kwamba walimsaidia sana.
Alianza kazi yake kama wakili katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Pia alikuwa mwanachama wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi na alikuwa msimamizi wa sheria.
Pia alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Tawi la Uhalifu uliopangwa, na wakati huo moja ya majukumu yake ilikuwa kutoa ushauri kwa Mkurugenzi wa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi ya Kenya, haswa katika uwanja wa sheria za uhalifu uliopangwa.
Nuradeen, kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hii, alikuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Kenya, wakati wa uongozi wake, aliwafungulia mashitaka wanasiasa mashuhuri, ambao baadhi yao walikuwa na nyadhifa za juu, waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi.
Pia aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Uhalifu uliopangwa, wakati akifanya kazi katika idara hiyo hiyo ya NIS.

Chanzo cha picha, Nurdine Hajji
Haji alishika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma ya Kenya mnamo Aprili 2018. Hata hivyo, alikiri kwamba alikabiliwa na changamoto kubwa kutoka ndani na nje.
"Hata nikiwa katika kazi hii nilitishwa na watu ambao waliona kuwa maamuzi yangu, yawe ya kufunguliwa mashitaka au kutoshtakiwa, hayakuwa na manufaa kwao."
Noordin ana uzoefu mkubwa katika shughuli za uchunguzi na usalama, akiwa amehudumu kama Mahakama ya Juu ya Kenya kwa miaka 19.
Jina la Nuradeen na familia yake si geni masikioni mwa Wakenya.
Babake ni Mohammed Yusuf Haji, alikuwa mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya.
Yusuf Haji amekuwa akifanya kazi na serikali ya Kenya kwa muda mrefu, akianza kama gavana wa wilaya.
Pia alishikilia nyadhifa za Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Usalama na kwa muda mrefu alikuwa mbunge, na akawa seneta wa kwanza wa Garissa.
Yusuf Haji alifariki tarehe 15 Februari 2021 jijini Nairobi.
"Wakati mmoja alinusurika shambulio la Al-Shabaab"
Alinusurika shambulio la Al- Shabab

Chanzo cha picha, Reuters
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Noordin alipozungumza na vyombo vya habari mwaka wa 2021, kama mwendesha mashtaka mkuu wa Kenya, alisema kuwa yeye na familia yake walikuwa walengwa wa shambulio la kigaidi lililotekelezwa na al-Shabaab lenye makao yake nchini Somalia.
Akizungumza na kituo cha redio cha eneo hilo, Noordin alifichua kwamba babake, ambaye alifariki mwaka huo huo - Mohamed Yusuf Haji, ambaye alikuwa seneta wa Garissa - na yeye walikuwa kwenye "orodha ya al-shabaab ya watu ambao walinuiwa kuuawa katika shambulio hilo lilitokea kwenye " Jengo la kibiashara la "West Gate" jijini Nairobi mnamo 2013.
"Ukiangalia taarifa za kijasusi ambazo zilitolewa mwaka wa 2013, hasa ile inayohusu shambulio la West Gate, unaweza kuona kwamba mimi na familia yangu tulikuwa walengwa wa al-Shabaab," alisema.
"Al-Shabaab daima husema kwamba watatushughulikia sisi kama familia na kama mtu binafsi, na sababu ya kutushambulia ni kwa sababu ya kazi tuliyofanya." Alisema Noordin.












