Kwanini baadhi ya watu wanataka kujiua hadharani katika nchi hii?

Nchini Bangladesh, mwanaume mmoja alijiteketeza kwa moto kwenye eneo la kilabu cha pombe mjini Dhaka, na kufa mwaka mmoja baadaye.
Mapema, mwanaume mwingine alijionyesha moja kwa moja katika matangazo ya acebook Live na kujipiga kichwani.
Matukio kama haya ya kujiua hadharani yameibua hisia mbali mbali miongoni mwa watu wa Bangladesh
Kujipiga risasi kichwani
Mwezi februari mwaka huu, Abu Mohsin Khan, mfanyabiashara kutoka Dhaka alijiweka kwenye matangazo ya moja kwa moja ya Facbook na kujipiga risasi mwenyewe kichwani.
Abu Mohsin Khan alizungumza katika Facebook moja kwa moja kwa sauti ya utulivu kwa zaidi ya dakika 16. Alikuwa mtulivu alipokuwa akizungumza.
Miwani yake ilikuwa na kivuli. Alianza kwa kueleza utambulisho wake. Alielezea kutoridhishwa na watu wa familia yake.
Alielezea jinsi wafanyabiashara walivyodanganywa. Alikuwa akiongea taratibu huku akitulia kwa muda mfupi na mrefu katikati ya maneno mara nyingi.
Sauti yake ilikuwa ikisikika mara kwa mara. Mara mbili alirejea mistari ya Kalama, na kusoma Sura za Koran.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pia alithibitisha kwamba pisto aliyoitumia kujiua alikuwa ameipata kwa njia halali kwa kuonyesha kibali chake katika matangazo ya moja kwa moja yaani -Facebook Live.
Kujitoa kafara katika moto katika klabu
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Julai 4, mwanaume alijichoma kwa moto ghafla katika eneo la wazi mbele klabu ya waandishi wa habari. Kama anavyoonekana kwenye video, mwanaume huyo alionekana akiwa amelala akiwa amenyauka huku mikono na migu yake vikiwa vimetupwa mbali naye.
Moto ulikuwa ukiwaka kwenye mwili wake wote. Wakati ule, watu walikimbilia kwenye eneo la tukio na kumwagia maji ili kuuzima moto kwenye mwili wake. Licha ya kwamba wakati huo sehemu kubwa ya mwili wake ilikuwa imeungua.
Katika picha moja, maji yanamwagwa kwneye mwili wake, nguo zake ziliungua na alikuwa karibu mtupu.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 50 alitambuliwa kama Mohammad Anisur Rahman al maarufu Gazi Anis. Alikuwa ni mfanyabiashara.
Kaka yake Anisur Rahman, Nazrul Islam ameiambia BBC Bangla kwamba kaka yake kwanza alianza biashara ya kuuza magari. Aliiacha biashara hiyo na kuanza kufanya biashara na mmiliki wa magari Henolax.
Alijichoma moto Jumatatu baada ya kudanganywa pale.
Lazwa katika ghospitali ya taasisi ya Sheikh Hasina National Burn mjini Dhaka. Alifariki pale Jumanne asubuhi
Kujaribu kuelezea hasira na kuvutia umakini:

Dkt. Mehzabin Haque, Profesa wa elimu na ushauri wa kisaikolojia, alisema kwamba mtu anayetaka kutekeleza mauji yake hadharani huwa anakuwa na uhakika kwa 100% kwamba anataka kufa.
Alizungumzia kuunga mkono muungano wa Marekani, lakini akasema kuwa kiasi fulani cha uhuru sio jibu. Mtu anayetekeleza mauaji yake huwa anahisi kufanya hivyo. "
"Halafu anataka kufanya kitu ili kila mtu amtazame. Kila mtu analazimishwa kulipia garama yake. Kama angejiua ndani ya nyumba ,labda hakuna mtu fulani asingejua, halafu watu wasahau." "Lakini wakati mambo yanapotokea hadharani, ni muhimu kuelewa kwamba kwamba hajaribu tu kujiua pekee, anaingiza hasira na chuki ndani ya mtu mwingine mara anapokufa. Wanachagua njia hii ya kutoa hasira yao kuwapokezea watu wengine wanaotaka waipate. "
'Kan Pate Roi ni kitengo kinachotoa usaidizi wa kisaikolojia nchini Bangladesh. Shirika hilo lisilo la kiserikali linasema kuwa kuanzia Aprili 2020 hadi Mei 2021 watu wapatao 13,000 wamekwishapiga simu kwao kuomba msaada wa ushauri nasaha.
Wengi wao ni wanaume. Wengi wanaume haw ani wale walio kati ya umri wa miaka 20 na 40.
Arun Das, ambaye ni mratibu wa shirika hilo, anasema wengi wao huwa wanaelezea shinikizo la kipato kama chanzo cha hisia za msongo wa mawazo.
"Wengi wao huelezea kuhusu matatizo ya mahusiano, na wengi wao ni wasichana wanaozungumzia hili. Wanaume mara nyingi huwa na matatizo ya kikazi, wanapitia ugumu wa kupata fedha, ndio maana walikuwa na msongo wa mawazo- wanaume huzungumzia kuhusu mambo haya. Simu nyingine tunazozipata kutoka kwa wanaume ni kuhusu uraibu . "
Profesa Dkt. Mehzabin Haque anasema kwamba tukio la mauaji ya kujiua hadharani huwashitua sana watu.
"Kadhri jambo linavyotisha ndivyo linavyowasaidia kuwa ‘’njia ya kuondokana nalo’’ kwa wale wanaohangaishwa na msongo wa mawazo ," alisema.














