Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chakula kinachozalishwa maabara kuanza kuuzwa mitaani
Nyama, maziwa, na sukari vilivyozalishwa maabara vinaweza kuanza kuuzwa kwa matumizi ya binadamu.
Itaanza kuuzwa huko Uingereza kwa mara ya kwanza ndani ya miaka miwili, mapema kuliko ilivyotarajiwa.
Shirika la Viwango vya Chakula (FSA) linachunguza jinsi linavyoweza kuharakisha mchakato wa uidhinishwaji wa vyakula vilivyozalishwa maabara.
Bidhaa hizo zinakuzwa kutoka kwa seli za mimea midogo yenye kemikali.
Makampuni ya Uingereza yameongoza katika uwanja huu kisayansi, lakini yanaona kwamba yamezuiwa na kanuni za sasa.
Chakula cha mbwa kilichozalishwa kutoka kwenye nyama iliyokuzwa kiwandani kilianza kuuzwa Uingereza kwa mara ya kwanza mwezi jana.
Mnamo 2020, Singapore ilikua nchi ya kwanza kuidhinisha uuzaji wa nyama inayozalishwa kwa seli kwa matumizi ya binadamu, ikifuatiwa na Marekani miaka mitatu baadaye na Israeli mwaka jana.
Hata hivyo, Italia na majimbo ya Alabama na Florida nchini Marekani yameweka marufuku.
Mamlaka inayosimamia Chakula (FSA) inapanga kuweka kanuni mpya kwa kushirikiana na wataalamu wa makampuni ya chakula na watafiti.
Mamlaka hiyo inakusudia kukamilisha tathmini kamili ya usalama wa vyakula vilivyozalishwa maabara ndani ya mchakato wa miaka miwili inayoanza.
Lakini wakosoaji wanasema kwamba kuwa na makampuni yaliyohusika katika uundaji wa kanuni mpya kuna mgongano wa maslahi.
Mpango huu ni jibu kwa wasiwasi wa makampuni ya Uingereza kwamba yanapoteza nafasi katika ushindani wa kimataifa, ambapo mchakato wa idhini unachukua nusu ya muda.
Profesa Robin May, mtaalamu mkuu wa FSA, aliiambia BBC News kwamba hakutakuwa na mjadala kuhusu usalama wa watumiaji.
"Tunafanya kazi kwa karibu sana na makampuni yanayohusika na makundi ya wataalamu ili kubuni muundo wa udhibiti ambao ni mzuri, lakini kwa gharama zote kuhakikisha usalama wa bidhaa hizi unabaki kuwa wa juu iwezekanavyo," alisema.
Hata hivyo, wakosoaji kama Pat Thomas, mkurugenzi wa kikundi cha kampeni cha Beyond GM, hawaamini mbinu hii.
"Makampuni yaliyohusika katika kusaidia FSA kuunda kanuni hizi ni yale yanayoweza kufaidika zaidi kutokana na kupungua kwa udhibiti, na kama hii ingekuwa bidhaa nyingine yoyote ya chakula, tungesngependezwa nayo," alisema.
Waziri wa Sayansi, Lord Vallance, alikubaliana na mchakato unaoelezwa kama "kupunguzwa kwa udhibiti."
"Hii sio kupunguzwa kwa udhibiti, ni udhibiti unaoelekea katika ubunifu," aliiambia BBC News.
"Hii ni tofauti muhimu, kwa sababu tunajaribu kupata udhibiti unaoendana na mahitaji ya ubunifu na kupunguza urasimu."
Vyakula vilivyozalishwa maabara vinakuzwa kuwa tishu za mimea au wanyama kutoka kwenye seli ndogo.
Hii wakati mwingine inaweza kuhusisha ubadilishaji wa jeni ili kuboresha chakula.
Manufaa yake ni bora kwa mazingira na kwa afya zaidi.
Serikali inataka makampuni ya vyakula vilivyozalishwa maabara yaendelee kustawi kwa sababu inatumaini yanaweza kuunda ajira mpya na kuchangia ukuaji wa uchumi.
Uingereza ni bora katika sayansi, lakini mchakato wa sasa wa kuidhinisha unachukua muda mrefu zaidi kuliko katika nchi nyingine.
Singapore, Marekani, na Israeli hasa wana taratibu za haraka.
Ivy Farm Technologies huko Oxford iko tayari kuanzisha nyama za maabara, zinazozalishwa kutoka kwenye seli zilizochukuliwa kutoka kwenye seli za ng'ombe aina ya Wagyu na Aberdeen Angus.
Kampuni hiyo iliiomba idhini ya kuuza minofu yake kwenye mikahawa mwanzoni mwa mwaka jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ivy Farm, Dkt. Harsh Amin, alieleza kwamba miaka miwili ni muda mrefu sana kusubiri.
"Kama tunaweza kupunguza muda huo kuwa chini ya mwaka mmoja, huku tukiendelea kuimarisha zaidi viwango vya usalama wa chakula Uingereza, hilo litaleta msaada kwa makampuni yanayoanza kama yetu."
Dkt. Alicia Graham ana simulizi kama hiyo. Akifanya kazi katika Kituo cha Bezos cha Imperial College kilichopo magharibi mwa London, amepata njia mbadala ya kukuza sukari.
Inahusisha kuingiza jeni zianzopatikana katika matunda ya berry.
Mchakato huu unamwezesha kuzalisha kiasi kikubwa cha kristali zinazofanya iwe tamu.
Haisababishi unene, anasema, ina utamu unaoweza kutumika kama njia mbadala na ya kiafya katika vinywaji laini.
Katika jaribio hili, nimeruhusiwa kuonja. Ilikuwa tamu sana na kwa mbali kuna ladha ya asidi na matunda, kama ladha ya maji ya limau.
Lakini kampuni ya Dkt. Graham, MadeSweetly, haijaruhusiwa kuuza hadi ipate idhini.
"Njia ya kupata idhini si rahisi," ananiambia.
"Hizi ni teknolojia mpya, ambazo sio rahisi kwa msimamizi kuzifuata.
Lakini hiyo inamaanisha hatuna njia maalum ya kuidhinisha bidhaa, na hiyo ndio tungependa."
Mamlaka ya usimamizi wa Chakula (FSA) inasema itakamilisha tathmini kamili ya usalama wa vyakula viwili vilivyozalishwa maabara ndani ya miaka miwili ijayo na kuwa na mifumo ya haraka na bora kwa maombi ya uidhinishwaji wa vyakula vipya vilivyotengenezwa maabara.
Profesa May wa FSA anasema kuwa lengo la kushirikiana na wataalamu kutoka kwenye makampuni yaliyohusika pamoja na wasomi ni kuhakikisha sayansi inafanyika vizuri.
"Inaweza kuwa viumu sana, na ni muhimu kuelewa sayansi ili kuhakikisha vyakula ni salama kabla ya kuidhinisha."
Lakini Bi. Thomas anasema kuwa vyakula hivi vya teknolojia ya juu huenda visiwe rafiki kwa mazingira kama inavyodaiwa, kutokana na kutumia nishati katika uzalishaji na kwamba katika baadhi ya nyakati manufaa yake ya kiafya yanapotosha.
"Vyakula vilivyozalishwa maabara ni vyakula vilivyoandaliwa sana na tuko katika enzi ambazo tunajaribu kuwahimiza watu kupunguza kula vyakula vya namna hiyo, kwa sababu vina athari za kiafya," alisema.
"Na ni vyema kusema kwamba vyakula hivi vilivyoandaliwa sana havijawahi kuwa sehemu ya lishe ya binadamu."