Salman Rushdie ni nani? Mwandishi aliyeibuka kutoka mafichoni

Salman Rushdie, outside King's College chapel in Cambridge in 1993

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Salman Rushdie, nje ya kanisa dogo la King's College katika Cambridge mwaka 1993

Kwa miongo mitano aliyojihusisha na fasihi, Sir Salman Rushdie si mgeni na vitisho vya kuaawa anavyokabiliwa navyo kutokana na kazi yake.

Mwandishi huyu wa riwaya ni mmoja kati ya waandishi wa Uingereza wanao pigiwa upatu na aliye na ufanisi, wakati riwaya yake ya pili, Midnight's Children, ikishinda tuzo ya Booker Prize mnamo 1981.

Lakini ni riwaya yake ya nne, The Satanic Verses, iliyochapishwa mnamo 1988, ambayo ndio ilikumbwa na mzozo na kupingwa kimataifa na kuzusha rabsha katika kiwango ambacho hakikutarajiwa.

Katika ulimwengu wa kiislamu, Waislamu wengi walighadhabishwa baada ya kuchapishwa kitabu hicho, wakilalamika kuwa namna mtume Muhammad alivyoelezewa ndani ya kitabu hicho ni tusi kubwa kwa imani ya kiislamu.

Rushdie, mwenye umri wa miaka 75 alitishiwa maisha na alilazimika kuingia mafichoni, na serikali ya Uingereza ilimpatia ulinzi wa polisi.

Mara moja Iran ilivunja uhusiano na Uingereza katika kulalamika na kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ruhollah Khomeini, alitangaza fatwa - akitaka kiongozi huyo auawe mnamo 1989 – mwaka mmoja baada ya kitabu chake kuchapishwa.

Lakini katika mataifa ya magharibi, waandishi na wataalamu walikemea tishio dhidi ya uhuru wa kujieleza lililotokana na hisia zilizoibuka kufuatia kutolewa kwa kitabu hicho.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aya ya Shetani, kilichapishwa mwaka 1988, na kusababisha msuko suko wa kimataifa wa kiwango ambach hakikutarajiwa
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Salman Rushdie alizaliwa Bombay – ambayo sasa inajulikana kama Mumbai – miezi miwili kabla ya India kujitangazia uhuru dhidi ya Uingereza.

 Akiwa na umri wa miaka 14, alipelekwa England kusoma shule katika mji wa Rugby, baadaye alijipatia shahada ya Historia katika chou cha kifahari Kings College huko Cambridge.

 Alipata uraia Uingereza, na kuisahau dini ya Kiislamu. Alifanya kazi kwa muda mfupi kama muigizaji alafu baadaye kama mwandishi wa matangazo ya biashara, huku akiwa anandelea kuandika riwaya.

 Kitabu chake cha kwanza kuchapishwa, Grimus, hakikuapata ufanisi mkubwa, lakini baadhi ya wakosoaji walimuona kama mwandishi mwenye uwezo wa kutosha.

 Ilimchukua Rushdie miaka mitano kuandika kitabu chake cha pili, Midnight's Children, kilichoshinda tuzo ya Booker Prize mnamo 1981. Kilisifiwa pakubwa na alifanikiwa kuuza nakala nusu milioni.

Kitabu hicho cha Midnight's Children kilikuwa ni kuhusu India, na riwaya yake ya tatu Shame – kilichotolewa mnamo 1983 – kilikuwa ni kuhusu mabadiliko ya Pakistan. Miaka minne baadaye , aliandika riwaya ya The Jaguar Smile, iliohadithia safari ya Nicaragua.

 Mnamo Septemba 1988, kazi ambayo ingelihatarisha Maisha yake, Riwaya ya The Satanic Verses, ilichapishwa.

Riwaya hiyo ilizusha ghadhabu au hasira miongoni mwa baadhi ya wasilamu, walioona yaliomo ndani ya kitabu hicho ni kufuru.

 India ilikuwa nchi ya kwanza kukipiga marufuku. Pakistan ikafuata kama zilivyofuata kufanya pia mataifa mengine ya kiislamu duniani na Afrika kusini pia.

 Riwaya hiyo ilisifiwa katika sehemu nyingi na ilishinda tuzo ya riwaya ya Whitbread Prize. Lakini shutuma ziliongezeka, na miezi miwili baadaye maandamano yalishika kasi.

Waandmaanaji walishuhudiwa wakiandamana kupinga Aya za shetani mjini Paris Februari 1989

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waandmaanaji walishuhudiwa wakiandamana kupinga Aya za shetani mjini Paris Februari 1989

Baadhi ya wasilamu waliona kama ameitusi dini ya kiislamu.

Walipinga – miongoni mwa mengine – makahaba wawili ndani ya kitabu hicho kupewa majina ya wake za Mtume Muhammad.

 Kichwa cha kitabu hicho kilitaja aya mbili zilizotolewa na Mtume Muhammad ndani ya Quran, kwasababu aliamini zilitokana na Shetani.

 January mwaka 1989, Waislamu huko Bradford Uingereza waliteketeza moto nakala ya kitabu hicho na duka la kuuza vitabu WHSmith liliacha kukiweka kitabu hicho. Rushdie alipinga mashtaka ya kukufuru.

 Huko Mumbai, nyumbani anakotokea Rushdie, Watu 12 waliuawa wakati wa maandamano makali ya Waislamu, Ubalozi wa Uingereza Tehran ulipigwa mawe, na ktita cha $3m (£2.5m) kiliahidiwa kwa yeyote atakayemuua mwandishi huyo.

 Huku hayo yakijiri, nchini Uingereza baadhi ya viongozi wa kiislamu walisihi kuwa na utulivu, wengine walimuunga mkono Ayatollah. Marekani, Ufaransa na mataifa mengine ya magharii yalishutumu vitisho hivyo vya kumuua Rushdie.

Wakati huu Rushdie ambaye alikuwa mafichoni na mkewe chini ya ulinzi mkali wa polisi - alielezea kujuta pakubwa kwa mfadhaiko aliousababisha kwa waislamu, lakini Ayatollah raliitisha upya kuuawa kwa mwandishi huyo.

Ofisi za kampuni ya uchapishaji vitabu Viking Penguin mjini London zilizingirwa na kuliwasilishwa vitisho vya mauaji katika ofisi zake New York.

Lakini kitabu hicho kiliuzwa sana katika pande zote za Atlantiki. Maandamano dhidi ya hisia kali za kiislamu yaliungwa mkono katika mataifa ya Umoja wa Ulaya, yote ambayo yaliamua kuwarudisha nyumbani mabalozi wao kutoka Tehran.

Muislamu Mhindi aliyevalia barakoaya Rushdie alikuwa anapinga uwepo wa mwandishi katika Bombay mwezi Januari 2004

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muislamu Mhindi aliyevalia barakoaya Rushdie alikuwa anapinga uwepo wa mwandishi katika Bombay mwezi Januari 2004
Aya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rushdie halilazimika kwenye mafichoni na kupata ulinzi wa polisi kutokana na kitabu chake cha Aya za Shetani

Lakini tishio hizo hazikuelekezwa kwa Rushdie tu kutokana na kitabu hicho.

 Mfasiri wa kitabu hicho kutoka Japan alipatikana ameuawa katika chou kimoja kikuu kaskzini mashriki mwa Tokoyo mnamo Julai 1991.

 Polisi anasema mfasiri huyo, Hitoshi Igarashi, aliyehudumu kama mhadhiri msaidizi alidungwa kisu mara kadhaa na kuachwa nje ya ofisi yake katika chou kikuu cha Tsukuba University. Aliyemuua hajapatikana.

 Mapema mwezi huo huo, aliyekitafsiri kitabu hicho cha Satanic Verses, Ettore Capriolo, alichomwa kisu nyumbani kwake huko Milan ijapokuwa aliponea shambulio hilo.

 Na aliyekitafsiri kitabu hicho kutoka Norway, William Nygaard, alipigwa risasi mnamo 1993 nje ya nyumba yake Oslo – hata na yeye aliponea.

Mwandishi tajika, vitabu vyake vya baadaye Rushdie ni Pamoja na riwaya ya Watoto, Haroun and the Sea of Stories (1990), kitabu chenye mkusanyiko wa insha, Imaginary Homelands (1991), na riwaya za East, West (1994), The Moor's Last Sigh (1995), The Ground Beneath Her Feet (1999), Pamoja na Fury (2001).

 Alihusika katika uigizaji waw a riwaya yake ya Midnight's Children ilioonyeshwa London mnamo 2003.

 Katika miongo miwili iliopita amechapisha Shalimar the Clown, The Enchantress of Florence, Two Years Eight Months na Twenty-Eight Nights, The Golden House na Quichotte.

Rushdie ameoa mara nne na ana Watoto wawili.

 Hivi sasa anaishi Marekani na alituzwa heshima na Malkia wa Uingereza kwa huduma zake katika fasihi.

 Mnamo 2012, alichapisha kumbukumbu ya Maisha yake katika kukabiliwa na mzozo wa kitabu chake The Satanic Verses.

 Mnamo 1998 serikali ya Iran iliacha kuunga rasmi hukumu ya kifo dhidi ya Rushdie na katika miaka ya hivi karibuni mwandishi huyo amekuwa akifurahia kiwango kipya cha uhuru.

 Lakini tishio dhidi ya Maisha yake bado zinaendelea chini chini, na kiongozi mkuu wa sasa wa Iran - Ayatollah Ali Khamenei – wakati mmoja alisema kuwa fatwa dhidi ya Rushdie ni kama "risasi iliyofyetuliwa ambayo haitulii mpaka itakapolenga shabaha".