'Ninapigania kuishi Rwanda'
Na Lebo Diseko
BBC News, Kigali

"Ninapigania kuishi tu," ananiambia mwanaume anayeonekana kuwa na hofu kayika sauti inayosikika kutetemeka kiasi.
Tumesimama kwenye magharibi mwa mji mkuu wa Rwanda Kigali. Umezingirwa na miti ambayo imetuficha macho ya wadadisi ambao wangetaka kujua kile tunachoongea.
Mohammed alikuja katika nchi hii akitafuta uhamiaji. Anasema alitorokea Rwanda akitoka Ethiopia, ambako amekuwa mkimbizi hadi pale mawakala kutoka katika nchi yake ya nyumbani walipojaribu kumteka nyara.
Mohammed anasema maisha yake mjini Kigali yamekuwa magumu, lakini anahofia sana athari za kuzungumza na mwandishi wa habari kiasi kwamba aliniomba nisifichue jina lake halisi au nchi alikotoka, isipokuwa kwamba iko katika Afrika.
Kwa siku kadhaa tumekuwa tukijaribu kumpata mtu anayeomba uhamiaji nchini Rwanda kuzungumza nasi na kurekodiwa. Mara kwa mara watu wanakubali, na ghafla hawapatikani, mara nyingi baada ya kutembelewa na ‘’kiongozi wa kijamii’.
"Nimeomba uhamiaji," Mohammed ananiambia.
"Maafisa hawasemi hapana, lakini kila kitu ni ‘kesho’, au 'uje wiki ijayo'. Ni karibu mwaka mmoja hawajanipatia’’.
Nilizungumza na Mohammed kuhusiana na uamuzi wa mahakama ya juu zaidi ya London - kwamba ilikuwa ni kinyume cha sheria kwa serikali ya Uingereza kuwa na mpango tata wa kuwatuma wahamiaji Rwanda, ambako kundi Human Rights Watch (HRW) linasea, kuna, ‘’ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza, na kuwafunga watu kiholela, kuwatendea mabaya, na mateso".

Shirika la Umoja wa Mataifala wakimbizi liliambia mahakama kwamba Rwanda inakosa "kiwango cha chini cha mfumo wa upatikanaji, kuaminika na usawa kwa ajili ya wahamiaji ".
Lina wasi wasi kwamba watu wanaweza kurejeshwa katika nchi ambazo wanaweza kukabiliwa na mateso.
Na katika ripoti yake ya mwezi Juni shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilisema kwamba " mchakato wa ufanisi na unaozingatia muda kwa wanaoomba uhamiaji unatia hofu,ambapo maamuzi huchukua hadi mwaka au miaka miwili kutolewa katika baadhi ya visa ".
Mohammed anasema anahisi maisha yake yamo mashakani. Hawezi kufanya kazi kulingana na sheria kwasababu hana makaratasi yanayofaa.
"Marafiki na ndugu husaidia," ananiambia, akiongeza kuwa kazi za ajabu humpatia kipato kidogo.
Lakini kwasababu ana mke na watoto wa kuwasaidia, ukosefu wa uhakika wa maisha umemuathiri.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
"Wale waliohojiwa walisema walilengwa kutokana na mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wao wa kijinsia na kutendewa vibaya zaidi kuliko mahabusu wengine . Maafisa wa polisi au walinzi waliwashutumu kwa kutokuwa na makazi, wezi , wahalifu na kuwashikilia katika chumba kilichotengwa kwa ajili ya wanaume 'wahalifu'," lilisema shirika hilo.
Mtu mmoja anayefahamu unyanyapaa unaoambatana na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja nchini Rwanda ni Patrick Uwayezu.
Ni mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja wa kanisa la Kiinjilisti linalofahamika kama Evangelical Church of God in Africa nchini Rwanda, likiwa ni kanisa pekee mjini Kigali linalowapokea waaumini wapenzi wa jinsia moja LGBT.
Mwanaume mwembamba, mwenye sauti nzuri ya kuimba, anaongoza kwaya Jumapili tulipotembelea kanisa.
Baadaye aliniambia kuwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja LGBT mara nyingi hupata ugumu wa kupata huduma kama vile huduma ya afya kwasababu ya mitizamo kuwahusu. Pia inaweza kuathiri fursa za watu za kupata kazi.
"Iwapo utaficha utambulisho wako wanaweza kukupa kazi. Lakini kama [waajiri watabaini ] utambulisho watakwambia: 'nenda, nenda, hatuwezi kufanyakazi na wewe .'"
"Ninadhani watu wengi hawatuelewi katika nchi hii ," anasema.

Katika ziara yetu ya siku sita tuliomba mara sita kufanya mahojiano na serikali. Ingawa Msemaji alikubali kufanya mahojiano, mahojiano yaliyoahidiwa hayakufanyika.
Hatahivyo tulipata taarifa ambapo msemaji alisema : "Ubaguzi wa aina zote ni kinyume cha sheria kulingana na katiba yetu na Rwanda inamkaribisha kila mtu."
Taarifa ilisema kuwa msimamo wa Umoja wa Mataifa ulikuwa ni "wazi unakinzana" kwani uliikosoa Rwanda huku ukiendelea kuwapeleka wahamiaji nchini humo, wakiwemo zaidi ya 100 kutoka Libya mapema mwaka huu.
Pia kuna hadithi za wakimbizi wenye mafanikio nchini Rwanda. Teklay Teame aliwasili hapa kutoka Eritrea takriban miaka 25 iliyopita, katika mwaka 1998.
Kwasasa anafanya biashara ya maduka ya jumla na Supamaketi.
Wafanyakazi wake wanashughuli nyingi za kujaza lori maboksi makubwa na kuyabeba katika moja ya maduka yake mengi wakati nilipokutana naye.

"Nilipowasili hapa, kila kitu kilikuwa kipya kwangu. Lakini watu walikuwa rafiki sana haikunichukua muda mrefu kuingiliana nao. Nilianza na wafanyakazi wanne. Sasa ninawafanyakazi zaidi ya 600 ,"anasema.
Tofauti na wakimbizi wengi, Bw Teklay alikuwa ana pesa zinazohitajika kuanza biashara yake.
Bado, anasema, Rwanda inatoa fursa kwa wote, ili mradi ufuate sheria.
Bw Teklay anasema anafahamu Waeritrea ambao "walikuja hapa bila kitu kama wakimbizi. Lakini wameanza maisha yao na biashara."
Nilimuuliza iwapo anaelewa hofu ya wale waliopinga mpango wa wanaoomba uhamiaji Uingereza wa kupelekwa Rwanda.
"Sijui ni nini wanachoogopa, lakini sioni haja yoyote ya kuogopa hapa," anajibu.
Mandhari ilionekana kuwa nzuri sana wakti jua lilipowaka juu ya Kigali: Jua lenye mwanagza jekundu linatoweka nyuma ya vilima.
Msururu wa magari barabarani na jiji chini linampangilio na ufanisi, hali ambayo nchi nyingine duniani zinaweza kuionea wivu. Wengi wanasema nyuma ya hayo kuna hali ya hofu.
Swali kwa majaji wa Uingereza ni iwapo hofu hiyo inatosha kuachana na mpango wa kuwatuma waombaji wa uhamiaji Rwanda.















