Uhamiaji: Kwanini Uingereza inataka kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda?

Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly anatia saini mkataba mpya wa uhamiaji na Rwanda ili kujaribu kushughulikia wasiwasi kuhusu mpango wa serikali wa kuwapeleka wanaotafuta hifadhi nchini humo.
Mwezi Novemba mwaka huu, Mahakama ya Juu ya Uingereza iliamua kwamba mpango huo haukuwa halali kwa sababu ya hatari ya waomba hifadhi waliotumwa Rwanda kurudishwa katika nchi zao, ambapo wanaweza kukabiliwa na madhara.
Mpango wa hifadhi ya Rwanda ni upi?
Mpango huo wa majaribio wa miaka mitano utawezesha baadhi ya wakimbizi wanaowasili nchini Uingereza kupelekwa Rwanda, ili wakaombe hifadhi huko.
Kundi la kwanza la waomba hifadhi linatarajiwa kuwasili Juni 14.
Mpango huo zaidi unalenga wahamiaji wachanga wasio na waume ambao hufika kwa kile ambacho serikali ya Uingereza inakiita "mbinu zisizo halali, hatari au zisizo za lazima", kama vile kwa boti ndogo au kufichwa kwenye lori.
Waomba hifadhi wa Uingereza wanatoka wapi?
Hadi hivi karibuni, waomba hifadhi wengi wanaovuka bahari kuingia Ungereza wanatoka Iran - 80% mwaka 2018, na 66% mwaka 2019.
Lakini kufikia sasa kuna mchanganyiko wawatu kutoka mataifa tofauti. Wairan walikuwa kama 30% ya waliofika kwa mashua ndogo mwaka jana. Takriban 21% walikuwa Wairaq, 11% Waeritrea na 9% Wasyria. Takriban 75% walikuwa wanaume wenye umri wa miaka 18 hadi 39.
Mnamo 2021, watu 28,526 wanajulikana kuvuka Idhaa ya Kiingereza kwa boti ndogo - kutoka 8,404 mnamo 2020. Idadi hiyo inatarajiwa kuogezeka zaidi mwaka huu.

Ni watu wangapi wamepelekwa Rwanda?
"Mtu yeyote aliyeingia Uingereza kinyume cha sheria" tangu Januari 1 anaweza kupelekwa Rwanda, hakuna idadi iliyowekwa, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema.
Lakini chanzo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani kiliiambia BBC kwamba, katika wakimbizi 37 wa awali waliopangwa kusafirishwa Jumanne, lakini changamoto za kisheria kuhusu utumwa wa kisasa na haki za binadamu zimepunguza idadi hiyo kwa kiasi kikubwa.
Kwa mujibu wa shirika la upendo Care4Calais, watu 11 sasa wanaweza kusafirishwa.
Je, ni hatua gani za kisheria?
Mashirika ya Misaada yanapinga mpango huo mahakamani, yakisema wanaotafuta hifadhi hawapewi muda wa kutosha kukata rufaa ya haki ya kukaa Uingereza.
Makundi mengine yamehoji iwapo Rwanda ni salama kwa wanaotafuta hifadhi na kwamba sera hiyo inakiuka sheria za haki za binadamu.
Mahakama ya Rufaa ya Uingereza ilikataa ombi la kusitisha safari ya ndege siku ya Jumanne.
Shirika la misaada la Asylum Aid limetuma maombi ya zuio dhidi ya safari hiyo ya ndege.
Mwanasheria wa Umoja wa Mataifa aliiambia Mahakama Kuu ya London kwamba wakimbizi watakuwa katika hatari ya "madhara makubwa, yasiyoweza kurekebishwa" ikiwa watapelekwa Rwanda.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini Bw. Johnson alisema serikali ilijua kwamba "mawakili makini sana" watapinga mahakamani sera hiyo.
Alisema wanaharakati "Wanaharakati wanataka kuwa na njia ya wazi kabisa ya uhamiaji" na ilikuwa muhimu "kukomesha magenge ya wahalifu" kusafirisha watu katika Idhaa katika mashua hatari.
Wakosoaji wa mpango huo ni pamoja na Justin Welby, mkuu wa Kanisa la Uingereza, ambaye alisema "kanuni lazima izingatie hukumu ya Mungu, na haiwezi". Na kulingana na ripoti za gazeti, Prince Charles ameelezea kuwa "ya kutisha".
Itagharimu pesa ngapi?
Uingereza inawekeza paundi milioni 120 katika "maendeleo ya uchumi na ukuaji wa Rwanda" kama sehemu ya makubaliano.
Ofisi ya Mambo ya Ndani ilisema mfumo wa hifadhi ya Uingereza kwa sasa unagharimu £1.5bn kwa mwaka, huku zaidi ya £4.7m kwa siku zikitumika katika hoteli kuwahudumia wahamiaji wasio na makazi.
Ulinganisho umefanywa na mfumo wa Australia wa kuwahudumia wahamiaji nje ya nchi, ambao ulikadiriwa kugharimu $957m (£546m) mnamo 2021-22.
Gharama ya kuwaondoa watu kutoka Uingereza kwa ndege ya kukodi ilikuwa zaidi ya pauni 13,000 kwa kila mtu mnamo 2020.
Rwanda inawahifadhi vipi wakimbizi?
Rwanda inarekebisha hosteli karibu na mji mkuu, Kigali, ili kuwahifadhi wahamiaji hao kutoka Uingereza. Waandishi wa habari ambao wametembelea maeneo hayo wanasema ni ya msingi.
Nchi hiyo tayari ina yakriban wakimbizi 150,000, wengi kutoka nchi jirani za Burundi na DR Congo.
Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya pia wameanzisha "kituo cha usafiri" huko Gashora, kilomita 90 kutoka mji mkuu, Kigali, ili kuwahifadhi wakimbizi 300 kutoka Mashariki ya Kati na kwingineko barani Afrika.
Walijaribu kuvuka bahari ya Mediterania kutoka Libya hadi Ulaya, lakini walinaswa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Libya.
Nchi hiyo kwa sasa ni nyumbani kwa wakimbizi 150,000, wengi wao kutoka nchi jirani ya Burundi na DR Congo.
Maisha yako vipi Rwanda?
Baadhi ya wakimbizi nchini Rwanda wameweza kupata kazi kama vibarua wa mashambani na watumishi wa nyumbani. Hata hivyo, wengi hawana ajira na wanategemea manufaa ya serikali ya takriban £35 kwa mwezi.
Serikali ya Rwanda inasema nchi hiyo imekuwa na ukuaji wa "muujiza" wa kiuchumi tangu 1994, wakati vita vya mauaji ya halaiki vilipoua watu 800,000.
Idadi ya watu wanaoishi chini ya mstari wa umaskini wa kitaifa imepungua kutoka 77% mwaka wa 2001 hadi 55% mwaka wa 2017. Umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa uliongezeka kutoka miaka 29 katikati ya miaka ya 1990 hadi miaka 69 mwaka wa 2019.
Hata hivyo, Rwanda inasalia kuwa mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, ikishika nafasi ya 165 kwa mapato ya wastani kwa kila mkuu wa watu. Takriban 70% ya watu milioni 13 nchini humo wanaishi kutoka mkono hadi mdomo kama wakulima wa kujikimu.













