Je binadamu ni wa kulaumiwa kwa hali mbaya ya hewa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wataalamu wanaonya kuwa magharibi mwa Ufaransa kunakabiliwa na "kiwango cha joto cha juu ambacho hakikutarajiwa" huku wimbi la joto likiendelea kuyapiga maeneo mengi ya Ulaya.
Viwango vya juu vya joto pia vinatarajiwa kuwa vya rekodi ya juu katia Uingereza, na visa vya moto katika Uhispania, Ureno na Ugiriki vimewalazimisha maelfu kukimbia.
Maeneo ya India na Pakistan pia yalishuhudia viwango vya juu kama 50C katika msururu wa mawimbi ya joto mapema mwaka huu, na Ethiopia na Somalia zimekuwa zikishuhudia vipindi vya ukame zaidi kuwahi kuzikumbwa kwa miongo kadhaa.
"Tazama kile ambacho mabadiliko ya tabia nchi yanafanya kwa sayari," watu mara kwa mara huzungumzia kwenye mitandao ya kijamii ya habari.
Lakini je inawezekana kufahamu iwapo matukio ya hali zisizo za kawaida za hewa kama hizo tunazozishuhudia yana uhusiano na ongozeko la joto duniani linalosababishwa ana binadamu?
Chanzo cha hali ya hewa
Jibu fupi ni ndio. Wanasayansi wengi wanakubaliana kwamba katika wanaweza kujibu swali la ni kwanini tukio lilisababishwa au kutokusababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, kwasababu ya elimu ya sayansi inayofahamika kama matukio yasiyo ya kawaida ya mazingira.
Ni kitengo cha sayansi, lakini ambacho "kinachunguza athari na sababu zake ",kulingana na Dr Thomas Smith, profesa msaidizi katika jiografia ya mazingira katika chuo kikuu cha uchumi cha London - London School of Economics.
Kikundi ca wanasayansi katika eneo hili kinachofahamika kama (WWA) -hivi karibuni kilichapisha muongozo kuhusu jinsi ya kuelezea uhusiano huu baina ya matukio yasiyo ya kawaida ya hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mmoja wa waandishi wakuu, Mwanamazingira Mjerumani Friederike Otto wa taasisi ya Imperial College London, aliiambia BBCkwamba licha ya watu zaidi kufahamu kuhusu jinsi ongezeko la joto duniani linavyoaathiri matukio ya yasiyo ya kawaida ya hali ya hewa, "bado kuna ukosefu wa uelewa kuhusu jinsi yanavyoweza kuathiri katika maeneo tofauti ."
Yeye na wenzake walielezea namna moshi mkubwa unavyoweza kusababisha saratani ya mapafu. Walielezea kisa cha aina hiyo, madaktari hawawezi kusema bila shaka kwamba sigara ilisababisha saratan, lakini wanaweza kusema kwamba uharibifu ulisababishwa na sigara.
Inafanya kazi vipi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbinu zilizotumiwa ni za miongozo ya kompyuta kufuatilia matukio . Ya kwanza ilichochea hali ya hewa kama tunayoishuhudia leo, likiwemo ongezeko la joto duniani linalosababishwa na binadamu.
Hii inamaanisha kutumia mfumo mazingira unaofanana na na hali sawa za hewa tena na tena, kutengeneza miaka mingi ya hali ya hewa katika hali ya sasa ya hewa.
Aina mpya ya majaribio iliondoa ushawishi wa hewa chafu, na kufananisha mazingira ya karibu na kile kilichokuwepo katika mapinduzi ya viwanda.
Halafu wanasayansi walihesabu idadi za matukio yasiyo ya kawaida ya hali ya hewa yanayojitokeza katika visa vyote – kwa ongezeko la joo duniani na bila ongezeko hilo
Kwa kufananisha idadi hizo, wanaweza kusema kwama iwapo tukio lilitokea mara tatu swa na tukio la kwanza, ongezeko la joto duniani lilionekana kuwa na uwezekano mara tatu wa kusababishwa na binadamu .
'Je mawimbi ya joto yote yanasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi '

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini kiuhalisia, kiwango ambacho matujio ya hali mbaya zaidi ya hewa yanaathiri mabadiliko ya tabia nchi kinatofautiana sana.
"Kwasababu ongezeko la joto duniani, mawimbi yote ya joto yanasababisha mabadiliko ya tabia nchi," anasema Dr Otto.
Matokeo ya hili, swahili muhimu la kuuliza wakati inakabiliwa na viwango vya joto la kupita kiasi ni : 'Je ni vipi ongezeko la joto dunia linayafanya kuwa mabaya zaidi au yasiyokuwa mabaya sana?'

Chanzo cha picha, Getty Images
Walielezea kwa mfano, ukame mara nyingi hutokea kwasbaabu ya sababu mbali mbali, ikiwa ni pamoja na uhaba wa mvua, kunyesha kwa kiwango cha chini cha mvua, viwango vya juu vya joto na mgongano wa hewa ya angani na ardhini.
Mafuriko, pia hutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na sababu ya mvua kubwa lakini pia kuna sababu nyingine zaidi zinazosababishwa na binadamu kama vile matumizi ya ardhi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hadithi ya Dr Otto inaelezea ushahidi ulioonekana wakati wimbi la joto kali lilipopiga mji wa Moscow mwaka 2010.
"Wakati huo, swali lilikuwa kuhusu iwapo hali ya hewa ya ongezeko la joto dunia ilikuwa na athari yoyote kwa joto hilo au jibu halikujibiwa’’
Mnamo mwaka 2012, alipata nyaraka mbili zilizoelezea kuhusu tukio.
Wakati ule, alikuwa akifanyia kazi miongozo ya hali ya hewa katika Chuo kikuu cha Oxford baada ya kusomea fizikia na kumaliza shahada ya udaktari katika falsafa.
"Niliamua kuandika waraka nikiunganisha mbinu mbili. Na kuanzia pale, nilichagua kuweka juhudi zaidi katika kitengo hiki."

Chanzo cha picha, Getty Images
"Tunapozungumzia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kwa kawida huwa tunazungumzia viwango vya joto na hiyo ni hatua ya kudhania ," anasema Dr Otto.
Dr Otto anaona mabadiliko ya tabia nchi kama tisho kubwa zaidikwa usawa na haki, na "mabadiliko ya hali ya hewa sasa yanajionyesha katika mfumo wa hali halisi," anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Dr Otto anatumi kuwa kikundi chake cha utafiti kitasaidia malengo kadhaa muhimu.
Wakati mwingine, kwa mfano, ripoti rasmi huwa zinaharakisha kusema majanga yanasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, wakati wataalamu wanaseama, ni muhimu kuepuka kusema kuwa viwango vya juu vya juu vya joto vyote vinasababishwa na mabadiliko yasiyo ya kawaida ya tabia nchi.
Watafiti wa hali ya hewa wanasema kwamba matokeo ya utafiti pia yanawza kutumiwa katika kahakama kama ushahiti ambao utasaidia kuwasukuma kuchukua hatua za kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi au hata kuoma fidia.
Zaidi ya hayo, inatumainiwa kuwa kadri sayansi iyakavyotueleza kuhusu hali inayoweza kuwa baadaye na kutuelezea hali mbaya za hewa na athari zake- hususan katika maeneo ambayo hayakuwahi kushuhudia mara kwa mara matukio mabaya ya hali ya hewa miaka ya nyuma - ndivyo tunavyoweza kuchukua hatua za mabadiliko ya tabia nchi kwa ubora zaidi.















