Mabadiliko ya tabia nchi: Jinsi upandaji miti unavyohifadhi mazingira
Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinajadiliwa kila kona ya dunia na maeneo mbalimbali duniani tayari yanaona athari na moja kwa moja.
Kwa mujibu wa shirika la WMO (World Meteorological Organization) Joto limeendelea kuongezeka duniani pamoja na kina cha bahari.
Huko visiwani Zanzibar jamii imeanza kupambana na athari hizo.
Mbarouk Omar kutoka shirika la Community Forest Pemba anatoa elimu ya mabadiliko hayo kila pembe ya visiwa vya Zanzibar.
Lakini kwanini anafanya shughuli hii?

