Maisha katika nyuzi joto 50: Moto wenye sumu unaochochea mabadiliko ya tabia nchi

Maelezo ya video, Maisha katika nyuzi joto 50: Moto wenye sumu unaochochea mabadiliko ya tabia nchi

Joy na familia yake ni miongoni mwa Wanigeria milioni mbili wanaoishi ndani ya kilo mita nne ya moto wa gesi unaowaka katika eneo la kusini lenye utajiri wa mafuta.

Alipokuwa mdogo Joy anakumbuka hali ya hewa nchini mwake haikuwa mbaya. Mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa na athari kubwa Nigeria. Ardhi zenye rotuba zinageuka kuwa jangwa , huku mafuriko yakiwa jambo la kawaidi eneo la kusini.

Kiwanda cha mafuta nchini humo kinafanya hali kuwa mabaya zaidi kwani – uchomaji wa gesi asilia ambayo hutolewa wakati mafuta inapochimbwa- ni jambo la kawaida licha ya kuwa inaenda kinyume cha sheria.