Mabadiliko ya tabia nchi yalivyotenganisha familia

Maelezo ya video, Mabadiliko ya tabia nchi yalivyoitenganisha fammila hii

Feroza anamlea mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka sita peke yake. Mume wake alikuwa mkulima lakini alilazimika kuondoka kwenda mjini kwani maji ya chumvi yaliharibu ardhi yao.

Wanaishi katika msitu mkubwa zaidi wa mikoko duniani - Sunderbans -- nchini India. Lakini maji yanaongezeka na visiwa vinazama, kwani vimbunga vinapiga mara kwa mara.