Mabadiliko ya tabia nchi: Njia sita tusizotarajia kuwa zinaweza kuokoa ulimwengu

Kujaribu kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa ndiyo changamoto kubwa zaidi kuwahi kumkumba mwanadamu.
Kwa bahati nzuri kuna watu wenye akili nyingi duniani wanaolishughulikia tatizo hili kwa kila njia, na unaweza kushangazwa na baadhi ya suluhu wamekuja nazo.
1. Kuwaelimisha wasichana

Chanzo cha picha, Amelia Flower @ameliaflower
Kuboresha elimu kote duniani linaonekana kama jambo lililo rahisi. Lakini kuwaelimisha zaidi wasichana haileti tu manufaa ya kijamii na kiuchumi bali pia husaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Hii ni kwa sababu wasichana huanza kupata watato baada ya muda wakati wako kwenye masomo. Iwapo wasichana wote watasoma hadi wahitimu shule ya upili, ifikapo mwaka 2050 watu duniani watapungua kwa milioni 840.
Ni kweli kwamba wakati suala la mabadiliko ya hali ya hewa linazungumziwa idadi ya watu pia huwa ni chanzo.
Kuwaelimisha wasichana ni zaidi ya suala la idadi ya watu duniani.
Wanawake wana uwezo wa kushiriki katika kazi, biashara na siasa, vitu ambavyo vinaweza kuwa siri ya kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa.
Utabiri unaonyesha kuwa kuweka wanawake zaidi katika usimamizi yaweza kuchangia kuwepo kwa sera bora kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa njia gani? Wanawake viongozi wana tabia ya kusikiliza ushauri wa kisayansi jinsi ilivyodhihirika wakati wa janga na corona.
2. Mianzi au Bamboo

Chanzo cha picha, Amelia Flower @ameliaflower
Muanzi ni mmea unaokuwa kwa haraka zaidi duniani. Unaweza kukua hadi mita moja kwa siku na unachukua gesi ya kaboni kwa haraka kuliko miti. Mianzi iliyoboreshwa pia inaweza kuwa yenye nguvu kuliko chuma.
Haya yote huufanya mmea huu kuwa bora katika kutengeneza fenicha na kwa ujenzi.
Kupanda mmea wa muanzi pia una manufaa mengine. Unastahimili wadudu na unaweza kuboresha ubora wa udongo, kuzuia mmomonyoko wa udongo na kupunguza hatari ya kutokea mafuriko.
Arief Rabik anasimamia wakfu wa muanzi nchini Indonesia, wenye lengo la kupunguza gesi ya kaboni kupitia vijiji 1000 vya mti huo.
Kila kijiji kitazungukwa na kilomita 20 mraba za msitu wa Bamboo, mimea ya chakula na mifugo. Anataka kupeleka wazo hilo katika nchi zingina tisa.
3. Kutumia sheria kupambana na wachafuzi

Chanzo cha picha, Rohan Dahotre @rohandahotre
Mawakili wa mazingira kwa wingi wanatumia sheria kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Sheria ndio moja ya silaha zenye nguvu zaidi kwa sasa kuwajibisha kampuni zinazochafua mazingira na hata serikali.
Hivi majuzi tu, mahakama nchini Uholanzi iliamua kuwa kampuni ya mafuta ya Shell itapunguza gesi chafu kuambatana na makubaliano ya hali ya hewa ya Paris - ushindi mkubwa.
Na sio tu sheria inayohusu mazingira inayoonekana kuokoa. Mawakili wamekuwa wabunifu, wanatumia sheria za haki za binadamu, za ajira na hata za kampuni kupambana na mabadliko ya hali ya hewa.
Mwaka 2020 kikundi cha wawekezaji kilicho na hisa za thamani ya dola 35 tu kilifanikiwa kuzuia kiwanda cha mkaa wa mawe kujengwa nchini Poland. Kwa njia gani? Kikundi hiki cha ClientEarth kilitumia hisa zake kwenye kampuni ya nishati nchini Paland Enea, kupinga uamuzi wa kampuni hiyo kujenga kiwanda cha mkaa wa mawe cha Ostroleka C.
Mahakama ikaamua kuwa kufungua kiwanda kipya cha mkaa wa mawe ilikuwa biashara mbaya iliyoku kinyume na sheria.
4. Kuwinda jokovu zenye gesi
Kila jokovu na kiyoyozi vina kemikali kwa mfano hydrofluorocarbons ( au HFCs).

Chanzo cha picha, Dandy Doodlez @dandydoodlez
Gesi hizi za HFCs ni chafu zaidi hata kuliko CO2, hadi kuchangia mwaka 2017 viongozi wa dunia wakakubaliana kuzimaliza.
Hatua hii pekee inakadiriwa kupunguza kuzia kuongezeka joto dunia kwa nyusi joto 0.5C.
Lakini idadi ya jokovu na viyoyozi vilivyo duniani bado na vingi
Kwa bahati nzuri kote duniani mafundi huwinda na kuharibu kemikali hizi.
5. Kufanya meli kuteleza zaidi

Chanzo cha picha, Kingsley Nebechi @kingsleynebechi
Wakati tunazungumzia biashara ya dunia, vitu kadhaa vinaweza kuwa kizingiti kikubwa. Sekta ya usafiri wa baharini ni muhimu kwa uchumi wa dunia - na asilimia 90 ya biashara ya dunia hupitia baharini, na sekta hii huchangia asilimia 2 ya gesi chafu huku idadi hii ikitarajiwa kuongezeka miongo inayokuja.
Kwa kuwa tunategema sana meli, kiumbe kidogo wa baharini kwa jina the barnacle anasababisha tatizo kubwa.
Meli zinazozuiwa na viumbe kama hawa hutumia asilimia 25 zaidi ya mafutaya diesel chafu ikilinganishwa na meli zinazoteleza.
Ili kupunguza gesi ya carbon inayosababishwa na viumbe hawa wa baharini, wataalamu wamebuni njia kuzifanya meli kuteleza zaidi.
Suala kuu hapa ni rahisi: kukinga ni bora kuliko kutibu - kupunguza kurundikana kwa viumbe wa baharini kabla kuwa kizuizi.
6. Kubuni mchele wa aina yake

Chanzo cha picha, Sarina Mantle @wildsuga
Je unafahamu kuwa kilimo cha mchele kinazalisha kiwango kikubwa cha gesi ya carbon. Mchele unazalisha carbon sawa na inayozalishwa kutoka sekta ya usafiri wa angani.
Hii ni kwa sababu asilimia kubwa ya mchele wetu hupandwa maeneo yanayofurika maji kuzuia kumea magugu.
Lakini maji haya huzuia oksijeni kufika kwenye udongo na kuchangia kuwepo mazingira bora kwa bakteria zinazozalisha gesi ya methane.
Methane ni gesi ambayo kwa kiwango cha kilo moja, inaweza kusababisha mara 25 kuongezeko joto duniani kuliko carbon dioxide.
Kuzuia hili wasayansi wanafanya mabadiliko katika kilimo cha mchele.
Wanaunda anaina tofauti za mchele zinozoweza kukua kwenye mashamba ya kawaida.
Kuna matumaini kuwa katika muda wa miaka kumi kutoka sasa, asilimia kubwa ya mchele wetu utapandwa katika mashamba ya kawaida yasiyofurika maji.













