Mabadiliko ya tabia nchi:'Tuko hapa kwa muda tu taifa letu litamezwa na bahari'

Chanzo cha picha, Min. de Relaciones Exteriores de Tuvalu
Hebu fikiri kwa muda kuhusu nyumba yako, asili yako, sehemu uliyoipenda zaidi katika dunia hii.
Na jinsi ilivyo vigumu hata kufikiria kwamba sehemu hii itatoweka kabisa kwenye uso wa dunia.
Kwa makumi kadhaa ya wakazi wa mataifa ya visiwa hofu hii ni halisi.
Kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari kunakotokana na mabadiliko ya tabia nchi tayari kunasababisha mmomonyoko wa ardhi na ukosefu wa maji ya kunywa katika visiwa hivi.
BBC imeangazia hali katika taifa dogo lililoko katika bahari ya Pacific, Tuvalu , ambalo limekuwa likizitaka nchi zinazochafua zaidi hali ya hewa kupunguza utoaji wa gesi chafu.
Nchi hii pia inajiandaa kukabiliana na hali mbaya zaidi : Kuzama kabisa kwa eneo lake lote.
Waziri wa sheria wa Tuvalu , mawasiliano na masuala ya kigeni, Simon Kofe, alituma ujumbe mzito kwa kikao cha mabadiliko ya tabia nchi- COP26, kikao kilichofanyika hivi karibuni katika mji wa Glasgow, Uskochi.
" Tunadidimia, lakini hali hiyo inatokea kwa kila mtu," alisema.
Kiwango cha maji, tisho lililopo
Tuvalu ina visiwa tisa na iko katika eneo la takriban kilomita 4,000 kutoka Australia na Hawaii. Majirani wa karibu zaidi ni Kiribati, Samoa na Fiji.
Nchi hii iko katika kilomita za mraba 26 ,ikiwa na idadi ya watu wapatao 12,000.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sawa na Kiribati na Maldives, miongoni mwa mengine, Tuvalu ni nchi iliyoundwa na visiwa vidogo vidogo, kwa hivyo hukabiliwa na hatari zaidi ya ongozeko la joto duniani "Kile ambacho tumekuwa tukikishuhudia kwa miaka mingi ni kwamba kwa kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari tunashuhudia mmomonyoko wa udongo wa sehemu ya kisiwa ." alisema Kofe.
MAP

Tuvalu imekuwa ikikabiliwa na upepo mkali na vipindi vya ukame, aliongeza waziri. Na viwango vya juu vya joto vimekausha mimea ya majini, ambayo ni muhimu kwa ulinzi wa mwambao na mazalio ya samaki.
Bahari na athari zake kwenye maji ya kunywa
Maji ya bahari yanapenya chini ya bahari katika baadhi ya maeneo na hii inaathiri chemichemi ya maji, Kofe anaeleza.
"Kwa kawaida huwa tunapata maji yatokanayo na mvua, lakini kwenye baadhi ya visiwa pia walikuwa wakichimba mashimo ya chemichemi kupata maji chini ardhini.
"Hilo haliwezekani kutokana na kupenya kwa maji ya bahari, kwa hiyo kimsingi tunategemea maji ya mvua tu."

Chanzo cha picha, Getty Images
Kupenya kwa maji ya bahari yenye chumvi pia kumeifanya mimea ya kilimo kuharibika.
Serikali ya Taiwan kwa sasa inafadhili na kuongoza mradi wa kuzalisha chakula kwa udhibiti wa hali ya mazingira nchini Tuvalu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mahangaiko ya nchi za visiwa.
Mataifa ya visiwa kama Tuvalu yamekuwa yakitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua kabambe za mabadiliko ya tabia nchi kwa zaidi ya miaka 30.
Mwaka 1990, nchi zilizoko katika bahari ya Pacific ziliunda muungano wa kidiplomasia kuanzia Caribbean, uliojumuisha nchi kama Antigua na Barbuda, na zile zilizoko katika bahari ya Hindi kama vile Maldives.
Lengo lilikuwa ni kubuni muungano kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Chanzo cha picha, Getty Images
. Wanasayansi wanasema nini?
Jopo la serikali mbali mbali la Umoja wa Mataifa la mabadiliko ya tabia nchi, IPCC lilielezea katika ripoti yake ya Agosti 9 mwaka huu kwamba viwango vya ongezeko la maji ya bahari duniani baina ya 1901 na 2018, kwasasa vimefikia milimita 3.7 kwa mwaka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hatahivyo, "hali ni mbaya zaidi katika kanda ya visiwa vilivyopo katia bahari ya Pacific, " Dkt Morgan Wairiu, mtaalamu wa mabadiliko ya tabia nchi na mratibu na kiongozi wa ukurasa kuhusu visiwa vidogo katika ripoti ya IPCC, aliimbia BBC kutoka visiwa vya Solomon.
" Katika Pacific Kusini wastani wa kupanda kwa viwango vya maji ya bahari ulikuwa ni kati ya milimita 5 hadi 11 katika kipindi cha kuanzia mwaka 1900 hadi mwaka 2018."

Chanzo cha picha, Getty Images
DKt Wairiu alisema kuwa shinikizo la maji katika visiwa vidogo vya Pacific litakuwa chini kwa 25% na ongezeko la nyuzijoto 1.5 ikilinganishwa na ongezeko la joto la nyuzijoto 2.
Wataalamu wanaelezea kwa ufupi hatari kuu kwa visiwa vidogo katika bahari ya Pacific:
Utafiti wa mwaka 2018 uliofanywa na wanasayansi nchini Marekani na Uholanzi, miongoni mwa wengine, ulibaini kuwa "nchi nyingi kati ya nchi za visiwa hazitakuwa zikikaliwa na watu kufikia kati kati ya karne hii ".
Sababu ni kwamba "viwango vya bahari vinavyopanda vitasababisha mafuriko''
Hali ya kisheria ambayo haikutarajiwa
Ikikabiliwa na hali halisi naya kutisha ya mabadiliko ya tabia nchi na ukosefu wa hatua zinazofaa za kidunia, Tuvalu inatafuta mbinu nyingine za upatikanaji wa suluhu kwa ajili ya hali yake ya baadaye.
"Hali mbaya zaidi ni ,bilashaka,kwamba tunalazimishwa kuhama na visiwa vyetu vinazama kabisa chini ya maji," Kofe aliiambia BBC.
"Na kulingana na sheria ya kimataifa, muda huu nchi inaweza kuwa na eneo lake la maji kama ina eneo la ardhi ambako mpaka huo unaweza kuchorwa."

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kanuni za kimataifa kwa sasa hazijali nchi kama yetu, kwasababu ni sehemu mpya kabisa sheria mpya ya kimataifa, hatujawahi kuona nchi iliyotoweka kutokana na mabadiliko ya tabia nchi."
Tuvalu kwa sasa inaangalia njia za kisheria inazoweza kuzifuata ili kukubalika kimataifa kwamba hata kama nchi itatoweka , iendelee kutambuliwa kama taifa na kuweza kupata raslimali zake za eneo lake la maji , alieleza Kofe.
Tofauti na Kiribati, Tuvalu ilinunua ardhi katika Fiji, ingawa Kofe alisema kwamba nchi yake " ilitoa tangazo kwa umma kwamba watatoa zawadi ya ardhi kwa Tuvalu kama tutadidimia baharini siku zijazo."
Waziri anapendelea kutofikiria kuhusu uwezekano wa kuhama.
"Hatujajua nchi ambayo tungependelea kuhamia, kwasababu pia tunaelewa kuwa kuhamakunaweza kutumiwa kama sababu na nchi kubwa zaidi ambao wanaweza kusema: 'tuliwapatia ardhi kuhama na tunaendelea na kazi yetu ya kutoa gesi chafu ". "Kuhama ni chaguo la mwisho."
Mapambano ya kisheria kwa ajili ya fidia
Tuvalu pia inataka kupata kitu fulani ambacho mataifa yaliyoendelea yanakitaja kwa sauti ya juu na nchi Tajiri zimekataa kukitoa: fidia kwa "uharibifu na hasara iliyosababishwa na maadiliko ya tabia nchi.
Pamoja na serikali ya Antigua na Barbuda, Tuvalu imesajili hivi karibuni kamati mpya na Umoja wa Mataifa.
"Mojawapo ya mawazo nyuma ya kuundwa kwa kamati hii ni kwamba kupitia kamati hii tunaweza kupata usaidizi wa Mahakama ya kimataifa ya sheria ya bahari na tunaweza kuiomba ushauri kwa ajili ya maagizo ya maoni kuhusu uharibufu na hasara ," Kofe alisema.
Mahakama ya kimataifa ya sheria za bahari, yenye makao Hamburg, Ujerumani, ina jukumu la kutatua mizozo inayohusiana na akubaliano ya Umoja wa mataifa ya mwaka 1982 kuhusu sheria za bahari.

Chanzo cha picha, Min. de Relaciones Exteriores de Tuvalu
Kamati mpya ya Tuvalu na Antigua na Barbuda itawaomba majaji juu ya iwapo wanaweza kudai fidia kutoka kwa nchi ambazo zimeifanya bahari kuwa ya joto kupitia uchafuzi wao, Payam Akhavan, wakili anayewakilisha nchi zote, aliwaambia waandishi wa habari.
Kama maoni ya mahakama yatafaa, nchi za visiwa zinaweza kuwasilisha madai ya kudai fidia mbele ya mahakama hiyo au mahakama nyinyine za kimataifa, aliongeza.
Mwaka 2009, nchi tajiri ziliahidi kuzipatia nchi zinazoendelea dola milioni 100 za Kimarekani kila mwaka kuanzia mwaka kuzisaidia katika kipindi cha mpito cha kupunguza chumi zinazotegemea hewa ya kaboni.
Hatahivyo wakati wa mkutano wa COP26, serikali ya Uingereza na mjumbe wa Marekani John Kerry kwa pamoja walisema lengo hilo linaweza kufikiwa tu katika mwaka 2023.
"Inasikitisha "
Katika ujumbe wake wa mwisho kwa mkutano wa COP26, Waziri mkuu wa Maldives ambaye pia ni waziri wa mazingira Aminath Shauna alisema kwamba tofauti baina ya "ongezeko la joto duniani la nyuzi joto 1.5 na nyuzi joto 2 kwetu sisi ni hukumu ya kifo."
Hata baada ya COP26, utafiti ulikadiria kuwa sayari dunia inakabiliwa na inaelekea katika janga la joto la walau nyuzi joto 2.4 kufikia mwishoni mwa karne hii.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa watu wa Tuvalu, uwezekano wa kuishia kuwa wakimbizi wa mabadiliko ya tabia nchi huongezeka kila mwaka wa kutochukuliwa hatua za dunia kudhibiti mabadiliko hayo.
"Inasikitisha na kushitua kwa kila mtu kuwa na wazo kwamba nyumba zaozinaweza kutoweka katika miaka michache ijayo. Wazo kwamba watoto wao na wajukuu huenda hawatakuwa na mahala pa kuishi." Anasema Simon Kofe.














