Mahusiano ya wazi ni nini na kwa nini yanaongezeka

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuwa na wenzi wa ziada wa kingono ukiwa katika ndoa kwa muda mrefu imekuwa mwiko. Na ingawa sio jambo la kawaida, sasa kuna shauku ya mahusiano ya aina hiyo kuwa wazi.
Dedeker Winston amekuwa katika mahusiano ya zaidi ya mke mmoja kwa zaidi ya muongo mmoja, lakini hajawahi kuona shauku kubwa kama ile iliyopo katika mahusiano ya wazi.
Suala hili limekuwa mwiko katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na Marekani, ambako Winston anaishi.
Sarah Levinson, mshauri ambaye anajishughulisha na masuala ya kujamiiana na mienendo ya uhusiano huko New York, pia amegundua shauku inayoongezeka katika mahusiano ya wazi ndani ya muongo mmoja uliopita. "Ilikuwa haijulikani sana miaka 10 iliyopita, lakini sasa ni jambo la kawaida sana," anasema.
Mahusiano ya wazi ni nini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mahusiano ya wazi mara nyingi huhusishwa na watu wanaojihusisha kimsingi na mahusiano ya kimapenzi nje ya ushirikiano wao wa watu wawili, uliopewa kipaumbele.
Kwa ufupi mahusiano ya wazi yanalenga zaidi juu ya ngono badala ya uhusiano wa kihisia na watu walio nje ya uhusiano wa kimsingi.
Kwa wengine, hii inamaanisha kwenda kujivinjari na watu wengine wasiokuwa wapenzi wao wa kimsingi. Uhusiano wa aina ni wa 'marafiki-wanaofaana'.
Kwa wengine, uhusiano wa wazi unamaanisha kukutana mara kwa mara lakini kwa muda mfupi na lengo ni kujamiana.
Na kwa wengine, mpangilio huu unaweza kuwa zaidi ya kufanya ngono na watu walio kwenye ndoa, lakini si kwenda kujivinjari.
Winston pia anataja kitu kinaitwa "usiulize, usiniambie" -mahusiano ya wazi, ambayo wanandoa wote wanaruhusu mwingine kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wengine – lakini hawataki tu kujadili matukio hayo pamoja.
Kuwa na shauku
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mitindo ya programu ya uchumba husaidia kuangazia kuongezeka kwa hamu ya uhusiano wazi.Kwanza, kumekuwa na kuibuka kwa majukwaa yanayolenga mada ya kutokuwa na mke mmoja, ikiwa ni pamoja na mahusiano ya wazi, ili kuhudumia wateja wanaoongezeka.
Lakini hata programu za kitamaduni za kuchumbiana kama vile OkCupid, zimeshuhudia ongezeko la maslahi katika mahusiano ya wazi.
"Wakati wengi wa wachumba wa OkCupid wanatafuta uhusiano wa kuwa na mke mmoja, mnamo 2021, watumiaji wanaotafuta uhusiano wa wasio na mke mmoja waliongezeka kwa 7%," mwakilishi wa OkCupid aliiambia BBC Worklife.
Zaidi ya hayo, data ya 2022 kutoka kwa programu ya kuchumbiana inayofahamika kama Hinge ilionyesha mtumiaji mmoja kati ya watano wa programu hiyo "angezingatia" kujaribu uhusiano wazi, wakati mmoja kati ya 10 tayari amejihusisha na mmoja.
Mkurugenzi wa sayansi ya uhusiano wa Hinge Logan Ury anasema huenda ongezeko hilo limechangiwa na athari za janga, kwani anaamini ilikuwa "fursa nzuri ya kutulia na kutafakari zaidi juu ya kile tunachotaka."
Miongoni mwa zaidi ya watumiaji milioni 1 wa OkCupid wanaoishi Uingereza waliojibu swali, ‘Je, ungependa kuwa na uhusiano wazi?’ katika programu, asilimia 31 walisema ndiyo mwaka wa 2022, ikilinganishwa na 29% mwaka wa 2021 na 26% mwaka wa 2020.

Chanzo cha picha, Getty Images
Washauri na wataalamu ikiwa ni pamoja na Levinson na Winston pia wameshuhudia ongezeko la wateja wanaotafuta ushauri kuhusu uhusiano wa wazi katika pita pita zao za kazi.
Winston anasema kwamba vijana wa kizazi cha milenia wanavutiwa sana na uhusiano wa wazi na "wanahoji tu jinsi walivyolelewa" - mara nyingi, kuamini kwamba ndoa ya muda mrefu, ndoa ya mke mmoja ni lengo la mwisho la mahusiano ya karibu.
Wenzao wanaojiita Generatin Z wamepatia uhusiano wa wazi jila la Situationship.
Huu ni uhusiano usio rasmi kati ya watu wawili na kuna vipengele vya mawasiliano ya kihisia na kimwili.
Lakini inafanya kazi nje ya dhana ya kawaida ya kuwa katika uhusiano rasmi na wa pekee wa kimapenzi.
Katika baadhi ya matukio, 'Situationship' ni mpangilio wa kawaida unaofaa kwa hali ya sasa.
Kwa mfano, hii inaweza kutumika kwa wanafunzi wawili wa mwaka wa mwisho wa chuo kikuu ambao hawataki kuendelea na uhusiano imara wa kimapenzi kwa sababu kazi mpya baada ya kuhitimu zinaweza kuwapeleka kwenye miji mipya.
''Situationship' ni maarufu kwa sababu inapinga 'vichochezi vya uhusiano," anasema Elizabeth Armstrong, Profesa wa sosholojia katika Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani ambaye anatafiti jinsia na uhusiano.
Uhusiano wa kimapenzi unapaswa kuwa safari ya moja kwa moja yenye malengo ambayo yanavuka hatua muhimu za uhusiano kama vile kuishi pamoja, uchumba na ndoa.















