Kifo cha Shinzo Abe: Polisi wa Japan walikosea wapi?

Chanzo cha picha, Reuters
Polisi wa Japan wanafanya kazi usiku na mchana kuchunguza mauaji ya Waziri Mkuu wa zamani Shinzo Abe.
Polisi sasa wamekiri kuwa kulikuwa na dosari katika upande wa usalama alilopewa Shinzo Abe.
Siku ya Ijumaa, Abe alipigwa risasi na mtu mwenye bunduki wakati wa kampeni za uchaguzi katika mji wa kusini wa Nara. Tukio hili limeshtua Japan nzima.
Mkuu wa Polisi wa Nara Tomoyaki Onizuka alisema, "Hatuwezi kukataa kwamba kulikuwa na tatizo fulani na usalama wa Abe."
Polisi wanasema mshukiwa aliyekamatwa kwa mauaji, Tetsuya Yamagimi (umri wa miaka 41), ana chuki na "shirika maalum".
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Japan vinavyonukuu vyanzo vinavyohusiana na uchunguzi huo, Yamagimi anaamini kuwa Kiabe alihusishwa na kundi la kidini lililomfilisi mama yake.
Polisi inafanya uchunguzi wa kina wa kifo cha Abe

Chanzo cha picha, Reuters
Mshukiwa amekiri kwamba alimfyatulia risasi Abe kwa bastola iliyotengenezwa nchini. Hata hivyo, Mkuu wa Polisi Onizuka anasema, “Jambo muhimu kwetu kwa wakati huu ni kuchunguza kwa kina na kujua nini kilitokea?
Yamagimi aliwaambia polisi kwamba mshtakiwa alikuwa amehudumu katika Jeshi la Wanamaji la Japan na Jeshi la Kujilinda kwa miaka mitatu. Kando na hayo, pia alifanya kazi katika kiwanda kimoja magharibi mwa Japani.
Abe alikuwa waziri mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi nchini Japani. Wakati alipopigwa risasi, alikuwa akijishughulisha na kampeni za uchaguzi za LDP kwa ajili ya uchaguzi wa baraza la juu la Bunge.
Waziri Mkuu wa sasa Fumio Kishida pia ndiye kiongozi wa LDP. Alisema kuwa alishtushwa na mauaji haya. Alisema kuwa hakuna utamaduni wa bunduki nchini Japani hata kidogo. Silaha hizo zimepigwa marufuku hapa. Na pia matukio ya vurugu za kisiasa hutokea mara chache.

Chanzo cha picha, Reuters
Waliohusika na mauaji ni kundi ama mtu binafsi?
Polisi wanachunguza kwa nini Abe ameuawa. Ni mtu mmoja tu aliyehusika katika njama hiyo ya kumuua au watu wengine pia wanahusika nayo.
Bastola iliyotumika kumuua Abe ilionekana kama ilitengenezwa nyumbani. Ilitengenezwa kwa mbao na chuma na ilikuwa imefungwa kwa mkanda mzito wa mweusi.
Baadaye, bastola na mabomu kadhaa yaliyotengenezwa nchini yalipatikana katika makazi ama nyumba ya mshtakiwa. Abe aliumia shingoni na mwili wake ulikuwa ukivuja damu nyingi.
Alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali. Inasemekana alikuwa na fahamu kwa dakika chache baada ya shambulio hilo. Lakini wakati anapelekwa hospitalini, alifariki. Alitangazwa kufariki saa 5:03 asubuhi kwa saa za huko.
Kabla ya hili, madaktari walijaribu sana kwa saa nyingi kumwokoa. Baada ya kushambuliwa siku ya Ijumaa, "Tunataka Demokrasia, Sio Vurugu" ujumbe huu ulisambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Japan. Watu waliogopa sana na kushtushwa na tukio hili.

Chanzo cha picha, Reuters
Hakuna utamaduni wa bunduki Japan, wengi washangazwa
Mwaka 2014, kulikuwa na visa sita pekee vya unyanyasaji wa bunduki nchini Japani. Ambapo katika mwaka huo huo watu 33,599 waliuawa Marekani kutokana na ghasia za bunduki.
Watu wanaonunua bunduki nchini Japani wanapaswa kufaulu mtihani mgumu pamoja na vipimo vya afya ya akili. Abe alikua waziri mkuu kwa mara ya kwanza mwaka 2006. Kisha akawa Waziri Mkuu kuanzia 2012 hadi 2020. Baada ya hayo, aliacha wadhifa huo akitaja sababu za kiafya.

Chanzo cha picha, Reuters
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aliandika katika salamu zake za rambirambi, "Uhusiano wangu na Shinzo Abe unatokea mbali. Nilimfahamu wakati wa uongozi wangu kama Waziri Mkuu wa Gujarat na urafiki wetu uliendelea hata baada ya kuwa Waziri Mkuu. Uelewa wake juu ya uchumi na mambo ya kimataifa yalinigusa sana."
Abe alikuwa mkali kwenye mambo ya nje na usalama

Chanzo cha picha, Reuters
Akiwa waziri mkuu, alichukua msimamo mkali kuhusu ulinzi na mambo ya nje. Baada ya Vita ya pili ya dunia, alitaka kufanyikika kwa marekebisho katika katiba kulinda masuala ya amani.
Sera yake ya uchumi iliyopata umaarufu inaitwa Abenomics. Hii ni pamoja na kupunguzwa kwa kiwango cha riba, vichocheo vya mzunguko wa fedha kwenye uchumi na marekebisho ya kimuundo.














