Tanuri na mifupa ya binadamu - BBC yatembelea eneo la 'maangamizi' Mexico

Chanzo cha picha, Getty Images
Milango ya shamba la Izaguirre inaonekana kama mingine yoyote unayoweza kukutana nayo.
Lakini kilicho nyuma ya milango hiyo ya chuma mieusi inadaiwa kuwa ni ushahidi wa vurugu mbaya zaidi za magendo ya dawa za kulevya nchini Mexico katika siku za hivi karibuni.
Kufuatia taarifa kuhusu eneo linalowezekana kuwa kaburi la halaiki, kikundi cha wanaharakati cha jamaa za baadhi ya maelfu ya watu waliotoweka nchini Mexico walikwenda kwenye shamba hilo, wakitarajia kupata dalili za wapendwa wao waliopotea.
Walichokutana nacho kilikuwa kibaya zaidi: jozi 200 za viatu, mamia ya nguo, masanduku mengi na magunia, yalitupwa baada ya wamiliki wenyewe inaoaminika waliuawa.
Chakusikitisha zaidi, tanuri kadhaa na vipande vya mifupa ya binadamu vilipatikana kwenye shamba hilo.
Eneo hilo lilitumiwa, wanaharakati hao wanadai, na kundi la New Generation Jalisco Cartel (CJNG) kwa ajili ya kusajili na kuwafunza washirika wao, na kuwatesa waathiriwa na kuchoma miili yao.
"Kulikuwa na vinyago vya watoto mle ndani," anasema Luz Toscano, mwanachama wa Buscadores Guerreros de Jalisco Collective.

"Watu walikuwa wamekata tamaa," anakumbuka.
"Waliona viatu na kusema: 'Hivi vinafanana na vile ambavyo jamaa yangu aliyepotea alikuwa amevaa'."
Toscano anaamini kuwa mamlaka lazima sasa ipitie vitu hivyo kimoja baada ya kingine na vikabidhiwe familia wa karibu ili kukaguliwa.
Kwa wengi, hata hivyo, sehemu mbaya zaidi ya ugunduzi huo wa kutisha ni kwamba polisi wa eneo hilo walivamia shamba hilo, karibu na kijiji cha Teuchitlán, hivi majuzi kama Septemba iliyopita.
Wakati huo waliwakamata watu 10 na kuwaachilia mateka wawili, ama hawakupata au hawakufichua ushahidi wowote wa ukubwa wa ghasia zilizotekelezwa huko.
Wakati bado raia wanasubiri kuona ikiwa kuna hatua iliyochukuliwa na mamlaka ya manispaa na serikali baada ya operesheni ya mwaka jana, wakosoaji na familia za waathiriwa zinawashutumu waziwazi kwa kushirikiana na makundi la magenge ya dawa za kulevya katika eneo la Jalisco.
Gavana wa Jimbo hilo Pablo Lemus alijibu katika ujumbe wa video.
Utawala wake ulikuwa ukishirikiana kikamilifu na mamlaka ya shirikisho, alisema, na kusisitiza kwamba "hakuna mtu yeyote katika eneo la Jalisco anayekubali kusema neno" juu ya kesi hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum, matukio ya Jalisco yanatishia kutia doa mwanzo mzuri wa urais wake.
Kwa kuzingatia mashaka makubwa juu ya hatua za polisi wa eneo hilo na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, ameamuru wachunguzi wa shirikisho kuchukua jukumu la kesi hiyo.
Aliwataka watu kutokurupuka kufikia maamuzi wakati uchunguzi ukiendelea.
"Ni muhimu kufanya uchunguzi kabla hatujafikia hitimisho lolote," alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari mapema wiki hii.
"Walipata nini kwenye eneo? Kabla ya jambo lolote, lazima tusikie kutoka kwa ofisi ya mwanasheria mkuu, ofisi ambayo itafahamisha nchi nzima walichopata."
Ikiwa watu wengi wa Mexico wataamini taarifa rasmi za tukio lenyewe, hilo ni swali lingine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mahali hapa sasa pana maafisa wa polisi, wachunguzi wa serikali kuu na timu za wachunguzi waliovalia ovaroli.
Vyovyote watakavyohitimisha, hata hivyo, vyombo vya habari nchini Mexico vinaita shamba la Izaguirre kuwa eneo la "maangamizi".
Wakati huo huo, jamaa za wanaotafuta wapendwa wao zimefika katika mji mkuu wa jimbo, Guadalajara, kabla ya maandamano ya wikendi hii kuwataka viongozi kuchukua hatua zaidi kutafuta watu waliopotea Mexico.
Rosario Magaña alikuwa miongoni mwao. Yeye ni mama ya Carlos Amador Magaña, ambaye alitoweka Juni 2017. Alikuwa na umri wa miaka 19 pekee.

"Bado najihisi mwenye kukata tamaa, hadi kufikia sasa ni miaka minane na bado niko katika hali hiyo hiyo", alisema - akizungumzia utafutaji wake usio na kikomo wa mwanawe ambaye alitekwa nyara pamoja na rafiki yake wa karibu.
"Ni mchakato wa polepole sana linapokuja suala la ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na uchunguzi."
"Bado nina imani na matumaini ya kumpata", alisisitiza. "Lakini niko katika hali ambayo haisongi mbele, na inakatisha tamaa."
Alipotoka kwenye ibada ya waathiriwa wasiojulikana katika shamba la Teuchitlán, Rosario alisema madai ya makosa, uangalizi, kula njama na uzembe katika kesi hiyo yalisisitiza tu magumu ambayo akina mama kama yeye wamekumbana nayo kwa miaka mingi katika kupata majibu ya maswali ya msingi kuhusu waliko watoto wao.
"Kuna makaburi mengi sana ya halaiki huko Jalisco, hifadhi nyingi sana magenge ya dawa za kulevya.











