Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi kubwa 5 za soka Jioni hii: Alsonso kumrithi Ancelotti Madrid
Xabi Alonso anatarajiwa kutua Real Madrid baada ya kutangaza kuondoka kwake Bayer Leverkusen. Mafanikio yake akiwa na Leverkusen yamezua ripoti kwamba atamrithi Carlo Ancelotti huko Real Madrid, huku Muitaliano huyo akitarajiwa kuondoka Santiago Bernabeu msimu huu wa joto. Alonso ameongeza uvumi huo baada ya kuwaambia wanahabari kuwa ataondoka Leverkusen hivi karibuni.
Rashford kutua Barcelona
Licha ya Aston Villa kutamani kumsajili kwa uhamisho wa kudumu kutokana na kiwango bora ambacho Marcus Rashford ameonyesha tangu ajiunge nao akitokea Manchester United mwezi Januari, inaripotiwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England anapania uhamisho kuelekea Barcelona, ambao wanaendelea kumfuatilia kwa nia ya kumsajili mwishoni mwa msimu (transfermarket.com).
Man United yapata mbadala wa Onana
Manchester United imeanzisha mazungumzo na kipa wa Torino, Vanja Milinkovic-Savic, kama mmoja wa wanaoweza kumrithi Andre Onana, hatua ambayo inaripotiwa kuingiza klabu ya Italia hiyo kwenye "hofu" huku Mashetani Wekundu wakitafuta suluhu kwenye nafasi ya golikipa (Goal.com).
Newcastle United yasaka mbadala wa Isak
Newcastle wametuma maskauti kumtazama mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko, ili kutafuta wanaoweza kumrithi Alexander Isak. Iwapo Isak atasalia, Newcastle wanafuatilia hali za Matheus Cunha, Bryan Mbeumo na Liam Delap ili kumsaidia msimu ujao (Skysport).
Ruud van Nistelrooy kuondoka Leicester
Ruud van Nistelrooy ametoa ishara kubwa zaidi kwamba mustakabali wake unaweza kuwa nje ya Leicester baada ya kuahidi "kuiacha klabu katika nafasi bora iwezekanavyo".
Alisema: "Wajibu wa meneja ni kwamba unafanya kazi na unafanya kila uwezalo kwa manufaa ya klabu ya soka.
"Hiyo ndio njia ninayoifanya. Hicho ndicho mashabiki wanaweza kutegemea, kwamba ninafanya hivyo.
"Kwa hivyo kazi ya kila siku ni, bila shaka, kuendeleza na kufanya vizuri kwa muda mfupi, lakini pia kufanya kila niwezalo kuacha klabu katika nafasi bora iwezekanavyo." (Skysport)