Vita vya Ukraine: Kutana na ndugu wanaotengeneza 'droni' zinazoisumbua Urusi vitani

Mzozo wa Ukraine ulianza na ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB2 zilichukua jukumu muhimu katika kusitisha kusonga mbele kwa Urusi.
Lakini sasa, inaonekana kwamba Urusi ina mkono wa juu na matumizi yake ya ndege zisizo na rubani za Shahed-136 zilizotengenezwa na Iran zinazoitwa 'kamikaze' ambazo hulipuka kwa athari.
Kwa mtaalam wa droni Sarah Kreps, hii yote ni sehemu ya vita kama mchakato wa mageuzi.
"Kulikuwa na hisia za mapema kwamba ndege zisizo na rubani zingeamua," profesa wa Chuo Kikuu cha Cornell anasema.

Neno 'kibadilisha mchezo' lilitumiwa kwanza kuhusu ndege isiyo na rubani ya Bayraktar TB2.
Inagharimu takriban $2m na ni saizi ya ndege ndogo yenye makombora ya kukabiliana na silaha yanayoongozwa na laser.
Lakini kwa ndugu hawa Kituruki Selcuk na Haluk Bayraktar ambao ndio wazalishaji wa ndege hizi, vita wakati mwingine haikwepeki.
"Bila shaka, vita ni jambo chungu sana, ni jambo chungu," anasema kaka mkubwa zaidi Haluk katika ofisi yake ambapo kumejaa midoli ya ndege zisizo na rubani za TB2 zenye nembo ya Ukraine.
"Watu wanakufa, na matamanio yangu tusingetengeneza ndege hizi zisizo na rubani.
"Unapokuwa chini ya shambulio kubwa kama hilo, unahitaji kujilinda na unaweza kufanya hivi tu kwa bidhaa kama hizo za kiteknolojia."
'Bingwa wa taifa'
Kwa nje, kampuni inayomilikiwa na familia nje kidogo ya Istanbul inaonekana kama chuo kikuu au kampuni ya teknolojia.
Watu walio na umri wa miaka 20 hivi waliovalia jeans hutembea kuzunguka eneo kubwa lililotunzwa vizuri kwa mpango.
Na katika mapokezi, vitabu kuhusu historia ya himaya ya Ottoman na namna ya kuswali kwa usahihi kiislamu vimerundikwa juu ya meza.
Kampuni ya Baykar si kampuni kubwa ya ulinzi nchini Uturuki lakini ni moja ya makampuni maarufu na muhimu zaidi.

Chanzo cha picha, Ukrainian Presidential Press Service
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ndege za aina hii zisizo na rubani zilisaidia Azabajani kuvishinda vikosi vya kijeshi vya Armenia na kunyakua ardhi kubwa katika eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh mnamo 2020.
Hapo ndipo walipoanza kupata kutambulika zaidi nje ya Uturuki. "Nguvu yake marasufu ilionekaa huko Karabakh, ilionekana katika mapambano ya Uturuki dhidi ya ugaidi, pia katika operesheni nchini Syria, na katika kuunda ukanda wa usalama huko Libya," anasema Haluk.
Kampuni hiyo ina uhusiano wa karibu na jeshi la Uturuki ambao walikuwa wanunuzi wa kwanza wa ndege zisizo na rubani.
Jeshi limetumia ndege hizo zisizo na rubani kuwalenga wanamgambo wa Kikurdi ndani na nje ya nchi. Ndugu wanathibitisha kuwa wanasambaza teknolojia hiyo kwa nchi takribani 24.
Hii inahusiana na maono ya Rais Erdogan ya kuifanya Uturuki kuwa muuzaji mkuu wa ndege zisizo na rubani kote Mashariki ya Kati na Afrika na pia katika nchi za Asia ya Kati.
Ninamuuliza Haluk ikiwa kampuni yake inaweka masharti yoyote juu ya matumizi ya ndege zisizo na rubani, kama vile kudhuru raia.
Anasema mamlaka ya Uturuki ilitoa leseni ya kuuza nje na kuweka sheria ikiwa ni pamoja na kwamba teknolojia hiyo haiwezi kutumika kinyume na haki za binadamu.
"Baykar inashirikiana na mamlaka za serikali husiak," anaongeza. "Teknolojia kama hizo zinauzwa kwa taasisi za serikali za nchi. Haziuzwi kwa taasisi za kiraia."
Haziuzwi
Uhusiano wa kampuni hiyo na Ukraine ni wa muda mrefu. Haluk anasema kandarasi ilitiwa saini mnamo 2018 na walianza kusambaza ndege zisizo na rubani mnamo 2019.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kyiv alizifuata nchi nyingi kwa ajili ya kupata ndege zisizo na rubani (drones), anaongeza, lakini ni Uturuki pekee iliyokubali kusambaza ndege hizo.
Ninamuuliza Urusi imepokeaje kwakuwa Moscow pia ni mshirika mkuu wa kimkakati wa Uturuki. Jibu la kwanza la Haluk ni kusema kwamba wao wanaunga mkono Ukraine.
"Vipi kama Moscow ingekupa pesa nyingi? Je, ungewauzia ndege zisizo na rubani pia?" Nauliza. "Pesa sio jambo muhimu zaidi. Pesa na bidhaa hazikuwa msingi wa biashara yetu," anasema Haluk.
"Haijalishi ni kiasi gani cha pesa kinachotolewa kwetu, jambo kama hilo halina mjadala. Msaada wetu wote unaipendelea Ukraine."
Kuna shinikizo toka kwa Putin?

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais Erdogan wa Uturuki alidaiwa kukiambia kikao cha juu cha chama kuwa Rais Putin anataka kupata ndege hizo zisizo na rubani. Haluk alishauriwa na ofisi yake ya wanahabari kutotumia jina la 'Putin' katika mahojiano bali azungumzie tu 'Urusi'.
Ndugu yake mdogo Selcuk, Afisa Mkuu, alikataa kutoa maoni. Ni wazi kutokana na maneno ya Haluk kwamba hakutakuwa na ushirikiano na Urusi kwenye ndege zisizo na rubani, angalau kwa muda wote wa uvamizi wao nchini Ukraine.
Lakini wachambuzi wengi wa nchi za Magharibi wanaishutumu Uturuki kwa kujaribu kuwa ndumilakuwili kwenye mzozo wa Ukraine na Urusi. Kwa upande mmoja, inauza ndege za kijeshi zisizo na rubani kwa Ukraine lakini kwa upande mwingine, inakataa kuunga mkono vikwazo vya Magharibi kwa Urusi. Na kuna zaidi ya biashara hatarini.














