Mvutano Ukraine: Marekani yajitetea uamuzi wake wa kuhamisha ubalozi

Ukrainian civilians take part in military training in Kyiv

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ukraine kushiriki katika mafunzo ya kijeshi kwa raia katika Kyiv

Waziri wa mambo ya nje nchini Marekani Antony Blinken amesema tishio la hivi karibuni "la hatua ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine inahalalisha uamuzi wa kuhamisha ubalozi wa Marekani mjini Kyiv.

Alizungumza hayo baada ya rais wa Ukraine kuhimiza utulivu, akisema adui mkubwa ni hofu.

Zaidi ya nchi kumi na mbili zimewahimiza raia wao kuondoka Ukraine.

Moscow, ikiwa na zaidi ya wanajeshi 100,000 karibu na mpaka, imekanusha kuwa ina mpango wa kuvamia.

Mshauri mkuu wa sera za mambo ya nje wa Kremlin Yuri Ushakov amepuuzia mbali onyo la Marekani kuhusu shambulio hilo.

Jumamosi nilishuhudia majaribio zaidi ya kupunguza mvutano katika eneo hilo.

Katika mazungumzo ya simu, Rais Joe Biden alimuonya kiongozi wa Urusi Vladimir Putin "kuhusu gharama za haraka na kali" ikiwa Urusi itatuma wanajeshi.

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace, wakati huohuo, alilinganisha juhudi za hivi karibuni kidiplomasia za Magharibi kukomesha uvamizi na kuwatuliza Ujerumani.

Bw Wallace aliliambia gazeti la Sunday Times "kuna mlio wa Munich angani" - akirejea makubaliano na Hitler ambayo yalishindwa kuzuia Vita vya Pili vya Dunia.

Bw Wallace pia alisema kuwa shambulio kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa shambulio kutokea na linaweza kuja "wakati wowote".

'Jambo la busara kufanya'

Uingereza, Marekani na Ujerumani ni miongoni mwa nchi kadhaa ambazo zimewataka raia wao kuondoka nchini Ukraine mara moja.

Uamuzi wa Marekani wa kuwahamisha wafanyakazi wengi wa ubalozi wake mjini Kyiv siku ya Jumamosi ulifuatiwa na hatua kama hizo za Canada na Australia.

Mataifa yote matatu badala yake yamehamishia operesheni katika mji wa magharibi wa Lviv, karibu na mpaka wa Poland - ingawa balozi wa Uingereza amesema atakaa katika mji mkuu wa Ukraine na timu kuu.

Bw Blinken alisema hatari ya kuchukua hatua za kijeshi "ni kubwa vya kutosha na tishio liko karibu vya kutosha" kwamba kuhamishwa ni "jambo la busara kufanya".

Lakini hapo awali Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alihimiza utulivu, akisema: "Kwa sasa, adui mkubwa wa watu ni hofu."

Bw Zelensky alisema kuwa ikiwa mataifa ya Magharibi yangekuwa na ushahidi dhabiti wa uvamizi unaokuja, bado hajauona.

Mwandishi wa BBC Zhanna Bezpiatchuk anasema hakuna dalili kubwa za hofu katika mji wa Kyiv au miji mingine mikuu ya Ukraine.

Lakini, aliongeza kuwa Ukraine wanaanza kuchukua tishio kutoka kwa Urusi kwa umakini na wanachukua hatua zao za dharura.

Mpango wa uokoaji wa dharura kwa wakazi milioni tatu wa Kyiv umeandaliwa na ofisi ya meya wa mji mkuu kama tahadhari.

m

Ikulu ya White House imeonya kuwa uvamizi unaweza kutokea wakati wowote, na unaweza kuanza kwa mlipuko wa mabomu kutoka angani.

1px transparent line

Mvutano umezidi kuongezeka huku Urusi ikiendelea kupeleka wanajeshi kwenye mpaka wa mashariki mwa Ukraine.

Pia imekuwa ikifanya mazoezi yake makubwa zaidi ya kijeshi kwa miaka mingi katika black sea, huku Ukraine ikiishutumu nchi hiyo kwa kuizuia kuingia baharini.

Mgogoro huo unakuja miaka minane baada ya Urusi kutwaa rasi ya Crimea kusini mwa Ukraine.

Tangu wakati huo, jeshi la Ukraine limeingia katika vita na waasi wanaoungwa mkono na Urusi katika maeneo ya mashariki karibu na mipaka ya Urusi.

Kremlin inasema haiwezi kukubali kwamba Ukraine - Jamhuri ya zamani ya Soviet yenye uhusiano wa kina wa kijamii na kitamaduni na Urusi - siku moja inaweza kujiunga na muungano wa kujihami wa Magharibi Nato, na imedai kwamba hii ikataliwa.

Marekani imekataa hilo, ikisema kuwa kama taifa huru Ukraine inapaswa kuwa huru kuamua ushirikiano yake ya usalama.