Nitajuaje kama ninasumbuliwa na hofu ya kuwa mbali na simu yangu?

Chanzo cha picha, Getty Images
Nitafahamu vipi kama nasumbuliwa na "Nomophobia", hali inayonifanya kuogopa kukaa mbali na simu yangu au kutumia mitandao mfano WhatsApp?
Miaka ya hivi karibuni , matumizi ya simu za mkononi yameendelea kukua kwa kasi zaidi, hasa vifaa janja.
Yamekuwa kama maisha mapya kwa watu wengi hauwezi kwenda mahali bila kuwa nayo.
Lakini, matumizi ya muda mrefu ya vifaa hivyo vya mawasiliano yanaweza kukusababisha kuwa na utegemezi na uraibu ambao baadae unaweza kukujengea hofu.
Nomophobia ( non-mobile-phone-phobia ) inaweza kueleweka kwa urahisi kama uoga uliopitiliza unaosababishwa na matumizi ya simu, mtu anapokuwa hajatumia kwa muda kidogo kifaa hicho cha mawasiliano anaingiwa na unyonge na kusababisha kuwa na uoga hata kuleta matatizo ya moyo.
Ni nini kisababishi cha hali hiyo ya hofu?
Kwasasa, utafiti uliofanywa unaonesha kuwa uoga unasababishwa na mambo makuu manne, kutokuwa na uwezo wa kuwasiliana na wengine au uwezo hafifu wa kupata taarifa.
Mfano,tabia zinazoletwa na Nomophobia, mtu anaweza kusahau simu yake nyumbani ila akiwa njiani anakumbuka kuwa ameisahau hapo ndipo anapokuwa na hofu kuu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ikiwa sababu kuu hasa ni hautokuwa na uwezo wa kuwasiliana na watu wengine ni vyema sasa kuangalia kama tabia hii inakutokea sanjari na hali hii ya nomophobia.
Vilevile hali hii inaweza kukutokea pale unapopata ujumbe mwingi kupitia kwenye tovuti ulizopakua kwenye kifaa chako cha mawasiliano.Ukiachana na utegemezi, nomophobia inasababisha zaidi hofu kuu, ambayo pia inaweza kusababisha matatizo makubwa kwenye maisha ya mtu, hasa pale anapokuwa hana uwezo wa kutumia simu.
Kuna tafiti kadhaa zimefanyika na kuonesha makundi yanayoathirika zaidi, (Wanafunzi hasa wa vyuo vikuu, walimu, manesi, waganga, n.k.) wanasumbuliwa zaidi na hili tatizo.
Imeonesha kuwa nomophobia imekuwa na matokeo hasi kwenye maisha ya mtu, kujiona haufai, hofu, kushuka kiwango cha elimu na hata kupata sonona.
Hata kupata matatizo ya afya ya akili na mwili kudhooofu pia.
Ni kina nani hasa wanaopata nomophobia?
Kuna makundi kadhaa ambayo ndio huathirika zaidi na nomophobia imeweza kuelezwa kupitia tafiti kadhaa zilizofanyika.
Mojawapo ikiwa, mtu mwenyewe ndio kisababishi, shauku na hamu inayojijenga pamoja na saa anazotumia mtu anapotumia vifaa hivyo vya mawasiliano.
Kwa upande mwingine, umri nao ni kisababishi kimojawapo, mtindo mbaya wa maisha waliojijengea, kama vile kutokupata mlo mzuri, kupunguza muda wa kulala, yote haya yanaweza kusababisha hali hii ya ugonjwa.
Tafiti nyingi zinahitajika zaidi kwenye upande wa matatizo haya.Ila hali hii ni moja ya matatizo yanayokua zaidi kutokana na maendeleo ya teknolojia yanayotokea kila uchwao.
Matokeo ya hofu ya kutokuwa karibu na simu

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa mfano, kuwa na tabia mbaya ya kula, kupungua kwa wakati wa kupumzika, kujitenga na jamii, kushuka kiwango cha utendaji kwenye masomo na kazini.
Kwa mfano, ugonjwa wa ndani ya carpal (shinikizo kubwa kwenye neva kwenye mkono ambayo inaruhusu hisia na matumizi mengine sehemu za mkono) inaweza kukua zaidi.
Lakini pia hali nyingine za kiakili kama vile hofu ya kuchangamana kijamii, kutokuwa na utulivu na unyonge.
Ili kuzuia shida hii kuathiri ustawi wetu wa mwili na akili, ni muhimu kukuza programu za elimu kutoka utotoni ambazo zitajitolea kutoa elimu juu ya matumizi ya vifaa vya kisasa na athari zake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hii inamaanisha hitaji la kutekeleza uwezo wa kutosha wa digitali na mwamko mkubwa kuhusu utumiaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kwa upande mwingine, inashauriwa kuwa mtu anayehusika afanye uchambuzi wa kibinafsi wa wakati wa kila siku uliotumiwa kwa kutumia simu yake.
Katika tafakari hii, madhumuni ya matumizi yao yanapaswa pia kutathminiwa, na hivyo kuchambua tabia zao kwa ujumla.Kwa kujitambua, mhusika anaweza kuamua ikiwa anahitaji kujitathimini wakati anaotumia kwenye simu yake. Na, ikiwa ni lazima, ikiwa unahitaji msaada kutoka kwa mtu wa tatu.
Kwa hivyo, ikiwa unafikiria kuwa maisha yako ya kila siku yanaathiriwa na aina ya matumizi ya simu yako na hii inasababisha shida, inawezekana kuwa unategemea kifaa hiki ambacho kinaweza kusababisha madhara ikiwa hautasuluhisha mapema.












