Afghanistan: Tofauti kati ya Taliban na kikundi kipya cha wanamgambo wa ISIS

Chanzo cha picha, Getty Images
Taliban na ISIS wote ni Wasunni wenye itikadi kali, na wote wanataka kujenga nchi ambazo zinaongozwa kwa sheria ya Kiislamu na wako tayari kuafikia lengo hilo kwa kutumia ghasia.
Makundi haya mawili ni maadui, lakini kwa vyovyote vile yamekuwa yakipigana vikali tangu mwaka 2015 wakati ISIS ilipoanzisha tawi la Islamic State la jimbo la Khorasan (ISKP) nchini Afghanistan, katika wakati ambao kwa mara ya kwanza ISIS lililitaka kujiimarisha na kupanua maeneo yake nje ya Iraq na Syria.
Makundi haya mawili ni yapi ?
Taliban kwa mara ya kwanza ilijitokeza mwaka 1994 wakati wa vita vya kiraia vya Afghanistan , na wengi kati ya wanajeshi wake ni wanafunzi-ambao majina yao yana mizizi ya neno Pashto - wengi wao wakiwa ni wahamiaji walioshiriki katika vita vya upinzani vya na vikosi vya Usovieti katika miaka ya 1980.

Chanzo cha picha, Getty Images
Taliban,ikiongozwa na Mullah Mohammed Omar, kwa mara ya kwanza ilichukua udhibiti wa jimbo la Herat na baadae nchi nzima mwezi Septemba mwaka 1996, na kuushinda utawala wa Burhanuddin Rabbani, na kuanzisha Milki ya Kiislamu ya Afghanistan ambapo ilianzisha mji mkuu wa Kandahar.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uongozi wa shirika hilo wenye msimamo mkali ulisababisha mauaji ya kikatili ya wapinzani wao, ukilizuwia Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula kupeleka chakula kwa raia waliokumbwa na njaa, huku likiwakandamiza wanawake, jambo lililoufanya muungano unaaongozwa na Marekani kuachia mamlaka mwezi Disemba.
Shambulio la ndege lililomuua kiongozi wa al-Qaeda Osama bin kwenye kituo cha biashara cha dunia -World Trade Center cha New York, kiliwauwa watu 2,996 na kuwajeruhi wengine 25,000.
Tangu wakati huo, wapiganaji wa Taliban wamekuwa wakisanyika na kuwa waasi, na wamekuwa wakiendelea kuiteka Afghanistan na kuwaondosha walinda amani wa Marekani.
Kikundi cha The Islamic State kwa mara ya kwanza kilindwa na kiongozi wa Jihadiwa Jordan Abu Musab al-Zarqawi mwaka 1999 kabla ya kuwa maarufu wakati kilipochukua udhibiti wa miji muhimu ya mashariki mwa Iraq mwaka 2014.
Mwezi Januari 2015, kikundi hiki kiliunda kikundi kilichoitwa ISKP mashariki mwa jimbo la Afghanistan la Nangarhar, ambacho kimekuwa kikiwaajiri wapiganaji watoro wa Taliban, hususan wale ambao wamekasirika kwamba kiongozi wao hashindi vita.
Je ni vipi makundi haya mawili yanahusiana ?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuundwa kwa kikundi cha ISKP kulimfanya kiongozi wa Taliban Mullah Akhtar Mohamed Mansour kuandika barua kwa mwenzake wa ISIS , Abu Bakr al-Baghdadi, akimtaka aache kuwaajiri wakimbizi akidai kuwa mapigano yoyote yanayofanyika ndani ya Afghanistan. Yanapaswa kuwa chini ya uongozi wa Taliban.
Makabiliano makali yaliibuka kati ya pande hizi mbili mwezi Juni 2015 na mengine baina ya makundi hayo mawili yakatokea katika jimbo la Zabul mwezi wa Novemba , kwa misingi ya iwapo wanapaswa kujiunga na ISIS.
Je nini kinachoendelea kwa sasa?
Afghanistan iko katika msukosuko baada ya Taliban kuchukua mji mkuu Kabul, Jumapili , na kutangaza taifa la kiislamu tena baada ya rais Ashraf Ghani kuondoka kwenye kasri la rais na kuelekea Tajikistan.
Operesheni hiyo ilitokea baada ya vikosi vya Marekani kuanda kuondoka nchini humo mwezi uliopitakwa agizo la rais wa Marekani Joe Biden.
Kuondoka kwa vikosi vya Marekani na washirika wake kutoka Afghanistan kulikuja miaka 20 baada ya uvamizi ulioongozwa na Marekani ulioagizwa na aliyekuwa rais wakati huo W. Bush aliyeanzisha vita vya ugaidi baada ya mashambulio ya Septemba 11.

Chanzo cha picha, Reuters/Leah Millis
Rais wa Marekani Biden alirudia azma yake ya kurejesha jukumu la usalama wa Afghanstan na akaamini kuwa jukumu hilo linaweza kutekelezwa na jeshi la Afghanistan ambalo Marekani iliwekeza dola trilioni moja katika kipindi cha miaka 20 ya kukabiliana na Taliban.
"Ukweli ni kwamba tumevishuhudia vikosi hivi kuwa havijaweza kuilinda nchi- na hilo limedhihirika haraka kama ilivyotarajiwa ," Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alilalamika Jumapili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati wa ghasia mjini Kabul wakati watu walipokuwa wakitoroka kwenye uwanja wa ndege, wafungwa 5,000 walitoroka kutoka kwenye gereza la Pul-e-Charki kwenye ngome ya kijeshi ya Bagram, ambaya hivi karibuni ilikuwa ikishikiliwa na vikosi vya usalama. Marekani ilisema wapiganaji wa ISIS na al-Qaeda walikuwa ni miongoni mwa wale walioshikiliwa katika gereza hilo.












