Mapenzi, ngono na ndoa zilikuwaje katika Misri ya Kale?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ingawa unaweza kufikiria kwamba tabia ya Wamisri wa zamani ilikuwa tofauti sana na yetu, walikuwa na hofu na mashaka kama yetu kuhusu dhana za mapenzi, ngono na ndoa.
Tofauti ni kwa njia walivyoshughulikia hisia hizo.
Katika ulimwengu wa kisasa, "ngono inauza" na wakati mwingine inaweza kuzingatiwa kuwa bure au hata mwiko. Cha mwisho hicho ni jambo ambalo Mmisri wa kawaida wa zamani hangeelewa.
Kwa Wamisri, ngono ilikuwa nguzo muhimu ya maisha, pamoja na kula na kulala, na kwa hivyo sio kitu cha kucheka, kuaibika, au kukwepa.
Na kuizungumzia, lugha ya Misri, kama zile za kisasa, ilikuwa na maneno ya kisanii ya kutaja neno hilo la kujamiiana matamshi ambayo yangeweza kutumiwa kueleza kama vile "kushikamana na", "kukutana", "kutumia muda wa kupendana pamoja "," kuingia ndani ya nyumba "," kulala na "au" kufurahia.'
Kwa kweli, mashairi ni chanzo cha kushangaza cha kujifunza juu ya maswala ya mapenzi na libido katika Misri ya Kale.

Chanzo cha picha, Getty Images
Shairi la Ufalme Mpya, kwa mfano, linaelezea uhusiano wa kimapenzi kama "alinionyeshea rangi ya mkumbatio wake."
"Rangi" mara nyingi ilitumika kama tasifida ya ngozi, na katika mashairi tunapata misemo kama "kuona rangi ya viungo vyake vyote" au "rangi yake ilikuwa laini."
Ingawaje ngono ilikuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya kila siku, ilikuwa vyema katika mipaka ya ndoa, ndiyo sababu watu wengi walioa, mara nyingi wakiwa na umri mdogo.
Kwa kuwa mashairi ya mapenzi ya Ufalme Mpya yamejaa matamanio ya kingono na ya kimapenzi, na pia mapenzi yasiyoruhusiwa, tunapata dalili juu ya mazoea ya kitamaduni ya wakati huo kupitia mashairi.
Kwa mfano: "Hajui kuhusu hamu yangu ya kumkumbatia, au angeamuandika mama yangu", inaturuhusu kujua kwamba ikiwa kijana alitaka kuoa, anapaswa kuzungumza na mama ya msichana kupata ruhusa.
Shairi mpya la Ufalme linaelezea jinsi kazi rahisi haziwezekani kwa sababu ya upendo: "Haitaniruhusu nifanye lolote kwa busara."
Wanandoa walio katika mapenzi pia walipeana majina ya utani kama "Paka", "Anayetafutwa sana" na 'Yeye (ambaye) ni mkali kama chui'.
"Mwaka wa kula'

Chanzo cha picha, Getty Images
Harusi ilikuwa tukio jepesi , bila sherehe ya kidini au ya kiraia; kwakwaida mwanamke - ingawa mara kwa mara mwanamume - alihamia tu nyumbani kwa mumewe, labda akiandamana na msafara uliopita barabara na sherehe.
Bila chochote cha sherehe au rasmi, ndoa nyingi ziliachwa bila hati, lakini matajiri mara nyingi waliunda mikataba inayoelezea athari za kifedha za talaka.
Lakini za kufurahisha zaidi ni nyaraka zinazoelezea ndoa za muda au za majaribio:"Utakuwa nyumbani mwangu ukiwa nami kama mke kuanzia leo, siku ya kwanza ya mwezi wa tatu wa msimu wa baridi wa mwaka wa kumi na sita, hadi siku ya kwanza ya mwezi wa nne wa msimu wa mafuriko wa mwaka wa kumi na saba. "
Ndoa hii ya muda ilijulikana kama "kula kwa mwaka mmoja" na iliruhusu wanandoa hao kujaribu ndoa, na vile vile kuondoka haraka ikiwa hakutakuwa na watoto wakati huu au ikiwa wataamua haifanyi kazi.
Maisha ya ndoa huko Misri ya Kale hayakuwa tofauti sana na ilivyo leo, na wanandoa walikuwa na shida nyingi sawa: kimsingi kulea, kulisha, na kutoa makazi kwa familia zao.
Walakini, sio ndoa zote za Misri za Kale zilikuwa kamilifu na ushahidi wa kimatibabu unaonyesha kuwa wanaume mara nyingi waliwasiliana na daktari kwa ajili ya shida za tendo la ngono ndani ya ndoa zao.
Lakini wanaume na wanawake walizini, na wanaume na wanawake wanaweza kusababisha talaka kwa sababu ya hii.
Uzinzi ulikuwa wa kawaida sana hivi kwamba ulionekana katika Kitabu cha Wafu katika kile kinachoitwa 'Kukiri dhambi zako', ambapo marehemu alikanusha kufanya mambo ambayo yalionekana kuwa haramu au hayakubaliki kijamii.

Chanzo cha picha, Getty Images
Iwapo ushauri huo ungepuuzwa…
Ingawa talaka ilipeanwa kwa sababu ya uzinzi, ikiwa mume alitaka, angeweza kuuliza kwamba mke wake mzinifu aadhibiwe vikali, wakati mwingine na kukatwa au kuuawa.
Walakini, adhabu hizi kali kwa ujumla zilikuwa njama za hadithi za fasihi, na talaka ilikuwa rahisi na ya kawaida katika ulimwengu wa kweli.
Wanaume na wanawake wangeweza kumpa talaka mmoja kwa mwenzake, mwanamume akisema tu, "Nimekukosa", au mwanamke akisema, "Mimi nime..", au mwanandoa akisema "Nakutaliki."
Talaka kwa ujumla ilikuwa rahisi kama harusi, na mwanamke huyo alihama kutoka kwa nyumba ya mumewe, labda arudi nyumbani kwa baba yake au kwake.
Talaka haikuleta unyanyapaa wowote kijamii na wanaume na wanawake walioa tena na wengi walikuwa na familia kubwa.
Walakini, ikiwa mwanamke angeachana na mume wake wakati akiwa na umri wa miaka 30, ilikuwa nadra kwake kuolewa tena. Katika umri huo, alichukuliwa kuwa mzee.













