Uchaguzi wa Uganda 2021: Jinsi Museveni alivyoitawala Uganda miaka 35

Waganda wenye umri chini ya miaka 35 -wanamjua rais mmoja peke yake na zaidi ya robo tatu ya wakazi wa nchi hiyo ni vijana.

Yoweri Museveni, aliingia madarakani baada ya kutoka katika mapigano ya msituni mwaka 1986, na anatambulika kuwa kiongozi amedumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.

Rais huyo mwenye miaka 76, ameweza kulifanya taifa hilo kuwa na amani kwa muda mrefu na kuleta maendeleo ambayo wengi wanafurahia.

Lakini aliweza kuimarisha utawala wake kwa kuhamasisha utu na ushirikiano , kutoa ajira , kuruhusu kuanzishwa kwa taasisi huru na kuwatenga wapinzani.

Wakati wa uchaguzi uliopita, miaka mitano iliyopita wakati alipokuwa anazungumzia suala la kuachia ngazi, alihoji: "Ninawezaje kuacha ndizi katika mgomba, nilipanda hivyo napaswa kuanza kula matunda yake?"

Hivyo hajamaliza bado kuvuna.

Utangulizi wangu kwa rais unaanzia miaka ya 1990 katika michezo ya kuigiza shuleni , ambapo ghasia za Milton Obote na Idi Amin zilifanyiwa maigizo.

Ghasia ambazo rais Museveni alizitamatisha apoingia madarakani Januari 26, 1986 akiwa na chama chake cha National Reistance Army.

Museveni alitoa picha kubwa kwa raia wa Uganda kuwa mleta amani na anawakumbusha fursa alizoziibua.

Rais anatambulika kama baba na babu wa taifa hilo.

Vijana wengi wa Uganda wanamuita jina la utani la "Sevo", na akiwaita Bazukulu (maana yake ikiwa ni wajukuu).

Lakini mwanaume huyu wa familia bado anang'ang'ania kubaki katika kiti chake anachokipenda huku watoto na wajukuu zake wakihangaika.

Katika kampeni yake ya awamu ya sita, ambayo ni kama ilianza mara tu baada ya uchaguzi uliopita, alikuwa akifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya nchi , kuzindua viwanda, kufungua barabara na masoko mapya.

Na akiwa anamfuatilia kwa karibu mpinzani wake kijana mwenye umri wa miaka 38-ambaye ni mwanamuziki Bobi Wine, Bwana Museveni amekuwa akionesha nguvu zake.

Mwezi Aprili mwaka jana , alikuwa anahamasisha vijana kufanya mazoezi wakati wa marufuku ya kutoka nje , alipigwa picha akiwa nafanya mazoezi 'push up' ,na alirudia mbinu hiyo mara kadhaa ikiwa ni pamoja na alipofanya mazoezi mbele ya wanafunzi kuwafurahisha, mwezi Novemba.

"Kama baba yako anakupenda, inabidi akuwezeshe . Ndani ya miaka mitano ijayo 'Sevo' atahakikisha kuwa mkimaliza shule mnapata ajira, tunapata ajira," alisema Angela Kirabo mwenye umri wa miaka 25 akigusia suala la ajira kwa vijana ambalo ndio wengi wanalilalamikia.

Mwanafunzi mwingine aliyehitimu masomo ya uchumi anajivunia kuwa Muzukulu (mjukuu), kukua katika familia iliyotawaliwa na chama National Resistance Movement (NRM). Yeye anadhani kuwa rais Museveni bado ana mambo mengi mazuri ambayo anaweza kuifanyia Uganda baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35 .

Ukomo wa miaka

Mmoja wa marafiki wa karibu na mshauri wake, John Nagenda, anasema kujitolea kwa bwana Museveni ndio kunaimarisha utawala wake.

"Alikuwa amejiandaa kufa kwa ajili ya Uganda. Ninaweza kusema kuwa tuna bahati ya kuwa na kiongozi huyu," Nagenda mwenye umri wa miaka 82 anaeleza.

"Watu wengine wengi wanataka urais kwa ajili yao binafsi , lakini Museveni anataka kwa ajili ya nchi yake na bara la Afrika kwa ujumla ...yeye ni mwafika halisi."

Chini ya katiba ya mwaka 1995 rais alikuwa hatakiwa kuwania tena nafasi ya urais baada ya mwaka 2005.

Ingawa kabla ya hapo alikuwa hataki kubaki madarakani, na alikuwa hakubaliani na wazo la yeye kuendelea kuwa kiongozi na kusema kuwa atarudi shambani kwake.

Mwandishi William Pike, ambaye wakati fulani ambaye alionekana kuwa karibu sana na rais na chama cha NRA, alielezea jinsi rais alivyochukia alipoambiwa kama anataka kubaki kuongoza Uganda kwa maisha yake yote, mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1990.

"Museveni alisema 'Bila shaka siwezi', lakini alionesha wazi kuwa amechukizwa na swali hilo na kuona kama tusi kwake.

Hakuwa anatania au anaigiza. Wakati huo hakuwa na nia kabisa ya kubaki madarakani.," bwana Pike aliandika.

Lakini kuna kitu kilibadili mawazo yake mwaka 2004, ingawa hajawahi kuweka wazi ni jambo gani lililomsukuma kubadili katiba na kuondoa ukomo wa umri katika katiba.

Alikuwa na fursa ya kuwa kiongozi mpaka alipofika miaka 75 .

Na baadae Desemba mwaka 2017, kikwazo cha umri kikaondolewa kwa mgombea wa rais suala ambalo lilileta ghasia bungeni.

Wengi waliona kuwa suala hili linampa rais mwanya kuongoza maisha yake yote.

Baadhi ya changamoto

Mafanikio yake katika jamii,Ameweza kuleta maendeleo katika programu za maendeleo za wanawake,wachuuzi na ajia za serikali.

Katika taifa ambalo 15% ya vijana hawana ajira na zaidi ya 21% wanakabiliwa na umaskini, na kuhamia katika chama kingine kunaonekana kuwa kunaweza kuwaokoa katika umaskini.

Lakini wafuasi wake wameeleza kuwa mabadiliko yanaweza kuja kama pale ambapo bwana Museveni akipewa miaka mingine mitano ya ziada.

Ukizungumzia suala la wasiwasi wa ajira, NRM imeweza kubadili uchumi wa Uganda kukua si ndani ya nchi tu bali duniai kote".

Licha ya mabadiliko ambayo anayo yanaathiri uhuru wa baadhi ya taasisi katika taifa hilo.

Hivi karibuni mahakama hakijawa chombo huru , kimejikuta kuwa kinafuata matakwa ya serikali.

Kwa mfano Desemba 16 mwaka 2005, wanajeshi wenye mafunzo ya hali ya juu walipelekwa katika mahakama kuu mjini, Kampala, na kuwakamata tena washukiwa wa uasi kwa makosa mengine ya uhaini.

"Waligeuza kuwa ukumbi wa vita ," James Ogoola aliandika mashairi kuhusu tukio hilo

Ikija kwenye upande wa mashindano ya matokeo ya uchaguzi , matokeo ya urais tangu mwaka 2001 yalikuwa yanaishia mahakamani.

Vyombo vya habari pia havijawa huru kutoa taarifa.

Kumekuwa na matukio ya waandishi kushikiliwa na vyombo vya usalama

Vyombo vya habari vingi viko chini ya rais Museveni hivyo ni ngumu kuripoti kwa usawa.

Wafuasi wa upinzani kupigwa risasi na kuuawa

Ilianza kuwa wazi miaka 20 iliyopita kuwa anataka kubaki madarakani, mara baada ya washirika wake kuanza kujiondoa katika chama.

Wapinzani wake wamekuwa wakiteswa na vyombo vya usalama.

Kizza Besigye kutoka chama cha jukwaa la mabadiliko ya kidemokrasia , aliwania kwa mara ya kwanza dhidi ya Museveni katika uchaguzi wa mwaka 2001.

Alishikiliwa na vyombo ya usalama, kuchunguzwa na kushutumiwa mashtaka kadhaa pamoja na ubakaji lakini hakuwahi kuwekwa hatiani.

Na sasa Bobi Wine, muimbaji ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, amekumbana na changamoto kadhaa na askari.

Mbunge huyo ambaye nyota aliyeweza kuvuta umati mkubwa wa vijana , alikumbana na maswaibu kadhaa katika kampeni zake.

Katika kampeni zake polisi walimkamata na kumfunga, wafuasi wake walipigwa mabomu ya machozi na kupigwa risasi kwa kuwa walikwa wanaenda kinyume na masharti dhidi ya corona.

Wakati wa kampeni , waandamanaji 54 waliuawa wakati Bobi Wine aliposhikiliwa na polisi na wengine wengi wanaaminika kuwa walipiwa risasi.

Kwa miaka 35 madarakani, amekuwa na mamlaka ya kitu.

Wakati yeye pia aliingia madarakani akiwa na miaka 40 katika jukumu hilo sasa iweje mtu mwenye umri kama wake kuchukua madaraka kuwa jambo la hatari.