Waganda wenye umri chini ya miaka 35 -wanamjua rais mmoja peke yake na zaidi ya robo tatu ya wakazi wa nchi hiyo ni vijana.
Yoweri Museveni, aliingia madarakani baada ya kutoka katika mapigano ya msituni mwaka 1986, na anatambulika kuwa kiongozi amedumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.
Rais huyo mwenye miaka 76, ameweza kulifanya taifa hilo kuwa na amani kwa muda mrefu na kuleta maendeleo ambayo wengi wanafurahia.
Lakini aliweza kuimarisha utawala wake kwa kuhamasisha utu na ushirikiano , kutoa ajira , kuruhusu kuanzishwa kwa taasisi huru na kuwatenga wapinzani.
Wakati wa uchaguzi uliopita, miaka mitano iliyopita wakati alipokuwa anazungumzia suala la kuachia ngazi, alihoji: "Ninawezaje kuacha ndizi katika mgomba, nilipanda hivyo napaswa kuanza kula matunda yake?"
Hivyo hajamaliza bado kuvuna.
Utangulizi wangu kwa rais unaanzia miaka ya 1990 katika michezo ya kuigiza shuleni , ambapo ghasia za Milton Obote na Idi Amin zilifanyiwa maigizo.
Ghasia ambazo rais Museveni alizitamatisha apoingia madarakani Januari 26, 1986 akiwa na chama chake cha National Reistance Army.
Museveni alitoa picha kubwa kwa raia wa Uganda kuwa mleta amani na anawakumbusha fursa alizoziibua.
Rais anatambulika kama baba na babu wa taifa hilo.
Vijana wengi wa Uganda wanamuita jina la utani la "Sevo", na akiwaita Bazukulu (maana yake ikiwa ni wajukuu).
Lakini mwanaume huyu wa familia bado anang'ang'ania kubaki katika kiti chake anachokipenda huku watoto na wajukuu zake wakihangaika.
Katika kampeni yake ya awamu ya sita, ambayo ni kama ilianza mara tu baada ya uchaguzi uliopita, alikuwa akifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya nchi , kuzindua viwanda, kufungua barabara na masoko mapya.
Na akiwa anamfuatilia kwa karibu mpinzani wake kijana mwenye umri wa miaka 38-ambaye ni mwanamuziki Bobi Wine, Bwana Museveni amekuwa akionesha nguvu zake.
Mwezi Aprili mwaka jana , alikuwa anahamasisha vijana kufanya mazoezi wakati wa marufuku ya kutoka nje , alipigwa picha akiwa nafanya mazoezi 'push up' ,na alirudia mbinu hiyo mara kadhaa ikiwa ni pamoja na alipofanya mazoezi mbele ya wanafunzi kuwafurahisha, mwezi Novemba.
"Kama baba yako anakupenda, inabidi akuwezeshe . Ndani ya miaka mitano ijayo 'Sevo' atahakikisha kuwa mkimaliza shule mnapata ajira, tunapata ajira," alisema Angela Kirabo mwenye umri wa miaka 25 akigusia suala la ajira kwa vijana ambalo ndio wengi wanalilalamikia.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Wafuasi wa Museveni wana amini kuwa bado ana mambo mengi ya kuifanyia kazi Uganda
Mwanafunzi mwingine aliyehitimu masomo ya uchumi anajivunia kuwa Muzukulu (mjukuu), kukua katika familia iliyotawaliwa na chama National Resistance Movement (NRM). Yeye anadhani kuwa rais Museveni bado ana mambo mengi mazuri ambayo anaweza kuifanyia Uganda baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35 .
Ukomo wa miaka
Mmoja wa marafiki wa karibu na mshauri wake, John Nagenda, anasema kujitolea kwa bwana Museveni ndio kunaimarisha utawala wake.
"Alikuwa amejiandaa kufa kwa ajili ya Uganda. Ninaweza kusema kuwa tuna bahati ya kuwa na kiongozi huyu," Nagenda mwenye umri wa miaka 82 anaeleza.
"Watu wengine wengi wanataka urais kwa ajili yao binafsi , lakini Museveni anataka kwa ajili ya nchi yake na bara la Afrika kwa ujumla ...yeye ni mwafika halisi."
Chini ya katiba ya mwaka 1995 rais alikuwa hatakiwa kuwania tena nafasi ya urais baada ya mwaka 2005.
Ingawa kabla ya hapo alikuwa hataki kubaki madarakani, na alikuwa hakubaliani na wazo la yeye kuendelea kuwa kiongozi na kusema kuwa atarudi shambani kwake.
Maelezo ya video, Kura za vijana zinaweza kumpa ushindi Bobi Wine?
Mwandishi William Pike, ambaye wakati fulani ambaye alionekana kuwa karibu sana na rais na chama cha NRA, alielezea jinsi rais alivyochukia alipoambiwa kama anataka kubaki kuongoza Uganda kwa maisha yake yote, mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1990.
"Museveni alisema 'Bila shaka siwezi', lakini alionesha wazi kuwa amechukizwa na swali hilo na kuona kama tusi kwake.
Hakuwa anatania au anaigiza. Wakati huo hakuwa na nia kabisa ya kubaki madarakani.," bwana Pike aliandika.
Lakini kuna kitu kilibadili mawazo yake mwaka 2004, ingawa hajawahi kuweka wazi ni jambo gani lililomsukuma kubadili katiba na kuondoa ukomo wa umri katika katiba.
Alikuwa na fursa ya kuwa kiongozi mpaka alipofika miaka 75 .
Na baadae Desemba mwaka 2017, kikwazo cha umri kikaondolewa kwa mgombea wa rais suala ambalo lilileta ghasia bungeni.
Wengi waliona kuwa suala hili linampa rais mwanya kuongoza maisha yake yote.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Kauli mbiu ya rais, kulinda siku zijazo
Baadhi ya changamoto
Mafanikio yake katika jamii,Ameweza kuleta maendeleo katika programu za maendeleo za wanawake,wachuuzi na ajia za serikali.
Katika taifa ambalo 15% ya vijana hawana ajira na zaidi ya 21% wanakabiliwa na umaskini, na kuhamia katika chama kingine kunaonekana kuwa kunaweza kuwaokoa katika umaskini.
Lakini wafuasi wake wameeleza kuwa mabadiliko yanaweza kuja kama pale ambapo bwana Museveni akipewa miaka mingine mitano ya ziada.
Ukizungumzia suala la wasiwasi wa ajira, NRM imeweza kubadili uchumi wa Uganda kukua si ndani ya nchi tu bali duniai kote".
Licha ya mabadiliko ambayo anayo yanaathiri uhuru wa baadhi ya taasisi katika taifa hilo.
Hivi karibuni mahakama hakijawa chombo huru , kimejikuta kuwa kinafuata matakwa ya serikali.
Kwa mfano Desemba 16 mwaka 2005, wanajeshi wenye mafunzo ya hali ya juu walipelekwa katika mahakama kuu mjini, Kampala, na kuwakamata tena washukiwa wa uasi kwa makosa mengine ya uhaini.
"Waligeuza kuwa ukumbi wa vita ," James Ogoola aliandika mashairi kuhusu tukio hilo
Ikija kwenye upande wa mashindano ya matokeo ya uchaguzi , matokeo ya urais tangu mwaka 2001 yalikuwa yanaishia mahakamani.
Vyombo vya habari pia havijawa huru kutoa taarifa.
Kumekuwa na matukio ya waandishi kushikiliwa na vyombo vya usalama
Vyombo vya habari vingi viko chini ya rais Museveni hivyo ni ngumu kuripoti kwa usawa.
Wagombea wa urais nchini Uganda
Taaluma: Mhandisi, Mwanasiasa
Umri: 57
Mwaka 1994, Patrick Oboi Amuriat aliwania ubunge. Kati ya 2001 na 2016, alikuwa mbunge wa alikuwa mkosoaji mkubwa kuhusu kuondolewa kwa ukomo wa muhula wa urais.
Amuriat amesoma Chuo Kikuu cha Makerere ambapo alipata shahada yake ya kwanza na ya pili katika Uhandisi wa Ujenzi. Amefanya kazi na makampuni kadhaa ya uhandisi nyumbani na ugenini, mashirika ya maenedeleo ya kijamii pamoja na kuwa mtumishi wa umma kama mhandisi wa wilaya.
Alikuwa miongoni mwa jopo la bunge ambalo liliunda chama cha Forum for Democray (FDC). Ni rais wa tatu wa chama cha FDC.
Taaluma: Mwandishi wa michezo, mchungaji
Umri: 48
Joseph Kiza Kabuleta ni kiongozi wa vuguvugu la Kupigania taifa na raia (ROCK)
Ukosoaji wake wa utawala wa chama tawala cha NRM ulimfanya kufungwa jela 2019. Alisema kwamba mateso aliopitia katika mikono ya vyombo vya usalama akiwa jela yalimfanya kumpinga rais Museveni katika kinyang’anyiro cha urais mwaka huu.
Kabuleta alifanya kazi kwa muda mfupi kama msimamizi katika majengo mjini kampala na ana cheti cha diploma katika uhandisi alichokipata baadaye miaka ya tisini, kisha alibadilisha taaluma na kuanza kuwa mwandishi wa michezo na alifanya kazi kama mwandishi katika kampunu ya The Crusader, kabla ya kujiunga na gazeti la The New Vision ambapo alikuwa mwandishi maarufu wa safu.
Baada ya kuondoka katika chumba cha habari 2016, alikuwa mchungaji kiongozi katika kanisa la watchman Ministries.
Taaluma: Mwandishi wa habari, Mtaalamu wa masuala ya fedha
Umri: 40
Nancy Linda Kalembe ndiye mwanamke wa pekee anayewania urais katika uchaguzi wa mwaka 202.
Ahadi yake kuu ya kampeni ni kuimarisha maisha ya wanawake, uchukuzi, miundo mbinu na biashara za jamii.
Nancy kalembe ana Shahada ya Sayansi katika masuala ya Idadi ya Watu kutoka Chuo Kikuu cha Makerere.
Taaluma: Hana ajira
Umri: 24
John Katumba ni mgombea mwenye umri mdogo zaidi katika kinyang'anyiro cha urais nchini Uganda. Ameweza kugombea baada ya kuondolewa kwa umri wa urais kufuatia marekebisho ya kikatiba yaliofanywa mwaka 2017.
Alifuzu kutoka chuo kikuu cha Makerere kitivo cha biashara mwezi Januari 2020 akipata shahada ya uchukuzi na mipangilio.
Ijapokuwa bado hajatoa ilani ya uchaguzi, Katumba ameahidi kuangazia ukosefu wa ajira na kuwawezesha wanawake.
Taaluma: Wakili, Mwanasiasa
Umri: 53
Norbert Mao amehudumu kama mbunge aliyechaguliwa katika jimbo la Gulu kwa awamu mbili kati ya 1996 na 2006.
Baadaye, alikua mwenyekiti wa mojawapo ya mabaraza katika wilaya ya Gulu ambapo ni wakati alipohusishwa kuwa mpatanishi kati ya waasi wa kundi la wapiganaji wa LRA na serikali ya Uganda. Alipigania sheria ya kutoa msamaha kama sheria muhimu ambayo ingesaidia katika kusitisha vita hivyo kwa amani kaskazini mwa Uganda.
Mwaka 2010, kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa rais wa chama cha Democratic Party, Mao alipigania urais wa Uganda katika uchaguzi wa 2011.
Mao ana shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Makerere ambapo alihudumu kama rais wa chama cha wanafunzi.
Taaluma: Mhandisi, Mtaalamu wa kilimo
Umri: 33
Mwaka 2016, Willy Mayambala alipigania kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama cha Forum for Democratic Change na kupoteza.
Ana Shahada ya Sayansi na Teknolojia kutoka Chuo Kikuu cha Kyambogo aliyoipata 2010. Baada ya kupata shahada, Mayambala alijiunga na mmoja ya wanafunzi wenzake kuanzisha kampuni ya Kamol Engineering Services Ltd na baadaye kuondoka miaka michache baadaye ambapo aliunda kamapuni yake binfasi JohnSemp Ltd.
Baba yake ambaye ni marehemu John Ssempala alikuwa alikuwa ni moja ya wapiganaji wa vita vya msituni vya 1980 hadi 1985 ambavyo vilimpatia madaraka rais Museveni.
Taaluma: Meja Jenerali Mstaafu , Mwanasiasa
Umri: 62
Meja Jenerali mstaafu Gregory Mugisha ndio rais na mgombea wa urais wa chama cha Alliance for National Transformation.
Muntu alikuwa mwanachama wa zamani wa kundi la waasi la NRA na alihusika pakubwa katika ufanisi wake kutokana na sifa yake ya kujitolea , utiifu na uwajibikaji.
Kufuatia ushindi wao 1996, Muntu alianza kwa kuongoza kitengo cha ujasusi wa kijeshi. Alikuwa kamanda wa kitengo maalumu cha jeshi 1989. Alishikilia wadhfa huo kwa miaka tisa hadi alipotofautiana na mkuu wa majeshi yote rais Yoweri Museveni 1989.
Ijapokuwa alimpatia wadhifa wa uwaziri Muntu alikataa wadhifa huo.
Alikuwa mbunge katika Bunge la Katiba la 1994-1995 ambalo lilijadili katiba ya Uganda. Mwaka 2021 Muntu alichaguliwa kuwa kamammoja ya wawakilishi wa Uganda katika bunge la Afrika Mashariki.
Taaluma: Rais wa Uganda
Umri: 76
Yoweri Kaguta Tubuhrburwa Museveni amekuwa rais wa Uganda tangu 1986 kufuatia uasi wa miaka mitano alioongoza dhidi ya uatawala wa awamu ya pili wa Apollo Milton Obote.
Aliahidi kuongoza kwa miaka minne pekee lakini sasa amefanya mabadiliko ya kikatiba mara mbili ili kumsaidia kusalia madarakani. Mara ya kwanza alihusika katika kubadilisha katiba 2005 ili kuondoa kikomo cha urais ili kumwezesha kuwania tena urais 2006 licha ya kuahidi hadharani 2001 kwamba hangewania urais tena.
Harakati zake za kuwania urais 2021 ziliwezeshwa kupitia marekebisho ya kikatiba mwaka 2017 kuondoa umri wa kikomo cha kuwania urais ambapo maafisa kutoka kikosi chake cha ulinzi walivamia bunge na kuwatoa nje viongozi waliokuwa wakipinga marekebisho hayo hadi pale yalipopitishwa.
Kabla ya sheria hiyo kupitishwa raia wa Uganda walio chini ya umri wa miaka 18 ama wale walio na zaidi ya umri wa miaka 75 walikuwa hawawezi kuwania urais.
Taaluma: Mchungaji
Umri: 38
Fred Mwesigye ameshikilia wadhifa wa mchungaji na mchungaji mshiriki katika kanisa la House of God Worship Ministry International, kanisa la God World Missions huko Kamwokya, Kampala na mchungaji kiongozi katika eneo la Kitoro mjini Entebe ambalo alilianzisha 2017.
Mwaka 2019, aliamua kujiunga na siasa ili kuitikia 'wito wa Mungu' kuiokoa Uganda kutoka kwa matatizo kwa kile ambacho anakiita enzi mpya ya mapenzi.
Ahadi yake kuu ni kuongeza mishahara ya walimu na madaktari pamoja na kuzuia kuparaganyika kwa taifa hilo 'kunakosababishwa' na chama tawala cha NRM, mathalan anataka kupunguza wilaya kutoka 135 hadi 62.
Taaluma: Mwanamuziki, mjasiriamali
Umri: 38
Robert Kyagulani Ssentamu, kwa jina maarufu Bobi Wine, ni mwanamuziki maarufu, msanii na mjasiriamali. Alianza kufanya muziki mapema miaka ya 2000 na kujitofautisha katika muziki wake aina ya dance hall kwa kuuchanganya na jumbe za masuala yanayokumba jamii.
Juni 2017, alipigania ubunge katika uchaguzi mdogo na kushinda kwa wingi wa kura dhidi ya chama tawala cha NRA na chama cha Forum for Democratic Change FDC.
Ijapokuwa kwa sasa anaongoza chama cha National Unity Platform (NUP), Kyagulani bado ni maarufu na na kundi la Nguvu ya Umma, vuguvugu aliloanzisha kupitia kampeni ya kutoondolewa kwa sheria ya ukomo wa umri wa kuwania urais.
Kyagulani katika siku za hivi karibuni amepata umaarufu mkubwa akionekana kuwa mpinzani mkuu wa rais Museveni katika uchaguzi wa urais wa 2021.
Taaluma: Wakili, Luteni Jenerali mstaafu
Umri: 61
Luteni Jenerali mstaafu Henry Tumukunde ni wakili ambaye aliipata Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Makerere 1981. Pia ana stashahada katika usimamizi wa mafuta na gesi kutoka Chuo cha Geneva.
Ni mbunge wa zamani wa chama tawala cha NRA tangu mwaka 1996, amehudumu kama katibu na mwambata wa kijeshi katika ubalozi wa Uganda nchini Uingereza , mkurugenzi wa mipango na usimamizi katika jeshi, mkuu wa idara ya ujasusi jeshini, kamanda wa kitengo cha nne cha jeshi kaskazini mwa Uganda na mkurugenzi mkuu wa shirika la usalama wa ndani.
Mwaka 2015, Tumukunde alistafaishwa kutoka jeshini akiwa katika wadhifa wa Luteni Jenerali na akarudishwa kuhudumu kama waziri wa masuala ya usalama kati ya 2016 na 2018.
Wafuasi wa upinzani kupigwa risasi na kuuawa
Ilianza kuwa wazi miaka 20 iliyopita kuwa anataka kubaki madarakani, mara baada ya washirika wake kuanza kujiondoa katika chama.
Wapinzani wake wamekuwa wakiteswa na vyombo vya usalama.
Kizza Besigye kutoka chama cha jukwaa la mabadiliko ya kidemokrasia , aliwania kwa mara ya kwanza dhidi ya Museveni katika uchaguzi wa mwaka 2001.
Alishikiliwa na vyombo ya usalama, kuchunguzwa na kushutumiwa mashtaka kadhaa pamoja na ubakaji lakini hakuwahi kuwekwa hatiani.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mgombea wa urais Bobi Wine ameungwa mkono na vijana
Na sasa Bobi Wine, muimbaji ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, amekumbana na changamoto kadhaa na askari.
Mbunge huyo ambaye nyota aliyeweza kuvuta umati mkubwa wa vijana , alikumbana na maswaibu kadhaa katika kampeni zake.
Katika kampeni zake polisi walimkamata na kumfunga, wafuasi wake walipigwa mabomu ya machozi na kupigwa risasi kwa kuwa walikwa wanaenda kinyume na masharti dhidi ya corona.
Wakati wa kampeni , waandamanaji 54 waliuawa wakati Bobi Wine aliposhikiliwa na polisi na wengine wengi wanaaminika kuwa walipiwa risasi.
Kwa miaka 35 madarakani, amekuwa na mamlaka ya kitu.
Wakati yeye pia aliingia madarakani akiwa na miaka 40 katika jukumu hilo sasa iweje mtu mwenye umri kama wake kuchukua madaraka kuwa jambo la hatari.