Halima Aden: Mtu yeyote asiniambie nivae nini au nifanye nini?

Chanzo cha picha, Fadil Berisha
Halima Aden ni miongoni mwa wanamitindo wa kwanza duniani kuvaa Hijabu.
Yeye ni mkimbizi mwenye asili ya Somalia na Marekani kutoka Kenya, Halima ameiambia BBC jinsi anavyojitahidi kutafuta usawa kati ya uwanamitindo na dini yake ya kiislamu.
Amesema ''Mwanamke yoyote hatakiwi kulazimishwa kuvaa hijabu wala kulazimishwa kuivua.''
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 22 ameingia katika tasnia ya ulimbwende wakati alipokuwa mwanamitindo wa kwanza kuvaa vazi la hijabu kuonekana katika majarida makubwa kama 'Vogue na Sports Illustrated', huku akitembea katika matamasha mengi akiwakilisha makampuni mbalimbali kama vile 'Yeezy na Max Mara'.
Kusherehekea uamuzi wangu
''Nasherehekea uamuzi wangu wa kuvaa hijabu. Sijawahi hata siku moja kumlazimisha mtu akubalianae na uamuzi wangu au avae kama ninavyovaa mimi'' amesema Halima ambaye kwa sasa ni mwanamitindo anayelipwa kiasi kikubwa cha fedha.
Mwandishi wa BBC, Urusi Alina Isachenka anasimulia jinsi alivyokutana na mlimbwende huyo.
Mara ya kwanza nilikutana na Halima nyuma ya tamasha fulani mjini Instanbul.
Amejifunika kote, alikuwa amevaa vazi refu lenye urembo urembo na Hijabu nyeusi.

Chanzo cha picha, AFP
Halima ana urefu wa cm 165 ambao ni kiwango cha juu cha urefu wa mwamitindi wa kawaida.
Akisindikizwa na meneja wake wa kike na mlinzi, Halima anaanza kuzungumza na yoyote atake pita mbele yake na kupiga picha aina ya 'selfie' pamoja na kupiga picha na waandaaji wa tamasha.
''Usijibadilishe. Badilisha mchezo'' amesema Halima.
Lengo kuu ni kutengeneza nafasi kwa wanawake wenye dini ya kiislamu sehemu mbalimbali duniani, ili sauti zao zisikike.
Mashindano ya urembo

Chanzo cha picha, Getty Images
Anabaki kuwa mkweli katika hilo.
Ni binti anayejua kutafuta mafanikio.

Chanzo cha picha, Getty Images
Halima alikuwa mshiriki wa kwanza kuvaa Hijab katika mashindano ya urembo ya Miss Minnesota nchini Marekani.
Hakushinda shindano hilo, ila lilimwezesha kujua zaidi kuhusu vazi la kuogelea linaloziba mwili mzima huku likimruhusu kutembea kwa uhuru zaidi.
''Nilikuwa nataka kurudi na kuwaambia wanawake wengine kuhusu bikini. Niwaeleze kuwa wanaweza kwenda kuogelea na kushiriki katika michezo.''

Chanzo cha picha, Sherri Hill
Baada ya muda mfupi tu aliweza kusaini mkataba na moja ya makampuni makubwa ya mitindo, 'IMG Models'.
Dini ya Halima inamaanisha hawezi kuonesha sehemu yoyote ile ya mwili wake, kasoro uso, mikono na miguu yake .

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kwangu kuwa mwanamitindo ninayevaa hijab-kuwa mwanamitindo wa mavazi ya kiislamu, ni jambo muhimu sana," alisema.
"Hivyo wabunifu na watu ninaofanya nao kazi huwa wanazingatia kunipa sehemu ya faragha katika kazi yangu."
"Kama wabunifu hawawezi kuniandali sehemu ya kuvaia ya peke yangu, huwa niko tayari kuondoka na kutoshiriki maonyesho."
Kuna uhuru wa kuchagua
Halima ni mhamasishaji wa uhuru wa kuchagua nini ambacho mwanamke anapaswa kukivaa.

Chanzo cha picha, WireImage
"Ninaamini kuwa kama mwanamke anaamini kuwa akivaa bikini na anajiona anavutia na yuko huru basi hakuna neno. Na hiyo ni sawa na mimi kuvaa hijabu na kujiona kuwa navutia na huru."
Anawavutia wengi
Halima anajivunia kuwa balozi wa shirika la watoto Unicef, ambapo ameweza kuzunguka maeneo mbalimbali duniani.

Chanzo cha picha, Future Productions, LLC
Halima amekuwa ana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii pia.
Kila picha anayoweka huwa inapendwa na maelfu ya watu na kupata maoni mamia.
Huwa anapenda kuweka picha zake kwenye mtando wa Instagram.

Chanzo cha picha, Halima Aden
Halima anatamani siku moja mama yake ahudhurie maonyesho yake makubwa.
Licha ya kuwa anafanya vizuri katika tasnia ya ulimbwende, lakini bado baadhi ya watu hawakubaliani na kile anachokifanya.













